Nampenda sana na inanitesa sana

Dec 15, 2018
78
53
Habari wakuu, ID hii ni mpya lakini mimi ni mwenyeji humu ndani, nimeamua kutumia ili kuepusha baadhi ya mambo.
Wakuu naamini ushauri wenu utanisaidia sana ndio maana nipo hapa. Ipo hivi:

Mwezi July katika mishe zangu nilikutana na mtoto mmoja mkali (wana duka) basi siku ya kwanza tu kumuona nikampenda sana, (mimi sio play boy mzee wa chapa ilale) nakumbuka toka nilivyoachana na girl friend wangu 2013 nilikua single (sio domo zege) maana kama ningeamua kua na mahusiano ningetaka sababu mpaka sasa kuna watoto watatu hivi wananielewa na wanalilia mapenzi yangu (sijisifu ni ukweli mtupu) lakini sijakua nao sababu nahitaji mwanamke mmoja wa kutulia nae kuanza maisha.

Basi yule mtoto dukani pale kila siku nikawa naenda (siku nyingine namkuta, siku nyingine mdogo ake, au dada yake au kaka yake) basi siku nisipomkuta nikamkuta kesho yake nikawa napiga nae story kufidia (wazazi wake wana maisha ya kizungu hawana noma mara kibao wamenikuta naongea na dogo hawaja mind) basi imeenda tukazoeana sana, hatimaye dogo akanipa namba, tukaanza ku chat kila siku kwa sms/whatsapp muda wote, usiku pia tunaenda mpaka saa sita saa saba. Basi katika ku chat na kuwasiliana nikajikuta nazidi kumpenda sana dogo, nae nahisi hivyo, mwanzo alikua anitafuti mpaka nianze mimi lakini tulienda mpaka nae akawa huru kunitafuta, muda mwingi akawa ananianza yeye, basi wakuu nikajiona bahati nzuri hiyo upande wangu.

Huyu mtoto anajielewa sana, narudia tena anajielewa, sikua na lengo la kumchezea, bali nilitumia ujanja wote kufanya juu chini kuomba dating lakini wapi dogo alinichomolea, pia kwenye issue ya mahusiano akanichomolea, lakini bado tunawasiliana kila siku asubuhi-usiku.
Kila nikimueleza kuhusu mahusiano anakataa kabisa, basi nikaamua kumtafuta dada yake nikaomba aniambie ukweli kuhusu mdogo ake, dada ake akaniambia hajui kama dogo ana mtu ama laah ila dogo hua hamfichi mambo yakekama angekua nae angeshajua.

Basi kila mtu akaenda field, wote tupo vyuo, huko nako dogo tukawa tunawasiliana sana, cha ajabu nikiomba hata picha dogo ananinyima, whatsapp tu hajaweka dp wala status, insta nako hajaweka picha hata profile pic hamna, indicators kibao zinazoonyesh dogo anajielewa zikanivuta sana kwake, nikakaza bado dogo akawa anakataa anadai ana mtu, basi nikawa najiuliza kama ana mtu ulimwengu huu mwanaume unaachaje mwanamke wako atumie karibi siku nzima kuwasiliana na mwanaume mwingine, maana dogo kila siku nipo nae whtsapp hadi usiku na interval ya ku reply ni dk 2.

Sasa majuzi nikiwa whatsapp nikamcheki dogo, mh sio kawaida ile meseji ya kwanza hakua amenijibu, nilivyomcheki ilipita dakika 6 ndio akaisoma, akanijibu basi nika reply, dakika 20 dogo yupo online haku reply, mh nikajua hapa kuna mwanaume mwingine ana chat nae labda nisubiri zamu yangu kesho, kesho inafika saa 2 asubuhi dg yupo online, hajanijibu, nikasepa offline, nakuja kufungua saa 6 mchana yupo online ajanibu, siku ya kwanza, ya pili ya tatu mpaka leo tunaenda siku ya 6 dogo ajanijibu, wakuu huyu mtoto nampenda sana naona ana kila sifa za kua wife material lakini najiuliza kwanini yupo online na hanijibu, kila siku hadi saa tano, saa sita usiku.

Natamani nimuanze tena lakini naogopa, wazungu wanasema not getting a message is also a message, kila nikiandika ujumbe nimtumie naishia kuufuta, nimebaki njia panda, roho inaniuma kumuona mtoto online muda wote, attention na mimi hana tena, na wala sijamkosea lolote, nampenda sana na laiti angejua malengo yangu kua sitaki kumchezea angetulia na mimi

Naombeni mnishauri wakuu nifanye nini, moyo wangu ni sensitive sana,, siku mbili sijalala wala kwenda class, kiukweli hili jambo limeniumiza sana, sana , sana.
_ _ _ F_ nakupenda sana usinitese tafadhali.

ASANTENI WAKUU, NAWASILISHA.
 
Ni watu wachache sana wenye mapenzi ya dhati huishia kukutana na wapenzi wao wa maisha kikweli. Wengi huishia kuoa / kuolewa na magalasha na kuishi maisha ya kuchepuka na kuibia....

Life is never fair.

Pole sana.
 
Ni watu wachache sana wenye mapenzi ya dhati huishia kukutana na wapenzi wao wa maisha kikweli. Wengi huishia kuoa / kuolewa na magalasha na kuishi maisha ya kuchepuka na kuibia....

Life is never fair.

Pole sana.
Kabisa mkuu, yani najuta bora hata nisingemfahamu toka mwanzo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu ushauri wangu ni kuwa jikaze utapona baada ya miaka michache mno. Kwa uzoefu wangu huyo dogo kama unavyomuita atakuelewa ila kwa kuchelewa sana. Na wakati amekuelewa wewe hutakuwa na interest tena maana utakuwa umeshamove on ama una mwingine mnapendana.

Wakati huo itakubidi uchukue uamuzi mgumu kwani atakuwa analia kila siku na utajiuliza je ni kweli ama anakuzingua. Zaidi atakuwa amechuja machoni pako.
 
Nacheka kama mazuri, tulia usipanic tulia utajua tu ukweli.

Mapenzi yanauma sana ukimpenda mtu kidhati ndo inavokuwaga.
Usije ukawa ndio wewe, maana naye alishazoea kusema 'Nacheka kama mazuri' all in all asante kwa ushauri
 
Thanks for your words mkuu, na ninatamani iwe hivyo
Mkuu ushauri wangu ni kuwa jikaze utapona baada ya miaka michache mno. Kwa uzoefu wangu huyo dogo kama unavyomuita atakuelewa ila kwa kuchelewa sana. Na wakati amekuelewa wewe hutakuwa na interest tena maana utakuwa umeshamove on ama una mwingine mnapendana.

Wakati huo itakubidi uchukue uamuzi mgumu kwani atakuwa analia kila siku na utajiuliza je ni kweli ama anakuzingua. Zaidi atakuwa amechuja machoni pako.
 
Back
Top Bottom