Namna ya kupata location ya simu ya mtu kwa namba ya Simu

HabariTech

Member
Sep 1, 2019
8
21
Hivi inawezekana kujua location ya mtu kwa kutumia namba ya simu? Hili ni swali ambalo nimeulizwa zaidi ya mara 10 mpaka sasa. Jibu ni ndiyo inawezekana kupata location ya simu ya mtu kwa kutumia namba ya simu anayotumia katika hiyo simu.

Nilishaandika kuhusu “Kuona location, sms & calls za mtu bila yeye kujua”, lakini inaonekana wengi hawakuridhika na hilo andiko kwa kuwa sikuelezea namna ya kutumia namba ya simu kuona location ya mtu. Hapa nitajibu swali ambalo wengi mmekuwa mkiniuliza.

Nina uhakika katika kila mahusiano (wapenzi) 10 kuna wawili ambao hawaaminiani au wanalindana sana kiasi kwamba wanatamani kujua mwenzake yuko wapi muda wote. Kuna baadhi ya wazazi hupenda kujua watoto wao wako eneo gani muda wote kwa ajili ya usalama.

Asilimia kubwa ya hawa watu huingia google kutafuta “Free phone number tracking”. Hata mimi ni mmoja wa watu nimewahi kufanya hivi hasa nikitaka kuwajua wale watu wa spam calls na spam texts za “ile pesa tuma huku”.

Kuna websites na application nyingi mtandaoni ambazo huwa wanatoa ahadi ya kwamba wanaweza kutrack namba za simu. Bahati mbaya apps nyingi huwa hazina uwezo huo au wanaishia kukwambia nchi tu ya hiyo namba. Nimechambua baadhi ya apps na websites bora kwa ajili ya hii kazi.

1. Truecaller

Truecaller wanasema wanataarifa za namba za simu za zaidi ya watu milioni 300 kutoka nchi tofauti tofauti duniani. Ni kama kitabu cha mtandaoni cha namba za simu za watu. Inawezekana hujawahi kutumia huduma za truecaller ila namba yako ipo huku ikiwa na jina, nchi pamoja na email yako.

Unaweza kupakua truecaller na kuitumia kama application ya phone kwenye simu yako. Ikitokea namba ngeni inakupigia, truecaller itakupa jina la huyo mtu kulingana na data ambazo zipo kwenye dataase yao.

Majina yanayokuwepo kwenye truecaller sio yale ambayo mtu alitumia kusajili namba yake, bali ni majina ambayo yanafata namna ambavyo watumiaji wengine wa truecaller wamesave hiyo namba. Hivyo mara nyingi truecaller huwa inatoa majina yaliyosahihi kuhusu namba utakayopokea.

Moja ya feature nzuri ya truecaller ni uwezo wa kuiweka namba kama spam na ikawa kama tangazo kwa watumiaji wote wa truecaller. Mfano mimi nikireport namba fulani kama spam, hiyo namba itakapo piga simu kwako itaandikwa kabisa kwamba ni spam (tapeli). Hii inaitwa community based spam reporting.

Truecaller ni application ya BURE haujitaji kulipia chochote kuitumia.

2. YoTracker

Hii ni website ambayo inawezesha kuona location ya simu ya mtu kwa kutumia namba ya simu tu.

Features​

  • Rahisi kutumia
  • Haikuhitaji kupakua third party apps za aina yoyote kutumia huduma yao. Kila kitu unatumia kwenye website yao.
  • Inaweza kujua location ya simu yoyote inayotumia Android, iOS, Windows au Blackberry OS.

3. NumberGuru

Kama unachotaka ni kuweka tu namba kisha upate taarifa zote kuhusu hiyo namba basi NumberGuru ndiyo website sahihi.

Features​

  • Imehakikiwa usalama na McAfee Security
  • Inatoa location ya simu za mobile na landline
  • Ni rahisi kutumika na mtu yeyote
  • Ili kupata taarifa zote za hiyo namba na kuweza kuziprint kama pdf utalipia kati ya $1 au $5

4. Online GPS Phone Tracker

Ni website inayokusaidia kujua location ya landline na mobile phones. Inafanya kazi kwa namba za simu za ncho zote duniani.

Ni ya bure, ila ili kupata huduma yake kuna survey ambayo watakuomba ukamilishe kabla hawajakupa majibu ya data unazotaka.

5. Mobile Apps Zinazotumika Kufanya Phone Number Tracking​

Mwisho​

Ni sahihi kusema kwamba teknolojia imefanya kuwa rahisi sana kuweza track simu za watu, lakini huduma hii haipo kwa polisi peke yao. Hata mimi na wewe tumepata uwezo huu kwa sababu ya hii teknolojia. Cha muhimu ni kutotumia hizi teknolojia kwa madhumuni mabaya. Ni muhimu kujihakikishia usalama wakati wote.
 
Nimejaribu hiyo ya 2 na nimeweka namba yangu na inaleta idadi ya msg contact na media ila haifungui. Pia kila uki search namba hyo hyo inaleta hesabu tofauti msg 538 ukisech tena msg 278 ukirudia msg 286 sasa hapa sio halisi.
Hiyo terue caller ndo siwez kuitumia maana haijawah kunipa jibu sahh.
Ngoja nijarb zingine
 
Truecaller nimedownload hakuna kitu,
Ebu fafanua tena

Otherwise it's scum!!!
 
Vipi kwa mtu aliekutapeli unaweza kujua locatio alipo kwa kutumia namba yake ya simu
 
Tupe nondo.... process ulizopitia
Mm nimetumia #truecaller
Ingia google chrome then andika truecaller na ingia kwenye official website baada ya hapo itakuomba ufanye usajili na baada ya hapo utaweka namba ya sim na italeta jina maarufu ambalo wengi wamesave kwenye namba hyo na kukupa access ya kuangalia location ya contact hyo.
Ikiwa kama haitapatikana bas itaonesha pahala ambapo namba ile ilisajiliwa!
 
Vipi kwenye kupata calls na text za mtu bila yeye kujua .inakuaje hapo maana sijaona ulipoandika
 
Back
Top Bottom