Nampenda Mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege.

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,921
14,821
Bwana Yesu Asifiwe jamani nampendaga sana Mtumishi wa Mungu Christopher Mwakasege kwanza hana Scandals ,Pili anampenda Mungu kikweli kweli tatu hana mafundisho ya uongo nne hajawahi kuchuja tangu nipo mdogo miaka 5 naenda kwenye mahubiri yake anakuja kuhubiri pale Upanga mtaani kwetu Lugalo mpaka leo alafu yupo hivyo hivyo!

Alafu huyu baba hazeeki jamaa doh kila siku yupo hivyo hivyo kama Malaika
watumishi wengine wangejifunza toka kwa huyu baba siri ya kumtumikia Mungu
Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu na Mwalimu Christopher Mwakasege AMEN
 
Huyu Mwl madini yake huwaga yanapenya vyema sana kwenye akili zetu anatumika vyema sana kuna wakati huko huko kwao Mbeya kwao kanisa gani sijui ila ni haya ya kipentecoste walitaka kumchafua et kuna mtu alikua amepandisha mapepo akawa anaongea vitu vya ajabu sana na vya kijinga sana et kuna siku mapepo yalimwilingilia mwakasege kupitia Microphone alikuwa kaiweka chini halaf akawa na tabia ya kutamani na kutembea na wake za watu ulikua ni upuuzi uliozimika haraka sana
 
Si mtu wa kutaka cheo(ukubwa/fahari)
Sijackia akijiita askofu, mtume, nabii, his excellent dr mh nabii mkuu noooo yeye daima hujiita Mwalimu Christopher Mwakasege.
Licha ya kuwa mwl mzuri wa dini lakini ni mwl mzuri wa uchumi kwani katika semina zake hutoa sana mafinzo ya kichumi na si wale nunua maji ya baraka upate magari kumbe wizi mtupu

Abarikiwe unyamfyale uju setano angangwisya!!!!
 
Back
Top Bottom