Nampenda sana na inanitesa sana

Nampenda sana na inanitesa sana

Ndugu yangu hupendwi...na pia jaribu kupunguza papara yaani usiwe na race nenda nae mdo mdogo mvungie ata week ikibidi mwezi mzima kama anakupenda atakutafuta
 
They blue tick you to that extent you paint your room blue..
Mwenywe inanikuta hii kwa toto moja ya engineering. Sema najipa moyo anasoma kitu ngumu na bora ajibu madesa boy wake.
 
mbona unajitesa hvyo mkuu apo ajakukubalia unaumia hvyo je angekua amekukubalia alaf afanye hvyo utajiweza kweli ???? unaacha kwenda class kwasabab ya kutojibiwa text ???? ebu penda maisha yako na ujipende mwenyew kwanza ina maana mahusiano yako ya kwanza hayakukufunza kitu chochote kuhus wanawake ? we wa kiume potezea endelea na maisha yako utajiaribia maisha kisa mtu ambae hana mwelekeo nawew
 
mbona unajitesa hvyo mkuu apo ajakukubalia unaumia hvyo je angekua amekukubalia alaf afanye hvyo utajiweza kweli ???? unaacha kwenda class kwasabab ya kutojibiwa text ???? ebu penda maisha yako na ujipende mwenyew kwanza ina maana mahusiano yako ya kwanza hayakukufunza kitu chochote kuhus wanawake ? we wa kiume potezea endelea na maisha yako utajiaribia maisha kisa mtu ambae hana mwelekeo nawew
Asante sana mkuu
 
Nimesoma uzi wako mwanzo hadi mwisho na hata majibu yako katika comments sijaona sehemu uliyosema uliwahi kumpa hela, hilo ni kosa mzee baba. Hata kama wazazi wake wangekuwa ndio wamiliki wa mlimani city mall na vilivyomo ndani yake pamoja na sheli zote za mjini, bado unalazimika kuhudumia mzee baba. Kuna mwenzako sasa anamuunga kifurushi cha wiki tu, kapewa attention kama yote. Mkono mtupu haulambwi ndugu.
 
Ni watu wachache sana wenye mapenzi ya dhati huishia kukutana na wapenzi wao wa maisha kikweli. Wengi huishia kuoa / kuolewa na magalasha na kuishi maisha ya kuchepuka na kuibia....

Life is never fair.

Pole sana.
sure..... life have never been fair ever since!!!!!!!!
 
Habari wakuu, ID hii ni mpya lakini mimi ni mwenyeji humu ndani, nimeamua kutumia ili kuepusha baadhi ya mambo.
Wakuu naamini ushauri wenu utanisaidia sana ndio maana nipo hapa. Ipo hivi:

Mwezi July katika mishe zangu nilikutana na mtoto mmoja mkali (wana duka) basi siku ya kwanza tu kumuona nikampenda sana, (mimi sio play boy mzee wa chapa ilale) nakumbuka toka nilivyoachana na girl friend wangu 2013 nilikua single (sio domo zege) maana kama ningeamua kua na mahusiano ningetaka sababu mpaka sasa kuna watoto watatu hivi wananielewa na wanalilia mapenzi yangu (sijisifu ni ukweli mtupu) lakini sijakua nao sababu nahitaji mwanamke mmoja wa kutulia nae kuanza maisha.

Basi yule mtoto dukani pale kila siku nikawa naenda (siku nyingine namkuta, siku nyingine mdogo ake, au dada yake au kaka yake) basi siku nisipomkuta nikamkuta kesho yake nikawa napiga nae story kufidia (wazazi wake wana maisha ya kizungu hawana noma mara kibao wamenikuta naongea na dogo hawaja mind) basi imeenda tukazoeana sana, hatimaye dogo akanipa namba, tukaanza ku chat kila siku kwa sms/whatsapp muda wote, usiku pia tunaenda mpaka saa sita saa saba. Basi katika ku chat na kuwasiliana nikajikuta nazidi kumpenda sana dogo, nae nahisi hivyo, mwanzo alikua anitafuti mpaka nianze mimi lakini tulienda mpaka nae akawa huru kunitafuta, muda mwingi akawa ananianza yeye, basi wakuu nikajiona bahati nzuri hiyo upande wangu.

