DOKEZO Tuzo za Filamu zinazoandaliwa na Bodi ya Filamu zina mchezo mchafu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ni kwa miaka mitatu sasa bodi ya filamu nchini Tanzania imekuwa ikiandaa tamasha la filamu nchini. Na kila mwaka kumekuwa na maneno ya kukatisha tamaa kwa waandaaji filamu nchini kutokana na hisia za kuwepo kwa upendeleo katika kuwapata washindi wa tuzo katika tamasha la Tanzania Film Festival Awards. Jambo ambalo limepelekea baadhi ya watayarishaji wa filamu nchini kulisusia tamasha hili.

Kwa kurejelea tamasha la mwaka huu December 2023, katika Kipengele cha filamu fupi. Filamu ambazo zilipita katika mchujo wa awali zilikuwa filamu fupi 44 tu. Ambapo katika hizi filamu 44 zilizopita hatua ya awali, ndimo ambamo zilitakiwa kupatikana filamu fupi tano zinazoteuliwa (final nomination) kwa kupigiwa kura katika Kipengele hicho. Jambo la ajabu ni kwamba katika filamu fupi tano zilizoingia hatua ya fainali filamu mbili hazikupita katika mchujo wa awali. Filamu hizo ni "Nia" na "Hukumu". Ambapo filamu ya "Nia" ilishinda Kipengele cha filamu bora fupi, na pia ilishinda Kipengele cha tuzo maalum ya majaji.

Kwa kuwa mashindano haya serikali inahusika, ni vema ndugu Kiango Kilozo - Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu atolee ufafanuzi ilikuwaje filamu ambazo hazikupita mchujo wa awali zikapenya kuingia fainali.

Vinginevyo inakuwa ni vigumu kuamini tamasha hili, kwa kuwa halitakuwa linawatendea haki waandaaji wa filamu na tasnia ya filamu nchini. Hivi vinaashiria kuwepo kwa dalili za rushwa katika tamasha hili.

Hapa chini naambatanisha filamu 44 fupi ambazo bodi ya filamu walizipitisha mchujo wa awali. Pia naambatanisha filamu tano ambazo bodi ya filamu waliziteua (nominate) kuwania tuzo Kipengele cha filamu bora, na kisha nitaambatanisha washindi katika vipengele vyote, lakini mahsusi nalenga Kipengele cha filamu fupi.

Screenshot_20231225_140458_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_140458_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_140453_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_140447_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_140458_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_140441_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141130_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141059_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_140807_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141050_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141055_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141050_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141105_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141113_Instagram.jpg
Screenshot_20231225_141152_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom