Nampenda sana na inanitesa sana

Nampenda sana na inanitesa sana

ZulFa sio, Hebu Malizen chuo kwanza, Kama Mungu amepanga bas mtakuwa pamoja,. Jitihad pekee za kukufanya ww uwe na Zulfa hapo baadae ni kusoma kwa bidii, ufaulu na upate kazi na uwe na hela.. Mbona Zulfa ataamia kabisa kwako..
 
We sio chaguo lake,usilazimishe.Mfano mzuri wewe umesema kuna mabinti wanaokupenda ila wewe huwapendi,kwa hiyo na kwa huyo anayekuumiza kichwa wewe,hakuitaji kimapenzi kwasababu sio chaguo lake;nakushauri tafuta mwingine.
Alafu trust me kama Kuna mabinti wanampenda jamaa anawakataa... Huyu demy atamtesa sana jamaa na hatamkubali milele zaidi atakuwa anamchoraa tuu..!!

Story kama ya best angu yeye alikuwa anajikuta HB sana anawakataa wadada lakini Alikuja kupenda mdada flani baada ya kuwa rafiki yake for 3 years Yule manzi alimkataaa kabisaa... Ikatokea tena akampenda manzi mwingne yule ndo alikuwa mpaka anavujisha mawasiliano yao...anawaambia washkaji kuwa hamtaki mwana akati mwana anajiona ana vigezo vyote vya kuwa na yule manzi!

KARMA IS REALLY....
 
Holy shit, unamfukuzia mwanamke for 6 months????? Mimi wiki moja tu nikiona mtu ananichukulia poa nabwaga manyanga, Nina pride kubwa sana.., coz naamini mwanamke anaenizungusha mda mrefu hanipendi, doooh mnaishije humo kwenye ndoa? Una uhakika huyo mkeo anakupenda au yupo na ww bhasi tu, kwa vile alikosa option MtamaMchungu
Ni story ndefu kidogo ningeweza kuandika thread nzima, lakini itoshe kusema when someone ticks all the right boxes, you know you have found the one. Checklist yote ilitimia, sijawahi ku-regret ule msako; it was all worth it. In the process nilijifunza vitu vingi, Pride is important lakini kuwa makini isikupofushe, feeding your pride inaweza kukukosesha vitu mzee.

Hilo la kunipenda, anajua Mungu mwenyezi, ila itoshe kusema sijawahi kuona sababu ya kutilia mashaka. Kuhusu Options zake, kwanza kila mtu alikuwa anamshangaa, katika foleni ya watu wooote umechukua haka kamjamaa. Kipindi niko chuo, walimu wanatamani kunifukuza chuo kabisa. Anyways, to me she was the best of the rest, labda because she was a challenge ilinipa morale zaidi. I don't know, ila tuna 10 happy years, which in itself is an achievement siku hizi.
 
Swali, unataka mke wa kuoa au tamaa za mwili tu.? Umesema unasoma, Vipi mpango wa shule.? Vipi unayo hela wewe? Je, unadhani utamuweza kweli kama mtoto mwenyewe anajitambua, umesema ww sio maneno yangu kuwa ni mtoto wa kishua. Mkuu nifupishe tu soma kwa bidii, tafuta mkwanja, jenga life kwanza. Mapenzi bila hela utarudi unalialia siku moja. Pole sana
 
Naombeni mnishauri wakuu nifanye nini, moyo wangu ni sensitive sana,, siku mbili sijalala wala kwenda class, kiukweli hili jambo limeniumiza sana, sana , sana.
_ _ _ F_ nakupenda sana usinitese tafadhali.

ASANTENI WAKUU, NAWASILISHA.
You are the victim of your own feelings. Ukitaka amani ni uweze kumudu hizo hisia zako. Kila kitu uko nacho wewe. If you get hurt its on you not her. Yeye umempa proposal mara kibao na kakataa, which is fair. Habari za kuspeculate on what she does with her life, ni mateso makubwa sana kwa upande wako. Get hold of your feelings now na uendelee na maisha. Love will come when its time. Kwanza hayo mapenzi ya chuo most of the times hayalipi bro, fanya maisha.
 
Ni story ndefu kidogo ningeweza kuandika thread nzima, lakini itoshe kusema when someone ticks all the right boxes, you know you have found the one. Checklist yote ilitimia, sijawahi ku-regret ule msako; it was all worth it. In the process nilijifunza vitu vingi, Pride is important lakini kuwa makini isikupofushe, feeding your pride inaweza kukukosesha vitu mzee.