Huyu mtoto anajielewa sana, narudia tena anajielewa, sikua na lengo la kumchezea, bali nilitumia ujanja wote kufanya juu chini kuomba dating lakini wapi dogo alinichomolea, pia kwenye issue ya mahusiano akanichomolea, lakini bado tunawasiliana kila siku asubuhi-usiku.
Kila nikimueleza kuhusu mahusiano anakataa kabisa, basi nikaamua kumtafuta dada yake nikaomba aniambie ukweli kuhusu mdogo ake, dada ake akaniambia hajui kama dogo ana mtu ama laah ila dogo hua hamfichi mambo yakekama angekua nae angeshajua.

Basi kila mtu akaenda field, wote tupo vyuo, huko nako dogo tukawa tunawasiliana sana, cha ajabu nikiomba hata picha dogo ananinyima, whatsapp tu hajaweka dp wala status, insta nako hajaweka picha hata profile pic hamna, indicators kibao zinazoonyesh dogo anajielewa zikanivuta sana kwake, nikakaza bado dogo akawa anakataa anadai ana mtu, basi nikawa najiuliza kama ana mtu ulimwengu huu mwanaume unaachaje mwanamke wako atumie karibi siku nzima kuwasiliana na mwanaume mwingine, maana dogo kila siku nipo nae whtsapp hadi usiku na interval ya ku reply ni dk 2.

Sasa majuzi nikiwa whatsapp nikamcheki dogo, mh sio kawaida ile meseji ya kwanza hakua amenijibu, nilivyomcheki ilipita dakika 6 ndio akaisoma, akanijibu basi nika reply, dakika 20 dogo yupo online haku reply, mh nikajua hapa kuna mwanaume mwingine ana chat nae labda nisubiri zamu yangu kesho, kesho inafika saa 2 asubuhi dg yupo online, hajanijibu, nikasepa offline, nakuja kufungua saa 6 mchana yupo online ajanibu, siku ya kwanza, ya pili ya tatu mpaka leo tunaenda siku ya 6 dogo ajanijibu, wakuu huyu mtoto nampenda sana naona ana kila sifa za kua wife material lakini najiuliza kwanini yupo online na hanijibu, kila siku hadi saa tano, saa sita usiku.

Natamani nimuanze tena lakini naogopa, wazungu wanasema not getting a message is also a message, kila nikiandika ujumbe nimtumie naishia kuufuta, nimebaki njia panda, roho inaniuma kumuona mtoto online muda wote, attention na mimi hana tena, na wala sijamkosea lolote, nampenda sana na laiti angejua malengo yangu kua sitaki kumchezea angetulia na mimi

Naombeni mnishauri wakuu nifanye nini, moyo wangu ni sensitive sana,, siku mbili sijalala wala kwenda class, kiukweli hili jambo limeniumiza sana, sana , sana.
_ _ _ F_ nakupenda sana usinitese tafadhali.

ASANTENI WAKUU, NAWASILISHA.
mkuu, huwezi hata kumpigia simu?..........


unaweza kuta ndio upo kwenye penati........ tuliza akili, dk ya 90+ hio[emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
*TUWAPIGIE KURA WASANII WETU MVP MUSIC AWARDS.* Hizi ni tuzo kubwa huko Nigeria. Turudishe heshima ya Tanzania.

Kwa kuwa wasanii wetu wengine wako wawili kwenye kipengele kimoja tupange tumpigie nani kura kila kipengele ili tusigawanye kura na tukashindwa kuchukua tuzo.

Vipengele:
*BEST MALE*
Hapa yupo Harmonize na Diamond. Tumpigie HARMONIZE kwa kuwa Diamond yupo kwenye vipengele vingine vingi.

*BEST FEMALE*
Tumpigie Maua Sama. Yupo peke yake toka Tz na East Africa

*BEST HIP HOP*
Hapa hakuna mbongo. Tumpe Khaligraph Jones mkali jirani yetu toka Kenya.

