Namna ya kusafisha pasi yako

Namna ya kusafisha pasi yako

Chukua panadol au paracetamol weka pasi yako ipate moto vya kutosha igeuze uibane vizuri chukua vidonge vyako kimoja kimoja au viwili. Viwili chukua gazeti au box nene weka vidonge vyako juu yaa pasi sehemu husika yenye uchafu ,vidonge vikianza kuyeyuka kama nyloni anza kuvisugulia pale uchafu wote utaondoka kama bado ongeza vidonge.

WARNING : HAKIKISHA UJIUJI ULE WA ZILE DAWA UNAO YEYUKA AUKUDONDOKEI MAANA NI ZAIDI YA UJI WA NYLON UTALIA KILIO CHA PAKA MWIZI ALIYE PIGWA AU UTALIA KAMA VILE UMESIKIA JINA LAKO KWENYE LIST YA RC WAKATI UNAJUA WAZI HAUFANYI HIYO BIASHARA
PILI ULE MOSHI WA DAWA UNAO TOKA BAADA YA DAWA KUYEYUKA UNAUMIZA SANA SO JITAIDI KUWEKA MBALI NA PUA YAKO PIA UKIMALIZA KUSUGUA FUTA NA GAZETI
Nimekuelewa vizuri na hongera kwa somo zuri sana. Natumai wengi wameelimika. Ila hivi watengenezaji wa hivyo vidonge wanajua huu ubunifu?
 
Hiyo baking soda nayo ni vijiko vya chakula? Napaka na kufuta na kitambaa pasi ikiwa ina moto au ikiwa kawaida?

Naam, kipimo cha baking soda ni kijiko cha chakula pia.

Jaribu ikiwa baridi, ikisaidia huna haja ya kuipasha moto. Ikishindikana pasha moto. Nayo ikishindikana, tupa hiyo pasi nunuwa nyingine.
 
Chukua pasi, pasha moto, tandazo chumvi, fanya ka unanyoosha juu ya chumvi.
 
chukua mkaa.. chomeka pasi kwenye umeme.. kisha iwashe ikichemka sugua na mkaa
 
Siku zote ni vizuri kujua chanzo cha tatizo kabla ya kutatua tatizo lenyewe,

  1. Je kinachosababisha Pasi kupata uchafu ni kipi?
  2. Ni njia gani za kuiepusha Pasi isipate uchafu? (Juu ya paa la Pasi)
 
Siku zote ni vizuri kujua chanzo cha tatizo kabla ya kutatua tatizo lenyewe,

  1. Je kinachosababisha Pasi kupata uchafu ni kipi?
  2. Ni njia gani za kuiepusha Pasi isipate uchafu? (Juu ya paa la Pasi)
Kwa mawazo yangu binafsi kinachosababisha pasi iwe chafu ni kuweka moto mkali kwenye nguo ambazo haziitaji moto mkali
mfano kuna baadhi ya nguo ambazo zinakama nyuzi flani hivi hata ukizikung'uta zinaonekana hivyo vinyuzi ni mojawapo ya chanzo, pia nguo za nylyon ni mojawapo ya chanzo
jitahidi usome maelezo kwenye lebo za nguo ambazo zinakua na maelezo ya utunzaji wa nguo husika (mara nyingi huwa nyuma ya nguo)
 
Safi sana Mkuu.
 
Ni dhahiri kwamba michango ya wadau wote kwenye hii thread yametusaidia wengi kujua namna ya kuondoa uchafu ulioganda kwenye pasi. Lakini pia kwa mtazamo wangu naona kama matumizi ya baking soda, panadol, asprin n.k. ni kama "tiba mbadala" kwa tatizo hilo la pasi.

Swali langu ni kwamba madukani hakuna kitu special kabisa kwa ajili ya kuondoa uchafu huo kwenye pasi?
 
Back
Top Bottom