Mungu siyo mtumwa wako, hafanyi kamwe mapenzi yako

Ghost boss

Member
May 3, 2019
33
56
Hakuna anayeishi kwa ajili yake

“Mungu wangu, mungu wangu mbona umeniacha”, hii ni kauli ya Yesu alipokuwa msalabani anakaribia kufa, na muda mchache baadaye Yesu alikufa, kumbuka kama yasemavyo maandiko, 'Ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu, na tuko".

Mungu sio Mungu wa wafu ni Mungu wa walio hai, hivyo ili kiumbe kife ni lazima Mungu atoke kwa hicho kiumbe, Mungu aliondoka na Yesu alikufa, basi ndani ya Mungu viumbe vinaishi na vinajimudu na vipo.

Kama ndio hivyo basi kila kiumbe kipo kwaajili ya Mungu, Yesu aliposema "Baba kama ukipenda ukiondoe kwangu kikombe hiki lakini mapenzi yako yatimizwe wala sio yangu," alimaanisha haishi kwaajili ya mapenzi yake ila kwaajili ya mapenzi ya Mungu, na katika maisha yake alikuapo na alijimudu kwani alikuwa ndani ya Mungu.

Basi sisi tupo na tunaishi na kujimudu, yaani tunapata mahitaji yetu kwasababu ya Mungu, hakuna anayeishi bila Mungu, kama pia yasemavyo maandiko;

Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana; ni mzaliwa wakwanza wa viumbe vyote.

Maana kwake vitu vyote vilimbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. vyote viliumbwa kwake na kwaajili yake. Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote uendelea kuwako kwa uwezo wake.

Basi hakuna kati yetu sisi binadamu anayeishi kwa ajili yake, kila kitu ulichonacho ni kwaajili ya Mungu, Mungu hayupo kukutumikia hivyo hafanyi unachotaka, isipokuwa wewe upo kwaajili ya kumtumikia na ni lazima tufanye mapenzi yake.

Sisi hatukuumbwa kwaajili yetu, ila kwaajili yake, hatumiliki mali kwaajili yetu Bali kwaajili yake.

Mara nyingi tunajidanganya na hatujali kabisa kabisa kuwa tulivyonavyo sio kwaajili yetu, na kule kuonyesha hatujielewi tunathubutu hata kumlazimisha Mungu atupe tunachotaka, tuna lazimisha tunafunga, tunalazimisha kusali Mungu atupe tunachotaka.

Kwakweli haitakaa itokee Mungu akakupa unachotaka bali atatupa anachotaka kwa kadili ya mapenzi yake na mpango wake wakufikia jambo lake.

Kila mtu anakitu alichopewa, wengine utajiri mkubwa na wengine vitu mbalimbali, lengo juu ya kupewa vitu hivi ni kumtumikia Mungu nasio kwaajili ya kujinufaisha wenyewe, lengo kuu la Mungu ni atumikiwe sio tujitumikie.

Mungu alituumba kwa faida zake binafsi na sio kwa faida yetu, haina haja ya kulazimisha mambo kwa kuwa lile ulipangiwa litakupata tu.

Mfano angalia kifo, kila MTU hataki kufa lakini tunajua wazi wazi kabisa wote tutakufa, lakini angalia tunavyojitahidi tusiingie kwenye hatari zitakazo tuua, labda tunakimbia kwenye mapigano au vurugu hatari ili kuepuka tusije tukafa.

Pia tunatibiwa kwa madaktari wasomi sana kwani tunajua hapo tutakikwepa kifo kitakacholetwa na ugonjwa, lakini katika jitihada zote hizi, mwisho wa siku tunakufa, tena kirahisi sana, bila purukushani. Sasa kifo kinatokea wapi wakati tunafanya jitihada za kukiepuka kwa nguvu zetu zote?

Mtu akishakufa hapo tunaona wanaitwa mapadri, wachungaji, mashekhi nk ili kufanya ibada na nyimbo za Mungu zinaimbwa, kwa nini lakini tunafanya hivi?

Akili inajua vizuri kabisa ila inaleweshwa kuwa tukiwa hai tupo kwaajili yetu na tukifa kwaajili ya Mungu, nani kakuambia Mungu ni Mungu wa wafu?

Ukweli sisi ndani yake tunaishi, tunajimudu na tuko, basi tukiwa hai tujue kuwa tupo ndani ya Mungu na ndio maana tunaishi na tuna yale mahitaji. Tujue tukifa Mungu hayupo pale maana hakuna kitu kinaishi bila Mungu, kumbuka maandiko yanasema; vyote uendelea kuwako kwa uwezo wake.

Yesu alisema Mungu wangu mbona umeniacha na ukweli akafa, Mungu yupo nasi sasa tunapoishi, bila Mungu hatuna uhai, na wakati wote tunaishi tunatakiwa tuishi kwaajili ya Mungu maana pale yupo karibu kabisa nasi.

