Namna filamu zinavyotumika kufundisha Jamii kuhusu Matatizo na Ugonjwa.

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Habarini Wanajukwaana na Watanganyika wenzangu kwa ujumla!
Ni wakati mwingine kama mmoja wa mwanamaendeleo katika jamii yangu kuleta mjadala mpana kuhusu mambo kadha wa kadha yanayoikumba jamii ya Watanganyika. Ni wazi kuwa filamu ni moja ya sehemu muhimu sana ya Maisha ya jamii ya sasa, kupitia filamu tunajifunza kuhusu mambo mengi ya msini kuhusu uchumi, tamaduni pamoja na masuala mengine ambayo yanakuja kwa njia ya picha mjongeo.
1705930630171.png

Ni suala la wazi na mtambuka kabsa kuona kuwa filamu zimekuwa ni sehemu kubwa sana ya kutoa elimu duniani, zikionya, zikielimisha, zikiburudisha na kutunza historia za kale, aidha za makabila au matukio yaliyowahi kutokea zamani. Kuanzia karne ya 19 filamu kadhaa zimepata nafasi ya kupewa sifa na nafasi kubwa ya kuwa ni filamu bora za muda wote, ukitazama filamu za Marehemu Charlie Chaplin utanielewa, au ukitazama filamu za James Bond au Agent 007.

Kwa wenzetu hutumia filamu na tamthilia zao kwa dhima kubwa zaidi kuliko sisi, huko Magharibi kwao filamu sio tu zinaburudisha bali zinakwenda mbali zaidi, filamu zinahifadhi historia mbalimbali, mfano ukitazama filamu za They Shall Not Grow Old, pamoja na Journey’s End za 2018 hizi zimechukua visa na Mikasa ya vita vya dunia vya Dunia WWI. Lakini pia wenzetu hutumia filamu kama sehemu ya kutia moyo wagonjwa na watu wenye matatizo ya kiafya kama vile Kansa au UKIMWI.
1705930951327.png

Ukitazama filamu za My Life Without Me ya 2003 pamoja na Alternate Endings, Makala ya 2019 zinaonesha kwa ukaribu uhalisi wa wagonjwa ambao walikuwa wakipambania Maisha yao dhidhi ya magonjwa haya.

India kuna filamu moja inaitwa Taare Zameen Par nadhani kuna watu wamekwisha kuitazama, ni filamu kuhusu mtoto mmoja ambaye alikuwa na matatizo ya afya ya akili, Ishaan Awasthi, ambaye alikuwa akifanya mambo yasiyo ya kawaida kabsa, herufi zake alikuwa akiandika kinyume nyume, na wakati mwingine hakupenda kabsa kuelekezwa kwa kelele na fujo. Alipelekwa shule ya kwanza ila walimu wakashindwa kufua dafu na wazazi wake wakaamua kumhamishia shule ya bweni, akiwa huko siku za mwanzo zilikuwa ni majanga zaidi, alikuwa akichezea kichapo na kufokewa sana.
1705931251041.png

Msaada wake ulikuwa kuwa ni Mwalimu wa Sanaa wa shule hiyo, jina la utani kama Nikam mwalimu ambaye kwa ucheshi wake ilikuwa ni ngumu sana kuona wanafunzi wakionesha utovu wa nidhamu, mwalimu huyu Ram Shankar Nikumbh maarufu kwa jina la Amir Khan huyu alikuwa pia ndo mwalimu wa shule ya Watoto wenye mahitaji maalumu ya Tulips. Ram ndo anakwenda kuokoa jahazi la mtoto Ishaan ambaye anawaogopa walimu wote wa shule hiyo.

Mwishoni tunaona Ram akifanya utafiti wa ziada kujua tatzo kuu la Ishaan kwa kwenda kwao na kuongea na wazazi wake ila pia anakuja kujua tatizo ni kwenye vitu ambavyo wazazi wa Ishaan walimunulia Ishaan tokea akiwa mdogo, kuna michezo ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kijapani, na Kichina na aliona hii imechangia kwa ukubwa kumfanya Ishaan apate changamoto hiyo. Ishaan anapata nafuu na kupona kabsa na mwishoni anachora picha bora zaidi shuleni na kupendwa sana na walimu na wanafunzi wenzake.
1705931810129.png

Nimeamua kukupa tu wazo kuhusu filamu ya Taare Zameen Par kwa sababu moja, wenzetu wanajua kuandika filamu kuhusu kila nyaja ya jamii, kazi bora kutoka kwa Aamir Khan, iwe ni filamu inayozungumzia rushwa na ubadhilifu wa fedha basi utakutana na filamu za L.A. Confidential pamoja na The Secret Bride, iwe ni filamu yenye ujumbe wa mapenzi makali sana basi utakutana na filamu za Fifty Shades of Grey pamoja na Fifty Shades Darker.

Filamu hii ya Taare Zameen Par mpaka sasa imekuwa ni sehemu ya darasa kwa Watoto wa wazazi bila kusahau walezi haswa katika namna ya kuishi na Watoto wetu, ni filamu ambayo vituo na shule zenye mahitaji maalumu ndani ya India zimekuwa zikiwaonesha wanafunzi wenye changamoto mbalimbali ili kuwatia moyo wa nguvu katika harakati zao.
1705932186770.png

Tujiulize kwa Tanganyika tuna filamu zipi ambazo zimekuwa zikitumika kufundisha jamii masuala ya msingi ukiacha na ngono pamoja na mapenzi tu!? Heri ya Mkojani ambaye anatupatia vichekesho tu! Ila tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Taare Zameen Par ambapo Watoto wenye matatizo ya uelewa wanaweza kupata vitu kadhaa kutoka kwa Ishaan na hata filamu zingine kwa wagonjwa ambao wanaona kama wamefikia mwisho wa Maisha yao, filamu na tamthilia kadhaa zinaweza kuwarudishia tumaini la Maisha.

Ukienda kwenye shule za mahitaji maalumu kama Arun School For Mentally Handicapped pamoja na V. D Indian Society for Mentally Handicaped filamu kama Ordinary People pamoja na Taare Zameen Par zinaoneshwa kwa watoto kama namna ya kuwatia moyo.
1705932510539.png

Je watoto wetu wenye changamoto hii tunawaonesha filamu za namna gani tukiwa nao majumbani?! au ndo mwendo wa HUBA na tamthiliya za Azam!?

Nawasiliwasha!​
 
Back
Top Bottom