Hilo la kunipenda, anajua Mungu mwenyezi, ila itoshe kusema sijawahi kuona sababu ya kutilia mashaka. Kuhusu Options zake, kwanza kila mtu alikuwa anamshangaa, katika foleni ya watu wooote umechukua haka kamjamaa. Kipindi niko chuo, walimu wanatamani kunifukuza chuo kabisa. Anyways, to me she was the best of the rest, labda because she was a challenge ilinipa morale zaidi. I don't know, ila tuna 10 happy years, which in itself is an achievement siku hizi.
Mimi pia niko in same situation kama ya mtoa mada,Na siamin kwenye kuzungushana sana,ivyo nimeamua kutulia nione mwisho wake,coz kwangu mimi love is more worth when it is given for free,without struggle yoyote,ila kwa maelezo yako, nilichoelewa kilichokifanya upambane sana uwe na uyo mwanamke ni ile imani ya quality alizo nazo,na sio upendo.Na ndo maaana apo ulikoulizwa kama anakupenda yeye umesema anajua mungu.
 
Mimi pia niko in same situation kama ya mtoa mada,Na siamin kwenye kuzungushana sana,ivyo nimeamua kutulia nione mwisho wake,coz kwangu mimi love is more worth when it is given for free,without struggle yoyote,ila kwa maelezo yako, nilichoelewa kilichokifanya upambane sana uwe na uyo mwanamke ni ile imani ya quality alizo nazo,na sio upendo.Na ndo maaana apo ulikoulizwa kama anakupenda yeye umesema anajua mungu.
Mzee swali la mkeo anakupendaje, huwa sijibu. Huwa nasema tu sina sababu ya ku-doubt. Life has surprises mkuu, you should always leave some room for any eventuality.
 
Habari wakuu, ID hii ni mpya lakini mimi ni mwenyeji humu ndani, nimeamua kutumia ili kuepusha baadhi ya mambo.
Wakuu naamini ushauri wenu utanisaidia sana ndio maana nipo hapa. Ipo hivi:

Mwezi July katika mishe zangu nilikutana na mtoto mmoja mkali (wana duka) basi siku ya kwanza tu kumuona nikampenda sana, (mimi sio play boy mzee wa chapa ilale) nakumbuka toka nilivyoachana na girl friend wangu 2013 nilikua single (sio domo zege) maana kama ningeamua kua na mahusiano ningetaka sababu mpaka sasa kuna watoto watatu hivi wananielewa na wanalilia mapenzi yangu (sijisifu ni ukweli mtupu) lakini sijakua nao sababu nahitaji mwanamke mmoja wa kutulia nae kuanza maisha.

Basi yule mtoto dukani pale kila siku nikawa naenda (siku nyingine namkuta, siku nyingine mdogo ake, au dada yake au kaka yake) basi siku nisipomkuta nikamkuta kesho yake nikawa napiga nae story kufidia (wazazi wake wana maisha ya kizungu hawana noma mara kibao wamenikuta naongea na dogo hawaja mind) basi imeenda tukazoeana sana, hatimaye dogo akanipa namba, tukaanza ku chat kila siku kwa sms/whatsapp muda wote, usiku pia tunaenda mpaka saa sita saa saba. Basi katika ku chat na kuwasiliana nikajikuta nazidi kumpenda sana dogo, nae nahisi hivyo, mwanzo alikua anitafuti mpaka nianze mimi lakini tulienda mpaka nae akawa huru kunitafuta, muda mwingi akawa ananianza yeye, basi wakuu nikajiona bahati nzuri hiyo upande wangu.

Huyu mtoto anajielewa sana, narudia tena anajielewa, sikua na lengo la kumchezea, bali nilitumia ujanja wote kufanya juu chini kuomba dating lakini wapi dogo alinichomolea, pia kwenye issue ya mahusiano akanichomolea, lakini bado tunawasiliana kila siku asubuhi-usiku.
Kila nikimueleza kuhusu mahusiano anakataa kabisa, basi nikaamua kumtafuta dada yake nikaomba aniambie ukweli kuhusu mdogo ake, dada ake akaniambia hajui kama dogo ana mtu ama laah ila dogo hua hamfichi mambo yakekama angekua nae angeshajua.

Basi kila mtu akaenda field, wote tupo vyuo, huko nako dogo tukawa tunawasiliana sana, cha ajabu nikiomba hata picha dogo ananinyima, whatsapp tu hajaweka dp wala status, insta nako hajaweka picha hata profile pic hamna, indicators kibao zinazoonyesh dogo anajielewa zikanivuta sana kwake, nikakaza bado dogo akawa anakataa anadai ana mtu, basi nikawa najiuliza kama ana mtu ulimwengu huu mwanaume unaachaje mwanamke wako atumie karibi siku nzima kuwasiliana na mwanaume mwingine, maana dogo kila siku nipo nae whtsapp hadi usiku na interval ya ku reply ni dk 2.

