Simu ya mkopo imepotea. Naipataje?

Annonymous

JF-Expert Member
May 9, 2013
448
799
Habarini za Asubuhi wana JF
Niende direct kwenye jambo
Nilichukua simu ya mkopo ila ndani ya mwezi ilipotea (niliibiwa ) mahali, tar 24.2.2024). Ile simu kwa wakati huo wote kupitia google find my device ilikuwa inaonekana kwa dkk kama 30 hv kisha ikazimwa (wakatoa line, ikwa offline ndio mwisho) nikareport kampuni ya mkopo wakanielekeza nikachukue loss report nikaenda polisi wakanipatia loss na RB kisha baada ya hapo kama kawaida elf 30 ya kuanzia nkatoa ila huu mwezi wa 2 sijapigiwa simu.

Application ya wakopeshaji nikiingia naiona simu last seen ni tar 23 juzi tu hapa. Nikawasaliana na mkopeshaji akajibu hawezi kuitafuta ni chini ya polisi na polisi wakanielekeza nirudi kwa mkopeshaji (kampuni iliyonikopesha). Wadau hivi kuna taratibu gani za kuipata hii simu. Box la simu lipo na ilikopotelea napoamini bado ipo ni maeneo ya goba, DSM
 

Attachments

  • SmartSelect_20240224-092243_Easybuy.jpg
    SmartSelect_20240224-092243_Easybuy.jpg
    436.2 KB · Views: 13
Jambo ambalo ni hakika,kama ulitoa taarifa kwa kampuni iliyokukopesha imesha iblock simu! Kwa hiyo hata mwizi hana faida nayo!
 
Itakua jamaa aliyeiba anaendelea kulipia, kwanini mkopeshaji asiifunge, au unaendelea kulipa?
Anaendeleaje kulipia wakati unaona kabsa yeye kapoteza tarehe 24.2/ na mara ya mwisho kuitumia ilikuwa tarehe 23/02. So hapo ngoma imezimwa na haiko online.
 
Achana nayo fanya vitu vingine. Na mimi nilipotezaga ndani ya mwezi nikafata process zote ila kuna polisi akaniuliza bei ya simu kisha akasema kwa ushauri wake kama binadamu niachane nayo tu kwa vile naweza kutumia pesa nyingi sawa au zaidi ya gharama ya simu ili kuipata.

Mkopeshaji baadaye akasema niendelee kulipia, nikiwa na mwenendo mzuri watanipa simu nyingine. Nikasema kwanza naomba tafsiri ya mwenendo mzuri wa ulipaji kwa mujibu wa makubaliano hayo ni muda gani, pia naomba hayo anayoongea nije tuandikishane kabisa. Tukapoteana aisee.
 
Achana nayo hiyo, labda kama una vitu muhimu saaana ulihifadhi humo na huwezi pata pengine.

Hata hiyo 30k polisi sijui ulitoa ya nini wakati simu hutoipata.
Hasara sio kwako ni kwa wakopeshaji, wewe ushalipa kwa siku ulizotumia labda kama deni lilibaki kidogo.
 
Polisi ni watu wabaya sana,wanao uwezo kutrack simu ndani ya dakika mbili unaipata ila kwa uhuni wao hawataki kukusaidia.

Kuna jamaa yangu aliibiwa simu akiwa Bunda,kaenda kutoa taarifa polisi wakawa wanamzungusha,akawasiliana na jamaa yake polisi aliyekuwa Geita akafuatilia na baadae akazituma taarifa za simu kwa kituo cha polisi bunda ,polisi walimkamata mwizi mapema sana na mbaya zaidi mwizi alikuwa mtu wa karibuni na mshikaji wangu,

Polisi hawawezi kabisa kufanya kazi kwa uadilifu hata kidogo
 
Back
Top Bottom