Usiache kazi Kwa sababu unataka kumtumukia Mungu

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi
Mara ya Kwanza mkristo unapopata Neema ya kuhokoka , Roho Mtakatifu anaingia ndani yako na pale anapoingia ndani yako kuna kiu ya kutaka kumjua Mungu Sana inaingia ndani yako

Unakuwa na kiu kubwa Sana ya kumjua Mungu na wengine Kwa kukosa msaada wanajikuta wameingia kwenye njia mahangaiko ya kila aina

Namshukuru Mungu mara baada ya kuhokoka aliweka kiu ndani yangu ya kumjua yeye na nilipata walezi wakuniongoza na kunisaidia na kitu cha muhimu zaidi aliweka ndani yangu bidii ya kusoma Neno na kuwasilikiza watumishi mbalimbali ambao wamekuwa wazazi wangu WA kiroho

Nakumbuka mara baada ya kuhokoka Ile kiu ya kusoma Neno la Mungu ilileta Hofu nyumbani kwetu wakajua kijana huyu SASA hivi atatangaza anataka kwenda kusoma uchungaji, Hadi wazazi wakawa wananikataza kusoma Sana biblia??

Nilikuwa nakiu Sana ya kumtumikia Mungu na nilitumika Kwa sehemu yangu nilitumika kanisani kwenye vijana na shuleni pia nilitumika , bahati mbaya nilipata Neema nikiwa ndo ninamaliza masomo yangu niingie mtaani kutafufa Maisha

Kiu ya kumtumikia Mungu iliniweka njia panda Kati ya kufanya kazi au kumtumikia Mungu , namshukuru Mungu Kwa Baba yangu WA kiroho Mwl Christopher Mwakasege Kwa mafundisho yake ambayo kwakweli yaliniwekea kizuizi cha kuhacha kazi pasipo maelekezo ya Mungu

Mara Kwa mara Mwl alikuwa anasema kwenye mafundisho yake kwamba tumsikilize Mungu kabla ya kufanya maamuzi ya kuhacha kazi na kweli nilimsikiliza na ninaendelea kumskiliza kwakweli

Mwingine ni Askofu wangu msaidizi alikuwa msaada kwangu ni rafiki yangu Hadi kesho lakini alikuwa ananisisitiza Sana kufanya kazi Kwa bidii hata siku moja hakuwai kuniambia kuacha kazi niende kwenye uchungaji ingawa alikuwa ana nafasi ya kunipelekea chuoni tena buree lakini hakuwai kunishauri hicho kitu

Niliendelea kumtafuta Mungu kujua kusudi la Mimi kuweko duniani , ni hasara Sana kukaa duniani na kuondoka pasipo kujua kusudi lako uliloitiwa

Mungu ni mwaminifu nilipomtafuta Mungu kweli alinionekania akanijibu maswali ambayo zaidi ya miaka 10 iliyopita nilikuwa ninayo juu ya wito ambao Mungu ameweka

Biblia inasema kila aliye na mwana anao ushuhuda Ile kuwa na ushuhuda wa Mungu sio tiketi ya kwamba umeitwa kuwa mchungaji hapana

Mungu anataka kuwa na watu katika kila eneo, unaposoma neno la Mungu , unapata ufahamu juu ya kumtumikia Mungu , kila eneo Mungu ameliweka ili watu waweze kumtumikia

Ndio maana kama umehokoka na unafanya kazi usifanye haraka kuacha kazi , kama kwenye hiyo kazi muulize Mungu amekuitia nini? Kuna habari nyingi tunasoma watu wanaacha masomo wanaacha kazi wanaamua kumtumikia Mungu

Kumbe shetani anawatoa kwenye Edeni Zao , ukiona Mungu amekuokoa ukiwa katika kazi yoyote usijaribu kuacha kazi au kubadirisha kazi endelea kufanya hiyo kazi Hadi siku Mungu aseme sasa Nenda kituo kinachofata

Watu wengi wamearibu Maisha Yao Kwa kuacha kazi pasipo kupewa maelekezo na Mungu na mwisho WA siku Maisha Yao yamearibika

Hata kama Mtumishi WA Mungu ni mkubwa kiasi gani usikubali kupokea ushauri wowote WA kuacha kazi msikilize Mungu kwanza utakuja kujutia maamuzi yako baadae

Sio kila ushauri unatoka Kwa Mungu na duniani kuna watumishi wengine wanatumiwa na shetani pasipo kujijua kuwa muangalifu Sana kwenye maamuzi juu ya Maisha yako.

Hata kama ni nabii kama Musa ambaye anasema na Mungu uso Kwa uso ,nakusisitiza tena usijaribu kuacha kazi au masomo au biashara pasipo kumshirikisha Mungu labda kama biashara sio halali Kwa mujibu wa Sheria na maandiko hiyo omba Mungu akufungulie mlango WA kutokea

Na Mungu akubariki
 
Kumtumikia Mungu ni ibada ,kufanya kazi ni ibada .

Kwa hiyo,huwezi kutenganisha kufanya kazi na kumtumikia Mungu.
 
Back
Top Bottom