Genio the great
Senior Member
- Aug 29, 2022
- 159
- 491
Habari Wana jamvi, naiheshimu sana JamiiForums kwani ni forum ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuielimisha jamii katika nyanja mbalimbali.
Na hii ni kwasababu imejawa na watu wengi wenye ufahamu mkubwa juu ya mambo mbalimbali na experience tofauti. Leo nmesukumwa tushirikishane juu ya mada niliyoweka hapo juu.
Viongozi wengi wa dini pamoja na watumishi wengi kwenye shuhuda zao mbalimbali hasa upande wa dini ya kikristo ambayo ninaufahamu nayo Kwa asilimia nyingi kidgo nikilinganisha na dini nyingine.
Huwa wanaongea kwamba waliacha hiki(kazi) wakaamua kufanya hiki(kutumikia Mungu ) Kwa kumaanisha yaani sio Kwa kudonoa donoa.
Nilishawahi kumsikia Mtumishi wa Mungu mwl Christopher Mwakasege akisema zamani alikuwa afisa ugavi selikarin lakini lilipokuja swala la kumtumikia Mungu akaamua kuachana na kazi akaamua kufanya Hilo.
Japo awali anasema alipitia changamoto nyingi sana kwakuwa alikuwa na familia na inategemea mahitaji kutoka kwake lakini Leo tunaona Ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliofanikiwa kihuduma na kiuchumi pia.
Mimi nmemtaja yeye yawezekana nawewe Kuna ushuhuda wa wengine wengi unaowajua wenye senario za Namna hiyo.
Wewe kupitia hili umejifunza nini au unashauri nini mtu ambaye yupo kazini lakini kazi imekuwa kama mzigo kwake na ndani mwake anaona anawito wa kumtumikia Mungu ambao yawezekana ukabadiri hatima yake ikawa Bora zaidi.
Na akiwa anafanya lolote linalomuhusu Mungu Kuna mwanga anauona ila ujasiri wa kufanya maamuzi ya kuacha kazi ndio unakosekana Kwani familia inategemea.
Karibu sana Kwa mawazo na Mungu akubariki.
Na Mwl Kazidi "The code breaker"