Namna ya kusafisha pasi yako

Namna ya kusafisha pasi yako

Nani aliyegundua kua panadol inaisha pasi?
Au watengenezaji wa Panadol. Wametoa na maelekezo hayo?
 
Hiyo dawa uliyoisahau ni kidonge cha ASPIRIN.....

ASPIRIN ndiyo kiboko ya kila kitu! Inayeyuka kirahisi sana, na kuondoa uchafu kirahisi pia. Ila sasa, huo moshi wake, mwaweza kukohoa nyumba nzima.
 
Akili za kuambiwa changanya na zako,
Kama ni kidonge Usiiwekee uso karibu, utapaliwa na moshi wake.
 
Sijajua mnaosema panadol au paracetamol mmefanya utafiti wa madhara ya moshi utoakanao na kuungua kwa kemikali hiyo ikiingia kwenye mapafu ina madhara gani? halafu kwa pasi zenye matundu ya kutolea maji chini uchafu ukishayeyushwa na kidonge hicho unajificha kwenye matundu hayo je inasaidia?
Mwanzo nilikua natumia panadol lkn moshi wake ulikua unanisababishia
kupata mafua na kikohozi.
Siku hizi natumia steel wire ngumu zile zinazouzwa kwenye pakti, pasi hutakata vizuri bila ya kuniletea madhara yoyote.
 
Hivi panadol ni dawa au jina la kampuni?

Nauliza tu coz naona wengi wanasema "tumia panadol"
 
Sisi tuliozoea pasi ya mkaa ni mwendo wa kuisugua kwny mchanga mpk inakaa level kabisas.
 
Unaweza kutumia panadol ama colgate. Lazima uipashe sana moto ndipo iweze kusafishika
 
Habari wana JF
Nimekumbwa na changamoto moja ya kupasi nguo zangu mwenyewe zoezi nililoliacha miaka thelathini iliyopita, nimeshika pasi naona ni chafu sana. Huko zamani kuna dawa tulikua tunaiweka alafu uchafu unatoka na yenyewe inatoa moshi mkali, sijui ni panadol au septrin ila nimesahau na ni muda mrefu. Naomba kujuzwa njia nyepesi ili nisiunguze nguo zangu na kuzichafua, Asanteni.

Kama pasi chafu safisha kwa penati
 
We washa pasi yako weka moto mpaka mwisho then anza kuisafisha na ulimi mbona dakika tu itakuwa mbuya!!!
Kamati ya roho mbaya mpaka jf.kweli viwanda ni vya watoto vya chuma na mambo mengine tuwachie wachina[emoji3] [emoji3]
 
Wengi tunajua umuhimu wa pasi,pasi yangu ya umeme imechafuka sana kwenye kitako cha kunyooshea nguo, imekua nyeusi sana kiasi ikipata moto ule weusi unaungua na huwezi tena kunyoosha nguo,inaungua!je,kuna dawa yoyote ya kusafishia kuutoa?zawani nilikuwa natumia vidonge vya panadol kuuyeyusha uchafu huo kisha kuifuta ila kwa sasa imedunda....
 
Back
Top Bottom