Kumchukua marehemu kumpeleka kanisani au msikitini halafu kusali sala ndefu, haisaiidi kitu, kwakuwa Mungu hayupo na yule mfu ndio maana amekufa.

Jambo la muhimu kabisa tuombeane tukiwa hai, tufanye yale ya muhimu tukiwa hai, hatuishi kwaajili yetu na hatukai kwaajili yetu na hatupati mahitaji kwaajili yetu Bali yote ufanyika ili tuweze kupata nguvu ya kumtumikia yeye.

Kumbuka Mungu hakai na maiti ndio maana Yesu alilia Mungu amemwacha, huna haja ya kutafuta utajiri hata ukitafuta kama haipo kwenye mpango wa Mungu kuwa wewe tajiri huwi na hutakuwa.

Kama kifo hata ufanye juhudi kukikwepa utakufa tu na MTU hana namna ya kuimbia hatma yake, kama ni utajiri yeye atakupa nguvu ya kuwa tajiri na kwa faida yake, na yeye atakupa hali yeyote kwa faida yake.

Mungu hajibu maombi yako kwa faida yako bali kwa faida yake, Mungu sio mtumishi wa MTU ila MTU ni mtumishi wa Mungu, kama ilivyoandikwa ukiomba sawa sawa na mapenzi yake atawajibu.

Kwahiyo kuomba ni lazima maombi yetu yawe kwenye njia ya kile alichotutaka tufanye.

Mfano baba wa familia kuomba Mungu ampe uwezo wa kuwapatia chakula familia yake ni maombi sawa kabisa, maana Mungu amemweka juu ya familia na aipatie mahitaji hivyo haya ni maombi sawa sawa na mapenzi ya Mungu na ndio maana Mungu huwapa riziki watu wote wamwombao hata wasio mwomba ili waishi na watekeleze mapenzi yake.
 
Kila mtu anakitu alichopewa, wengine utajiri mkubwa na wengine vitu mbalimbali, lengo juu ya kupewa vitu hivi ni kumtumikia Mungu nasio kwaajili ya kujinufaisha wenyewe, lengo kuu la Mungu ni atumikiwe sio tujitumikie
Sir,,

Lengo kuu ni ili tutumikiane au tutumike kwa ajili yetu sote.

Mungu amekamilika so atake atumikiwe ili aongezeke nini?

Ila sie na viumbe na magimba mengine ndio wenye kuendelea, ndio wenye kuboreshwa siku hadi siku ndio tunaohitaji kusaidiana kufikia malengo kwa kutumikiana.

Labda kama utatafsiri kwamba; kumtumikia jirani ndio kumtumikia Mungu basi hapo tutaenda sawa. Kwamba lengo ni kumtumikia Mungu.

Asante kwa somo zuri ✌
 
Hakuna anayeishi kwa ajili yake

“Mungu wangu, mungu wangu mbona umeniacha”, hii ni kauli ya Yesu alipokuwa msalabani anakaribia kufa, na muda mchache baadaye Yesu alikufa, kumbuka kama yasemavyo maandiko, 'Ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu, na tuko".

Mungu sio Mungu wa wafu ni Mungu wa walio hai, hivyo ili kiumbe kife ni lazima Mungu atoke kwa hicho kiumbe, Mungu aliondoka na Yesu alikufa, basi ndani ya Mungu viumbe vinaishi na vinajimudu na vipo.

Kama ndio hivyo basi kila kiumbe kipo kwaajili ya Mungu, Yesu aliposema "Baba kama ukipenda ukiondoe kwangu kikombe hiki lakini mapenzi yako yatimizwe wala sio yangu," alimaanisha haishi kwaajili ya mapenzi yake ila kwaajili ya mapenzi ya Mungu, na katika maisha yake alikuapo na alijimudu kwani alikuwa ndani ya Mungu.

Basi sisi tupo na tunaishi na kujimudu, yaani tunapata mahitaji yetu kwasababu ya Mungu, hakuna anayeishi bila Mungu, kama pia yasemavyo maandiko;

Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana; ni mzaliwa wakwanza wa viumbe vyote.

Maana kwake vitu vyote vilimbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. vyote viliumbwa kwake na kwaajili yake. Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote uendelea kuwako kwa uwezo wake.

Basi hakuna kati yetu sisi binadamu anayeishi kwa ajili yake, kila kitu ulichonacho ni kwaajili ya Mungu, Mungu hayupo kukutumikia hivyo hafanyi unachotaka, isipokuwa wewe upo kwaajili ya kumtumikia na ni lazima tufanye mapenzi yake.

Sisi hatukuumbwa kwaajili yetu, ila kwaajili yake, hatumiliki mali kwaajili yetu Bali kwaajili yake.

