Nampenda sana na inanitesa sana

Nampenda sana na inanitesa sana

Swali, unataka mke wa kuoa au tamaa za mwili tu.? Umesema unasoma, Vipi mpango wa shule.? Vipi unayo hela wewe? Je, unadhani utamuweza kweli kama mtoto mwenyewe anajitambua, umesema ww sio maneno yangu kuwa ni mtoto wa kishua. Mkuu nifupishe tu soma kwa bidii, tafuta mkwanja, jenga life kwanza. Mapenzi bila hela utarudi unalialia siku moja. Pole sana
Asante mkuu, barikiwa.
 
Asante mkuu, umenikumbusha msemo wa usemao time is always right to do what is right.
You are the victim of your own feelings. Ukitaka amani ni uweze kumudu hizo hisia zako. Kila kitu uko nacho wewe. If you get hurt its on you not her. Yeye umempa proposal mara kibao na kakataa, which is fair. Habari za kuspeculate on what she does with her life, ni mateso makubwa sana kwa upande wako. Get hold of your feelings now na uendelee na maisha. Love will come when its time. Kwanza hayo mapenzi ya chuo most of the times hayalipi bro, fanya maisha.
 
Asante mkuu
Futa namba yake haraka na chats zenu zote. Ugulia wiki nzima alafu endelea na maisha. Atakutafutaga tu kwa wakati wake. Nina experience na hiyo kitu

Ukiwa katika situations kama hizo usipende njia itakayokufariji au kukufurahisha, penda njia itakayokupa matokeo unayoyataka.

Matokeo unayoyataka ni kuwa mke wako. Lenga hilo kwanza usitumie nguvu nyingi kwenye kujifariji
 
Mkuu maturity inaanzia miaka mingapi? Kwa uzoefu wako, maana now I'm 27
Laiti ungeyajua haya maisha kwa jicho kama lakupevuka wala usingethubutu kusema unamalengo unataka kumuoa

wote tumepita uko mku so pambana tu na hali yako ila ukivuka apo ukaja kwenye maturity utajicheka juu ya huo mkasa
 
Habari wakuu, ID hii ni mpya lakini mimi ni mwenyeji humu ndani, nimeamua kutumia ili kuepusha baadhi ya mambo.
Wakuu naamini ushauri wenu utanisaidia sana ndio maana nipo hapa. Ipo hivi:

Mwezi July katika mishe zangu nilikutana na mtoto mmoja mkali (wana duka) basi siku ya kwanza tu kumuona nikampenda sana, (mimi sio play boy mzee wa chapa ilale) nakumbuka toka nilivyoachana na girl friend wangu 2013 nilikua single (sio domo zege) maana kama ningeamua kua na mahusiano ningetaka sababu mpaka sasa kuna watoto watatu hivi wananielewa na wanalilia mapenzi yangu (sijisifu ni ukweli mtupu) lakini sijakua nao sababu nahitaji mwanamke mmoja wa kutulia nae kuanza maisha.

Basi yule mtoto dukani pale kila siku nikawa naenda (siku nyingine namkuta, siku nyingine mdogo ake, au dada yake au kaka yake) basi siku nisipomkuta nikamkuta kesho yake nikawa napiga nae story kufidia (wazazi wake wana maisha ya kizungu hawana noma mara kibao wamenikuta naongea na dogo hawaja mind) basi imeenda tukazoeana sana, hatimaye dogo akanipa namba, tukaanza ku chat kila siku kwa sms/whatsapp muda wote, usiku pia tunaenda mpaka saa sita saa saba. Basi katika ku chat na kuwasiliana nikajikuta nazidi kumpenda sana dogo, nae nahisi hivyo, mwanzo alikua anitafuti mpaka nianze mimi lakini tulienda mpaka nae akawa huru kunitafuta, muda mwingi akawa ananianza yeye, basi wakuu nikajiona bahati nzuri hiyo upande wangu.

Huyu mtoto anajielewa sana, narudia tena anajielewa, sikua na lengo la kumchezea, bali nilitumia ujanja wote kufanya juu chini kuomba dating lakini wapi dogo alinichomolea, pia kwenye issue ya mahusiano akanichomolea, lakini bado tunawasiliana kila siku asubuhi-usiku.
Kila nikimueleza kuhusu mahusiano anakataa kabisa, basi nikaamua kumtafuta dada yake nikaomba aniambie ukweli kuhusu mdogo ake, dada ake akaniambia hajui kama dogo ana mtu ama laah ila dogo hua hamfichi mambo yakekama angekua nae angeshajua.

Basi kila mtu akaenda field, wote tupo vyuo, huko nako dogo tukawa tunawasiliana sana, cha ajabu nikiomba hata picha dogo ananinyima, whatsapp tu hajaweka dp wala status, insta nako hajaweka picha hata profile pic hamna, indicators kibao zinazoonyesh dogo anajielewa zikanivuta sana kwake, nikakaza bado dogo akawa anakataa anadai ana mtu, basi nikawa najiuliza kama ana mtu ulimwengu huu mwanaume unaachaje mwanamke wako atumie karibi siku nzima kuwasiliana na mwanaume mwingine, maana dogo kila siku nipo nae whtsapp hadi usiku na interval ya ku reply ni dk 2.

Sasa majuzi nikiwa whatsapp nikamcheki dogo, mh sio kawaida ile meseji ya kwanza hakua amenijibu, nilivyomcheki ilipita dakika 6 ndio akaisoma, akanijibu basi nika reply, dakika 20 dogo yupo online haku reply, mh nikajua hapa kuna mwanaume mwingine ana chat nae labda nisubiri zamu yangu kesho, kesho inafika saa 2 asubuhi dg yupo online, hajanijibu, nikasepa offline, nakuja kufungua saa 6 mchana yupo online ajanibu, siku ya kwanza, ya pili ya tatu mpaka leo tunaenda siku ya 6 dogo ajanijibu, wakuu huyu mtoto nampenda sana naona ana kila sifa za kua wife material lakini najiuliza kwanini yupo online na hanijibu, kila siku hadi saa tano, saa sita usiku.

Natamani nimuanze tena lakini naogopa, wazungu wanasema not getting a message is also a message, kila nikiandika ujumbe nimtumie naishia kuufuta, nimebaki njia panda, roho inaniuma kumuona mtoto online muda wote, attention na mimi hana tena, na wala sijamkosea lolote, nampenda sana na laiti angejua malengo yangu kua sitaki kumchezea angetulia na mimi

Naombeni mnishauri wakuu nifanye nini, moyo wangu ni sensitive sana,, siku mbili sijalala wala kwenda class, kiukweli hili jambo limeniumiza sana, sana , sana.
_ _ _ F_ nakupenda sana usinitese tafadhali.

ASANTENI WAKUU, NAWASILISHA.
Why uendelee kuumia acha kujifanya mwambaa, mtafute muulize nini tatizo. Usijiumize bure.
 
Mkuu every one has got his own timeline ,, every man has his own decision to decide his destination,, namaanisha everything is a choice kama mtu fulani alichelewa kumfikia wife material wake hai guarantee mwingine pia nae atachelewa. Mwaka wa 4 Uhandisi wa kilimo
Ni vizuri ukiwa positive minded mzee baba...Ila save nayokuambia.
 
Inaonekana umeonesha mapepe mengi sana kwenye kumtaka, au pengine chats zako zinakuwa ni zile zile kwahy anakuwa bored. Acha kumchatisha pia ji keep busy tu kwa mda.
Kama anapokea sim mpigie umsalimie na kumjualia hali alf umuage mapema... Yan unakuwa mrahisi sana ndo shida
Ukiona pia hana time na wewe temana nae mapenzi haya lazimishwi
Oooyooo,hapa habari imeisha
 
Sio kila kitu tunachokipenda tunatakiwa kuwa nacho. Kubaliana na ukweli kuna mwenzio ameshauwin moyo wa dogo. Unavyoendelea kulazimisha anaweza akakubali jamaa akimzungua halafu wewe ukaweka ndani kabisa. Siku anaempenda akirudi utatuletea thread nyingine unalia.
 
Sio kila kitu tunachokipenda tunatakiwa kuwa nacho. Kubaliana na ukweli kuna mwenzio ameshauwin moyo wa dogo. Unavyoendelea kulazimisha anaweza akakubali jamaa akimzungua halafu wewe ukaweka ndani kabisa. Siku anaempenda akirudi utatuletea thread nyingine unalia.
 
Hivi anavohangaika huyo dada ashajua anapendwa, anamfanyia kusud tu na either yuko na mtu kweli au anamchosha tu hamtaki mtoa mada na hiyo ndio solution na yeye akae kimya as if hayupo duniani tena hapo dukani anasalimia kijuujuu anaondoka zake akifanya hivo ataona rangi halisi ya huyo dada
Ushauri wote umeshamaliza wewe mimi nakazia tu
 
Broo shukuru Mungu amekwambia kuwa hana hisia nawe kuliko angekukubalia alafu badaye aanze kukuzingua ndani ya mapenzi yenu ungechanganyikiwa kwakweli mm nikitongoza akisema tu hapana haiwezekani nikaenda mara ya pili tena akakataa bc naendelea mbele yanini kujitesa broo tafuta mwingine kuwa naye uyoo akija kukubali atatumia udhaifu wa upendo wako kukunyoosha na utalia sana acha uboyaa
 
Upendo hauna vipimo mkuu, huwezi kusema huyu nampenda sana huyu kidogo, love is just alove kama upo mahali basi unakuwepo hapo, tofauti na hapo ni kinyume chake means upendo haupo
Kupenda sana nalo ni tatizo,penda kiasi.Wakupenda sana ni Mama mzazi tu.
 
Asante mkuu, kwa madini haya, nitayafanyia kazi, lakini pia hata kama mwanamke yupo single hutimia neno nina mtu kama mechanism defensive yake
Broo shukuru Mungu amekwambia kuwa hana hisia nawe kuliko angekukubalia alafu badaye aanze kukuzingua ndani ya mapenzi yenu ungechanganyikiwa kwakweli mm nikitongoza akisema tu hapana haiwezekani nikaenda mara ya pili tena akakataa bc naendelea mbele yanini kujitesa broo tafuta mwingine kuwa naye uyoo akija kukubali atatumia udhaifu wa upendo wako kukunyoosha na utalia sana acha uboyaa
 
Sio kila kitu tunachokipenda tunatakiwa kuwa nacho. Kubaliana na ukweli kuna mwenzio ameshauwin moyo wa dogo. Unavyoendelea kulazimisha anaweza akakubali jamaa akimzungua halafu wewe ukaweka ndani kabisa. Siku anaempenda akirudi utatuletea thread nyingine unalia.
Nimekuelewa vizuri sana mkuu, asante.. Umeongea vizuri sana
 
Back
Top Bottom