Namna Biashara ya 'Network Marketing' ilivyonipeleka Polisi

Namna Biashara ya 'Network Marketing' ilivyonipeleka Polisi

Hao dawa yao ndogo sana, huwa nafanya hivi akija mmoja kupiga ngonjera za kujiunga huko lazima atakuganda kama ruba, kila muda ni simu na sms zisizoisha, huwa nawachimba vizuri nijue kiwango ninachotakiwa ili kujiunga mfano inaweza kuwa laki 5 au 7 au milioni kabisa.

Kwakua amenihakikishia utajiri na kanipa matumaini ya kutoboa huwa nawaambia wanikopeshe hicho kianzio, nikivuna nawarejeshea. Hutosikia tena kelele zao na kukusumbua ataacha.

We fanya kulazimisha akukope atatoka nduki nakwambia.

Hiyo ndio mbinu rasmi iliyothibitishwa kufukuza hizi headless zombies.😂😂
Hii nimeipendaa
 
Kuna mzee mmoja aliuziwa wale sungura unaambiwa kilo ni elfu 9-12, kafuga kama sungura 100 hivi Siku anawatafuta wanamwambia tushafungaga biashara,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapana aisee hao jamaa wanaonekana siyo watu wazuri!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mwaka wa kimasomo 2013/2014 niliingia UDSM nikiwa na Moto wa kusoma huku nimekosa Mkopo 100% (sikupata hata baada ya ku-appeal Mara 2). Moja ya mipango yangu ilikuwa ni kufanya Mishe ya kuniingizia kipato.

Baada ya kusoma kitabu Cha Bwana Emilian Busara na Mrembo Grace kuhusu HISA, AKIBA NA UWEKEZAJI nilianza kuwekeza katika Solo la hisa la Dar es Salaam (DSE) nikitumia Pocket money yangu. Hisa za CRDB, TBL, Maendeleo Bank, na hata Swissport nilikuwa nacheza nazo Sana.

Baada ya muda kupita, Ilizuka biashara moja ambayo binafsi sikuielewa kwa Wakati huo. Ila Classmates wenzangu wachache walionekana kuvutiwa nayo Sana na kuiongelea mno. Nilipoelekezwa Mara ya kwanza sikuielewa kabisa labda kwasababu sikuwahi kuona biashara ikifanyika nanna ile.

Baadaye nilikuja kuielewa baada ya kutumiwa video presentation ya jamaa mmoja ambaye aliianza akiwa chuo Tena UD palepale na muda huo akiwa anarekodi hiyo video alikuwa anaenjoy Sana maisha. Anasafiri Sana duniani, anamiliki Discovery moja Matata, mkwanja wake kwa mwezi ni HATARI

That day niliona Kama vile MUNGU kanishushia Neema ambayo nilikuwa naihitaji muda mrefu Sana. Nilianza kufikiria namna nitakavyoboresha maisha ya familia yangu, pamoja na Mimi mwenyewe. Nilianza kuona namiliki gari kabla sijamaliza chuo, nikisafiri dunia, nikitambulika, nk

To cut the story short, baada ya muda nilijiunga kwa kusaidiwa na aliyenionyesha biashara na nikawa 'New FBO'. Baada ya ku-Hustle Sana nikaja nikapanda cheo (level) ambayo 'kwenye Makaratasi' natakiwa niwe naingiza kuanzia 500k Hadi 800k ingawa kwa ground Mambo hayakuwa hivyo.

So Wakati napanda hicho cheo nilipaswa kukamilisha points (mauzo ya bidhaa) Mimi pamoja na timu. Pale tulikuwa tunawekewa Mindset ya ku-push KWA KILA NAMNA Hadi kieleweke na kutokata tamaa. So ikabidi nianze kupiga simu kukopa hela that night. Deadline ilikuwa ni saa 6 usiku.

Baada ya muda nilimpigia jamaa ambaye Sijawahi kumuona Wala kukutana naye Ila alikuwa anafanya hiyo biashara mkoani. Tulionana kwenye group la WhatsApp la timu yetu (wote tulio chini ya Aliyetuonyesha biashara). Nikambembeleza jamaa Hadi akanipa 400k kudadeki. So nikamalizia

Hesabu zangu ni kuwa kuanzia mwezi ujao ningelipwa kuanzia 500k Hadi 800k so ningemrudishia Mwana hela yake na ningeendelea na Mishe zangu.

Hapa ndipo Mambo yalipoanzia kwenda kushoto. Mwezi uliofuatia hakuna mkwanja ulioingia KABISA. Hata Tsh 10 sikukuta.

Kufuatilia nikaambiwa kuwa Kuna tatizo lilitokea Wkt najiunga so Wakati nadhani nilikuwa eligible kupata huo mkwanja, kumbe I wasn't.
Nguvu ziliniishia hii siku. Mbaya zaidi ni kuwa huku kitaa watu wananipongeza na kuona Kama vile nimeshatoka kimaisha Wakati Mambo ni tofauti

Baada ya miezi 2 ya kumzungusha jamaa, alikuja kunifanyia Mishe moja Matata.

Kumbe jamaa alikuja Dar kimya kimya (Kutoka Mtwara anapoishi) akamtafuta dada yake (mwalimu shule Fulani Sinza) akampa namba zangu anitafute Kama vile anahitaji bidhaa ninazouza.

Baada ya kupokea simu nilifurahi na nikamuibukia kule shule bila kujua kuwa najipeleka kwenye tundu la Simba. Na hata nilipofika sikuweza kumtambua mshikaji kwasababu hatukuwahi kuonana Mimi nikadhani ni mwalimu mwenzake Kumbe jamaa ananichora tu ninavyoelezea bidhaa.