Mara nyingi tunajidanganya na hatujali kabisa kabisa kuwa tulivyonavyo sio kwaajili yetu, na kule kuonyesha hatujielewi tunathubutu hata kumlazimisha Mungu atupe tunachotaka, tuna lazimisha tunafunga, tunalazimisha kusali Mungu atupe tunachotaka.

Kwakweli haitakaa itokee Mungu akakupa unachotaka bali atatupa anachotaka kwa kadili ya mapenzi yake na mpango wake wakufikia jambo lake.

Kila mtu anakitu alichopewa, wengine utajiri mkubwa na wengine vitu mbalimbali, lengo juu ya kupewa vitu hivi ni kumtumikia Mungu nasio kwaajili ya kujinufaisha wenyewe, lengo kuu la Mungu ni atumikiwe sio tujitumikie.

Mungu alituumba kwa faida zake binafsi na sio kwa faida yetu, haina haja ya kulazimisha mambo kwa kuwa lile ulipangiwa litakupata tu.

Mfano angalia kifo, kila MTU hataki kufa lakini tunajua wazi wazi kabisa wote tutakufa, lakini angalia tunavyojitahidi tusiingie kwenye hatari zitakazo tuua, labda tunakimbia kwenye mapigano au vurugu hatari ili kuepuka tusije tukafa.

Pia tunatibiwa kwa madaktari wasomi sana kwani tunajua hapo tutakikwepa kifo kitakacholetwa na ugonjwa, lakini katika jitihada zote hizi, mwisho wa siku tunakufa, tena kirahisi sana, bila purukushani. Sasa kifo kinatokea wapi wakati tunafanya jitihada za kukiepuka kwa nguvu zetu zote?

Mtu akishakufa hapo tunaona wanaitwa mapadri, wachungaji, mashekhi nk ili kufanya ibada na nyimbo za Mungu zinaimbwa, kwa nini lakini tunafanya hivi?

Akili inajua vizuri kabisa ila inaleweshwa kuwa tukiwa hai tupo kwaajili yetu na tukifa kwaajili ya Mungu, nani kakuambia Mungu ni Mungu wa wafu?

Ukweli sisi ndani yake tunaishi, tunajimudu na tuko, basi tukiwa hai tujue kuwa tupo ndani ya Mungu na ndio maana tunaishi na tuna yale mahitaji. Tujue tukifa Mungu hayupo pale maana hakuna kitu kinaishi bila Mungu, kumbuka maandiko yanasema; vyote uendelea kuwako kwa uwezo wake.

Yesu alisema Mungu wangu mbona umeniacha na ukweli akafa, Mungu yupo nasi sasa tunapoishi, bila Mungu hatuna uhai, na wakati wote tunaishi tunatakiwa tuishi kwaajili ya Mungu maana pale yupo karibu kabisa nasi.

Kumchukua marehemu kumpeleka kanisani au msikitini halafu kusali sala ndefu, haisaiidi kitu, kwakuwa Mungu hayupo na yule mfu ndio maana amekufa.

Jambo la muhimu kabisa tuombeane tukiwa hai, tufanye yale ya muhimu tukiwa hai, hatuishi kwaajili yetu na hatukai kwaajili yetu na hatupati mahitaji kwaajili yetu Bali yote ufanyika ili tuweze kupata nguvu ya kumtumikia yeye.

Kumbuka Mungu hakai na maiti ndio maana Yesu alilia Mungu amemwacha, huna haja ya kutafuta utajiri hata ukitafuta kama haipo kwenye mpango wa Mungu kuwa wewe tajiri huwi na hutakuwa.

Kama kifo hata ufanye juhudi kukikwepa utakufa tu na MTU hana namna ya kuimbia hatma yake, kama ni utajiri yeye atakupa nguvu ya kuwa tajiri na kwa faida yake, na yeye atakupa hali yeyote kwa faida yake.

Mungu hajibu maombi yako kwa faida yako bali kwa faida yake, Mungu sio mtumishi wa MTU ila MTU ni mtumishi wa Mungu, kama ilivyoandikwa ukiomba sawa sawa na mapenzi yake atawajibu.

Kwahiyo kuomba ni lazima maombi yetu yawe kwenye njia ya kile alichotutaka tufanye.

Mfano baba wa familia kuomba Mungu ampe uwezo wa kuwapatia chakula familia yake ni maombi sawa kabisa, maana Mungu amemweka juu ya familia na aipatie mahitaji hivyo haya ni maombi sawa sawa na mapenzi ya Mungu na ndio maana Mungu huwapa riziki watu wote wamwombao hata wasio mwomba ili waishi na watekeleze mapenzi yake.
Mungu si mtumwa wako. Kweli.

Kwa sababu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom