Nampenda Mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege.

Mwakasege akiwa Dar anaabudu Azania Front Lutheran Church Postal mpya
Ana of is Luther House Azania Front
Mbezi Beach Lutheran Tangibovu anaalikwaga seminar
Anaishi Simanjiro bwana sio kijenge
Sio Simanjiro ni Njiro jijini Arusha, pia ana ofisi yake Arusha
 
Daaah asante sana kwa kweli,pale anapokuja dar sijawah kosa semina zake kama nipo dar na mm,na pili nakumbuka tulienda na mke wng kwa ushauri tu kwake,akamwambia mke wngu ,,akasema nimeona kitu juu yako,nmeona umechanua kama maua,nmeona jina lako mahali fulan hakika utapata kile kilichokuleta,usiache kumshukuru Mungu maana amekustawisha kwa iman yako kwake,leo kalale kesho kabla ya saa kenda utaona nguvu ya Mungu,,kesho yake sa saba mke anapigiwa simu kwamba jina lako limetoka la kwanza kbsa kwenda kusoma nje..na tulishadunda zaid ya mara mbili kufukuzia scholaship,,toka siku hyo kiukwel siwez acha kusikiliza mahubiri yake tu hata Youtube,amenijenga snaa kiiman na Mungu azid kumwongezea kwa kwwli
 
Kabisaaa..... Na zama hizi zilivo za hatari usipokua na mafundisho na neno lakutosha lazima uende na maji.
 
Mafundisho ya Mwl Christopher Mwakasege yana [pumzi ya Mungu kabisa maaana ni yanafaa kabisa kwa maisha yetu kwa hali ya juu sana .tofauti na mikorogo mingine, hqalafu yuko humble sana hata kanisani anaposali kijenge ni muumini tu wa kawaida anasemaga Hamtazami aliyesimama mbele kufundisha ni nani lakin anaimani kinachoshushwa ni chakula chenye pumzi ya Bwana. Mungu azidi kumbariki sana huyu Mwl,
 
Kuna somo niliwahi kuhudhuria semina yake alilipa jina la MALANGO!...Sijui kama kunasomo la kiroho lililonibariki kama hili.

Mungu ampe afya tele mtumwa wake huyu.
Ni somo lililonifanya nizidi kuitafuta kweli ya INJILI. Mzaliwa wa kwanza ana nafasi gani kwenye Agano Jipya? Msaada hapo.
 
Mh!
Sina shida na sifa za mchungaji huyo wa kondoo ila upendo uliotajwa na mtoa mada hapo juu ulimaanisha hasa kuwa yu ampenda hasa kama mwalimu na mlezi wake kiimani ama ule wa kutamani awe mlezi na baba wa watoto wake?
Ni sentensi tata hasa kwetu sisi wa darasa la tatu A.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…