Mwishoni akaniuliza unamfahamu mtu anaitwa ___? (Jina la mwana) nikamjibu Ndiyo. Akaniuliza unamfahamu vipi? Nikamjibu pia kuwa tupo naye timu moja katika biashara Ila sikumwambia ishu za kumkopa mwana. Basi akaniambia "huyo uliyekaa naye hapo ndio huyo jamaa Mimi ni dada yake"

Hapa ndipo nilihisi miguu kuishiwa nguvu, jasho la ulimi likinitoka, na hata haja kubwa na ndogo zilianza kuja bila utaratibu waungwana. Acheni kabisa haya Mambo. Nilijiona mjinga Sana hii siku na nikajua kuwa kweli 'Za mwizi ni Arobaini'

Maswali yaliyofuata baada ya hapo sikuweza kuyajibu kiufasaha Tena. Ile confidence ya kuelezea 'ALOEVERA' ilipotea kabisa.
Mbaya zaidi kila nikiwaelezea situation ilivyokuwa hawakunielewa na mwisho wakaamua kuniitia polisi wakisema Mimi ni TAPELI . I wanted to cry that day.

Nilijaribu kupiga simu kwa viongozi wangu japo wanikope hata 200k ya kumfukuza mwana lakini wote waliniambia WAMEFULIA. Hapa ndipo nilipojua kuwa nipo Kwenye BIASHARA ISIYONIFAA. Yaani mtu anayetuambia anaingiza 3-6 Million na yeye Hana hata Senti au hawezi kunisaidia?

So mwisho nilipelekwa kituo Cha Polisi SHEKILANGO pale. Yule mwalimu (dada wa jamaa) alikuwa anafahamiana na afande mmoja. That was a first day napelekwa kituoni Tena nikiitwa TAPELI na MWIZI. it was embarrassing.

Hizi biashara Sio...

Ni Mungu tu aisee aliyefanya nitoke Polisi that day. Niliweka Bondi devices zangu pamoja na zile bidhaa zote ndipo tukaandikishiana pale mbele ya afande.Hivyo ndivyo nilivyotoka siku ile. Hela zote mfukoni walibeba bahati nzuri nilikuwa na hela ndogo kwenye soksi ndio ikawa nauli

Toka siku hiyo, sikutaka kusikia Tena ishu za ile biashara. I started to be dormant and baada ya muda niliiacha. Kuna sababu nyingine nyingi pia zilichangia Ila Leo tuijue hiyo moja tu.

Mpaka Leo sitaki kuzisikia hizo kampuni zinazoendesha hizo biashara. KABISA.

---MWISHO-

Mwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi huwa nailaumu sana serikali kwa kutokutambua hizi companies ni za kitapeli kabla hazijaleta madhara katika jamii. Kuna taasisi za kiserikali zinatakiwa kufanya screening ya hizi companies kabla hazijaanza kufanya kazi ila wanakuja kukurupuka baadae kabisa
 
dah mimi kuna siku rafik wa karibu alinishtuwa niibuke makumbusho so akanishawishi sanaa kuhusu Global Alliance mpaka akanionesha chini pale magari yamelundikana vijana wadogo wanaomiliki kupitia Global Alliance.jamaa alikuwa hachoki kunitafuta. nashukuru nilimchana live sina hiyo ela ya kupoteza.tangia siku hiyo no more stories.[emoji23][emoji23]

Haaa haaa ulikataa kuwa mzee wa Good morning?
 
Huu ujumbe inabidi ufike mbali zaidi... Usiishie hapa jukwaani tu, pole na yote Ndugu mtoa mada.
 
Haaa haaa ulikataa kuwa mzee wa Good morning?
aisee ukienda pale makumbusho utakuta vijana wengi sanaa wametupia inawezekana ndio dress codes zao (suti na tai juu) wanawashawishi vijana wenzio most of them ni wanachuo.unabaki unacheka na kuwahurumia tu [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kuna shost kaniitia biashara. Nikajua kafungua duka nikabeba na pesa nikamuungishe.
Kwenda ananipeleka kwenye hiyo ofisi.

Kwanza wenyewe wako tense. Inaonekana ni watu wameingizwa mkenge na wanatafuta pa kupumulia. Wanafake kujiamini wakati midomo na mikono inacheza. Wanaongea kama wako mbele ya hakimu na wao ni wakosaji.

Baada ya maelekezo ya makbrasha na hadithi za mafanikio niliwauliza gharama za bidhaa ya bei rahisi, nikaambiwa milioni 1. Wakaniuliza itachukuwa muda gani mimi kupata watu wawili nikawaambia labda mwaka. Shost na huyo mtaalam wakacheka kile kicheko cha maumivu. Then huyo mtaalam akarudia tena kunieleza huo mfumo wa malipo. Mi nikamuuliza yeye sasa yupo level gani akaniambia ni siri.
Nikaondoka vizuri bila kiashiria chochote kibaya.
Nikumuuleza shost saa ya gharama naweza kujinunulia ni sh 200,000. How nikanunue ya milioni 5 na mi si slayqueen? Huo utajiri unakujaje kwa matumizi ya anasa namna hii.

Ana watoto halafu weekend anashinda huko kwa ajili ya team work. Team work usiwe na muda wa familia wala kupumzika. Biashara yenyewe ya kuwashawishi wenye ndoto za utajiri kununua vitu vya anasa na huduma za anasa wapi na wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
IMG-20200130-WA0010.jpeg

QNET HAOOOO
 
Back
Top Bottom