Sasa majuzi nikiwa whatsapp nikamcheki dogo, mh sio kawaida ile meseji ya kwanza hakua amenijibu, nilivyomcheki ilipita dakika 6 ndio akaisoma, akanijibu basi nika reply, dakika 20 dogo yupo online haku reply, mh nikajua hapa kuna mwanaume mwingine ana chat nae labda nisubiri zamu yangu kesho, kesho inafika saa 2 asubuhi dg yupo online, hajanijibu, nikasepa offline, nakuja kufungua saa 6 mchana yupo online ajanibu, siku ya kwanza, ya pili ya tatu mpaka leo tunaenda siku ya 6 dogo ajanijibu, wakuu huyu mtoto nampenda sana naona ana kila sifa za kua wife material lakini najiuliza kwanini yupo online na hanijibu, kila siku hadi saa tano, saa sita usiku.

Natamani nimuanze tena lakini naogopa, wazungu wanasema not getting a message is also a message, kila nikiandika ujumbe nimtumie naishia kuufuta, nimebaki njia panda, roho inaniuma kumuona mtoto online muda wote, attention na mimi hana tena, na wala sijamkosea lolote, nampenda sana na laiti angejua malengo yangu kua sitaki kumchezea angetulia na mimi

Naombeni mnishauri wakuu nifanye nini, moyo wangu ni sensitive sana,, siku mbili sijalala wala kwenda class, kiukweli hili jambo limeniumiza sana, sana , sana.
_ _ _ F_ nakupenda sana usinitese tafadhali.

ASANTENI WAKUU, NAWASILISHA.
Futa namba yake haraka na chats zenu zote. Ugulia wiki nzima alafu endelea na maisha. Atakutafutaga tu kwa wakati wake. Nina experience na hiyo kitu

Ukiwa katika situations kama hizo usipende njia itakayokufariji au kukufurahisha, penda njia itakayokupa matokeo unayoyataka.

Matokeo unayoyataka ni kuwa mke wako. Lenga hilo kwanza usitumie nguvu nyingi kwenye kujifariji
 
Laiti ungeyajua haya maisha kwa jicho kama lakupevuka wala usingethubutu kusema unamalengo unataka kumuoa

wote tumepita uko mku so pambana tu na hali yako ila ukivuka apo ukaja kwenye maturity utajicheka juu ya huo mkasa
 
You've been friend-zoned my bro, japo unataka muende mbali. Gia ya kupiga stori 'zisizo' na maana dukani kwao na kuchat kusiko na focus unakuja kushtuka alishaamua kusepa kwingine!

Ni somo, get over it tafuta mwingine na usitumie 'any of the strategies' iliyokufelisha mwanzo!
 
Mkuu every one has got his own timeline ,, every man has his own decision to decide his destination,, namaanisha everything is a choice kama mtu fulani alichelewa kumfikia wife material wake hai guarantee mwingine pia nae atachelewa. Mwaka wa 4 Uhandisi wa kilimo
Ungejua safari uliyonayo hadi kuja kumfikia wife material wako hata usingetusumbua humu. Upo mwaka wa ngapi?
 
Lazima uzoeshe Moyo kupuuzia mambo ambayo unahisi yatakuumiza sana, ukishauseti hivyo utaishi kwa raha sana...Nakuambia haya maana wengine mambo kama haya hutokea na huyamaliza kimyakimya kwa kupuuzia na kupotezea, maana kwa nini uumie kwa jambo ambalo halikujengi bali linakuharibia na pengine linaweza kukukosesha hata kutomkumbuka Mungu kuwa ndiye atupaye uzima na afya, na Mungu pekee ndiye apangaye, pengine unaweza akakuwezesha kumpata yule umpendaye ambaye hatakutesa...maaan kwa dalili hizo ulizopata sioni mazuri huko mbele...Mpe Mungu kipaumbele, puuzia unayoona yatakuumiza, fanya yatakayokujenga na kukupa amani na furaha.
Asante mkuu
 
Kama umeona ndio wife material jikaze ndugu. Mimi pride yote ilibidi niweke mfukoni, miezi 6 hakuna call back wala message kujibiwa. Dah! Lakini ndio hivyo tena unakaza msuli, leo she's my wife for 4yrs been together for 10. Ila kama humpendi, usijitese.
Asante, mkuu kwa maneno yako
 
NINGEJUA UMRI WAKO kwanza na umri wake pia ningejua nishauri nn,maana nahc kuna kutokujielewa kati yenu hakuna mwanamke mgumu kwa mwanaume anayejielewa usiwe kama baba paroko au mchungaji ktk inshu za mahusiano hope utanielewa
Nishataja nyuma 27 yeye 25
 
Back
Top Bottom