*BEST POP*
Tumpigie *Diamond Platnumz* yupo peke yake toka Tz na East Africa

*BEST COLLABORATION*
Hapa kuna JIBEBE na KATIKA. Tuipigie kura KATIKA YA NAVY KENZO kwa kuwa Diamond bado yupo kwenye vipengele vingine vingi. Isitoshe na kwenye KATIKA yumo

*DIGITAL ARTIST OF THE YEAR*
*Tumpigie Diamond Platnumz.* Hapa yupo peke yake kutoka Tanzania & East Africa

*BEST GROUP OF THE YEAR*

Tuwapigie Navy Kenzo

*SONG OF THE YEAR*
Hapa kuna *African Beauty ya Diamond*, na kuna *KWANGWARU* ya Harmonize na Diamond. Tuipigie *KWANGWARU* maana itapata kura nyingi zaidi toka nchi nyjngine za Africa kwa kuwa mpaka sasa ndo most viewed African music video kwa 2018. Na pia Diamond yumo

*BEST NEW ARTIST*
Tumpigie MBOSSO. Yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*LISTENERS' CHOICE*
Hapa ipo KATIKA ya Navy Kenzo na KWANGWARU ya Navy Kenzo. Tuipigie KATIKA ya Navy Kenzo maana KWANGWARU tushaipigia hapo juu

*AFRICAN PRODUCER OF THE YEAR*
Tumpigie NAHREEL yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*AFRICAN ARTIST OF THE YEAR*
Tumpigie *Diamond Platnumz* yupo peke yake kutoka Tz & East Africa

*JINSI YA KUPIGA KURA*
Click hii link
Soundcity MVP Awards Festival – Nominees are… Vote Now

Utakutana na vipengele vya tuzo zenyewe na majina ya wasanii husika (Nominees) gusa msanii unayempigia kura. Kura nu mara 1.

Tuache team zisizokuwa na maana. Tulete tuzo nyumbani.

*SAMBAZA KWA GROUPS ZAKO ZOTE*
 
Kama anasoma hajibu na wewe muignore mpe a taste of her own medicine inasaidia

Unaweza kua pretender??? Act like humtaki tna japo moyoni unaugulia, punguza mazoea ww utakuja nipa mrejesho

Ukiona juhudi zako hazizai matunda leave her alone,hakupangwa awe wako
usijidai_kuna_kufa chukua ushauri huu....... umetoka kwa mwanamke and i'm she knows more than us(men)!
 
Tatizo lako ni moja tu, wewe ni mwanafunzi, najua utakataa ila hakuna mwanamke anae mtaka mwanaume ambae hawezi kumhudumia. Kasema huwezi kumhudumia coz wewe mwanafunzi.

Kwa nini hakujibu??

Jibu: anakupenda ila uwezo huna.

Ana jamaa mwingine ambae hampendi ila ana uwezo wa kumpa huduma.

Status yake kwa sasa: ana play safe asiteme big G kwa Karanga sa kuonjeshwa.

Nini kitatokea baadae: atawakosa nyote

Kwa nini atawakosa nyote: kwa sababu anauza Duka visent vidogo ganji havikosi hana njaa Sana'a kivile, ana imani atapata mwingine baadae.
duh.......


kweli dawa ya mwanamke ni mwanamke..........


aisee kumbe mshauri mzuri wa mahusiano kwa wanaume anatakiwa kuwa mwanamke, and vice versa!!
 
Kuwa mpole jifanye kama hata humuwazii anajaribu kukupima na akigundua udhaifu wako atakutesa sana, Mkuu.
Bora yangu mm nilishazoea ma barmedi sitaki pressure mie!
 
Sinaga upendo wa aina hii,mwanamke ndo anatakiwa akupende,sasa ww mwanaume unampenda mwanamke mpaka unalia lia humu,mwanamke akikupenda hawezi kukusaliti maana utajua huyu mwanamke ananipenda na lazima matumizi utatoa tu.
 
Sinaga upendo wa aina hii,mwanamke ndo anatakiwa akupende,sasa ww mwanaume unampenda mwanamke mpaka unalia lia humu,mwanamke akikupenda hawezi kukusaliti maana utajua huyu mwanamke ananipenda na lazima matumizi utatoa tu.
true
 
Back
Top Bottom