Nampenda sana na inanitesa sana

Nampenda sana na inanitesa sana

Kama anasoma hajibu na wewe muignore mpe a taste of her own medicine inasaidia

Unaweza kua pretender??? Act like humtaki tna japo moyoni unaugulia, punguza mazoea ww utakuja nipa mrejesho

Ukiona juhudi zako hazizai matunda leave her alone,hakupangwa awe wako
 
Watu tumeumbwa tofauti etiii... Mbona wengine aiseeh hatuwezi lia lia kisa eti mapenziii.

Hajibu sms unapotezea life linasonga, baaasi, kwani yeye pumzi.
 
Habari wakuu, ID hii ni mpya lakini mimi ni mwenyeji humu ndani, nimeamua kutumia ili kuepusha baadhi ya mambo.
Wakuu naamini ushauri wenu utanisaidia sana ndio maana nipo hapa. Ipo hivi:

Mwezi July katika mishe zangu nilikutana na mtoto mmoja mkali (wana duka) basi siku ya kwanza tu kumuona nikampenda sana, (mimi sio play boy mzee wa chapa ilale) nakumbuka toka nilivyoachana na girl friend wangu 2013 nilikua single (sio domo zege) maana kama ningeamua kua na mahusiano ningetaka sababu mpaka sasa kuna watoto watatu hivi wananielewa na wanalilia mapenzi yangu (sijisifu ni ukweli mtupu) lakini sijakua nao sababu nahitaji mwanamke mmoja wa kutulia nae kuanza maisha.

Basi yule mtoto dukani pale kila siku nikawa naenda (siku nyingine namkuta, siku nyingine mdogo ake, au dada yake au kaka yake) basi siku nisipomkuta nikamkuta kesho yake nikawa napiga nae story kufidia (wazazi wake wana maisha ya kizungu hawana noma mara kibao wamenikuta naongea na dogo hawaja mind) basi imeenda tukazoeana sana, hatimaye dogo akanipa namba, tukaanza ku chat kila siku kwa sms/whatsapp muda wote, usiku pia tunaenda mpaka saa sita saa saba. Basi katika ku chat na kuwasiliana nikajikuta nazidi kumpenda sana dogo, nae nahisi hivyo, mwanzo alikua anitafuti mpaka nianze mimi lakini tulienda mpaka nae akawa huru kunitafuta, muda mwingi akawa ananianza yeye, basi wakuu nikajiona bahati nzuri hiyo upande wangu.

Huyu mtoto anajielewa sana, narudia tena anajielewa, sikua na lengo la kumchezea, bali nilitumia ujanja wote kufanya juu chini kuomba dating lakini wapi dogo alinichomolea, pia kwenye issue ya mahusiano akanichomolea, lakini bado tunawasiliana kila siku asubuhi-usiku.
Kila nikimueleza kuhusu mahusiano anakataa kabisa, basi nikaamua kumtafuta dada yake nikaomba aniambie ukweli kuhusu mdogo ake, dada ake akaniambia hajui kama dogo ana mtu ama laah ila dogo hua hamfichi mambo yakekama angekua nae angeshajua.

Basi kila mtu akaenda field, wote tupo vyuo, huko nako dogo tukawa tunawasiliana sana, cha ajabu nikiomba hata picha dogo ananinyima, whatsapp tu hajaweka dp wala status, insta nako hajaweka picha hata profile pic hamna, indicators kibao zinazoonyesh dogo anajielewa zikanivuta sana kwake, nikakaza bado dogo akawa anakataa anadai ana mtu, basi nikawa najiuliza kama ana mtu ulimwengu huu mwanaume unaachaje mwanamke wako atumie karibi siku nzima kuwasiliana na mwanaume mwingine, maana dogo kila siku nipo nae whtsapp hadi usiku na interval ya ku reply ni dk 2.

Sasa majuzi nikiwa whatsapp nikamcheki dogo, mh sio kawaida ile meseji ya kwanza hakua amenijibu, nilivyomcheki ilipita dakika 6 ndio akaisoma, akanijibu basi nika reply, dakika 20 dogo yupo online haku reply, mh nikajua hapa kuna mwanaume mwingine ana chat nae labda nisubiri zamu yangu kesho, kesho inafika saa 2 asubuhi dg yupo online, hajanijibu, nikasepa offline, nakuja kufungua saa 6 mchana yupo online ajanibu, siku ya kwanza, ya pili ya tatu mpaka leo tunaenda siku ya 6 dogo ajanijibu, wakuu huyu mtoto nampenda sana naona ana kila sifa za kua wife material lakini najiuliza kwanini yupo online na hanijibu, kila siku hadi saa tano, saa sita usiku.

Natamani nimuanze tena lakini naogopa, wazungu wanasema not getting a message is also a message, kila nikiandika ujumbe nimtumie naishia kuufuta, nimebaki njia panda, roho inaniuma kumuona mtoto online muda wote, attention na mimi hana tena, na wala sijamkosea lolote, nampenda sana na laiti angejua malengo yangu kua sitaki kumchezea angetulia na mimi

Naombeni mnishauri wakuu nifanye nini, moyo wangu ni sensitive sana,, siku mbili sijalala wala kwenda class, kiukweli hili jambo limeniumiza sana, sana , sana.
_ _ _ F_ nakupenda sana usinitese tafadhali.

ASANTENI WAKUU, NAWASILISHA.
AMECHOKA KUCHAT ANATAKA UENDE DUKANI MKAPIGE STORY KM ZAMANI
 
Zaidi ya kuchat na kumuotea dukani, uwa mnatoka??
 
Kiufupi hajakukubali. Sasa wewe lazimisha uonee balaaa lake.

Alaf pesa zipoo sio unapiga jarambajaramba tuu mkono mtupu haulambwi na hata hivyo hakuna mwanamke mzuri atakae shinda uzuri Wa pesa.
 
Inaonekana umeonesha mapepe mengi sana kwenye kumtaka, au pengine chats zako zinakuwa ni zile zile kwahy anakuwa bored. Acha kumchatisha pia ji keep busy tu kwa mda.
Kama anapokea sim mpigie umsalimie na kumjualia hali alf umuage mapema... Yan unakuwa mrahisi sana ndo shida
Ukiona pia hana time na wewe temana nae mapenzi haya lazimishwi
 
Kama anasoma hajibu na wewe muignore mpe a taste of her own medicine inasaidia

Unaweza kua pretender??? Act like humtaki tna japo moyoni unaugulia, punguza mazoea ww utakuja nipa mrejesho

Ukiona juhudi zako hazizai matunda leave her alone,hakupangwa awe wako
You are Right Madame S mimi hua naita mapicha picha nikisha ona msichana ana nilete izi mambo basi na mm nampoteze kwanza whatsapp chat zake naziweka kwenye Archive huo muda wa kuangalia last seen yake sina status zake na freeze kisha nakula buyu nikiona hanitafuti within three days nadelete chats kimya kikizid na delete na contacts No hard Feelings kwa kweli life has to move on si kupangiwa kua naye najipa moyo konde lohh!!!
 
Tatizo lako ni moja tu, wewe ni mwanafunzi, najua utakataa ila hakuna mwanamke anae mtaka mwanaume ambae hawezi kumhudumia. Kasema huwezi kumhudumia coz wewe mwanafunzi.

Kwa nini hakujibu??

Jibu: anakupenda ila uwezo huna.

Ana jamaa mwingine ambae hampendi ila ana uwezo wa kumpa huduma.

Status yake kwa sasa: ana play safe asiteme big G kwa Karanga sa kuonjeshwa.

Nini kitatokea baadae: atawakosa nyote

Kwa nini atawakosa nyote: kwa sababu anauza Duka visent vidogo ganji havikosi hana njaa Sana'a kivile, ana imani atapata mwingine baadae.
 
Asante Madame kwa ushauri wako,, nitajitahidi kuufata na nitakupa mlejesho
 
Umeongea vizuri sana mkuu, sasa kwannn ue na mtu ambaye humpendi kisa maslahi? Inawezekanaje
Tatizo lako ni moja tu, wewe ni mwanafunzi, najua utakataa ila hakuna mwanamke anae mtaka mwanaume ambae hawezi kumhudumia. Kasema huwezi kumhudumia coz wewe mwanafunzi.

Kwa nini hakujibu??

Jibu: anakupenda ila uwezo huna.

Ana jamaa mwingine ambae hampendi ila ana uwezo wa kumpa huduma.

Status yake kwa sasa: ana play safe asiteme big G kwa Karanga sa kuonjeshwa.

Nini kitatokea baadae: atawakosa nyote

Kwa nini atawakosa nyote: kwa sababu anauza Duka visent vidogo ganji havikosi hana njaa Sana'a kivile, ana imani atapata mwingine baadae.
 
Hivi anavohangaika huyo dada ashajua anapendwa, anamfanyia kusud tu na either yuko na mtu kweli au anamchosha tu hamtaki mtoa mada na hiyo ndio solution na yeye akae kimya as if hayupo duniani tena hapo dukani anasalimia kijuujuu anaondoka zake akifanya hivo ataona rangi halisi ya huyo dada

Back
Top Bottom