Amroga aliyeshare naye biashara mpaka kuwa chizi

Amroga aliyeshare naye biashara mpaka kuwa chizi

Kevzy

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2026
Posts
969
Reaction score
1,696
Kwema-story ya kweli ambayo imenihusu moja Kwa moja na inaniumiza akili mpaka leo 2026 nikimuona jamaa akiwa chizi, cha ajabu akiniona ananifurahia na kutaka tukae tupige story

Moderata-kichwa cha habari kiache hivyo hivyo, tafadhali

2014, miezi ya mwanzoni asubuhi nimeamka Kwa kuchelewa nawahi kazini k/Koo , ghafla naitwa Kwa jina langu, fulani fulani samahani naomba unisubiri tuongee, nikamsubiri anikaribie baada ya salamu nikamwambia kuwa nimechelewa kazini kana jambo lako sensitive sana naomba tuongee jioni baada ya kurudi miangaiko yangu huko mjini Kwa masikitiko makubwa yule jamaa akanambia naomba tuongee Sasa hivi kaka tafadhali

Ni jamaa ambaye tumekuwa pamoja mtaani na michezo ya hapa na pale utotoni, na alikuwa ananishtakia kuhusu yeye na rafiki yetu mwingine ambaye watu wengi wanadhani ni ndugu yangu kutokana na ukaribu wetu

Jamaa akaanza kunambia kuwa wameingia share kwenye biashara na huyo rafiki yetu mwingine na biashara ina mwaka na miezi minne, na katika makubaliano yao kuwa pesa ya faida wataihifadhi bank ikiwa nyingi zaidi watagawana, kipindi ananishtakia bank account yao ilifikisha million 12, so baada ya pesa kuwa nyingi matatizo yakaanza, jamaa akawa anamtenga mwenzake na kuanza kumnyima majukumu na kufikia kuamisha ofice ilipo na kumficha alipoiamishia mambo yalianza kuwa mengi kati ya wawili walioshare hiyo biashara yao , huyo jamaa aliyekuja kunishtakia alisema kuwa huyo share mwenzake kwenye biashara kuwa anamroga, na anaomba niongee naye aache kumroga, na alinambia ikiwezekana amuachie pesa yote kwenye biashara Yao hiyo na ampe pesa aliyoweka kama share Ili kila mtu afanye mambo yake/waachane na kumbuka kuwa watu wengi wanajua huyo share mwenzake ni ndugu yangu ndio maana kaja kuniomba msaada niongee naye, nikahoji amejuaje kama anarogwa, jamaa akanambia kuwa hapo kwao huwa wana utaratibu wa kusoma dua kila ijumaa, wao ni waislam

So huyo msomaji dua/ostazi,sheikh baada ya dua ndio akamwambia kuwa awe makini na share wake kwenye biashara sio mtu mzuri kwake, kuwa anamchezea kimazingara, yeye na mama yake pamoja na sheikh walifanya jitihada za kumuita jamaa kuongea naye lakini alikataa so kaamua atafute ndugu zake aongee naye na kudhani mimi ni ndugu yake, akawa ananiomba nizungumze naye na nimuombe aache kumfanyia vitendo hivyo vya kumroga, kumbuka hiyo ni 2014

Katika visa jamaa alivyokuwa ananithimulia yeye na share mwenzake kwenye biashara alinambia kuwa, Kuna kipindi jamaa alikuwa na shida na laki 3 akasome course fulani veta na alimuomba mwenzake watoe laki 6 wagawane Ili yeye aende shule ila mwenzake alikataa alimwambia kuwa wamekubaliana wasitoe pesa mpaka zitapofika nyingi zaidi , hiyo siku nilichelewa kazini aisee kumsikiliza huyo jamaa maana alitake time, kunielezea na kazini sikufanya kazi kwa utulivu

Na ilivyokuwa mpaka wakaingia share , huyo anayemroga mwenzake, ndio alikuwa na biashara ila ikayumba na akafunga kampuni yake, baadae akasikia huyo mwenzake kapata pesa za mgao katika familia yake , akenda kumuomba waingie share Ili waendeshe biashara wote na jamaa alitoa pesa taslim million 1.5 wakaiingiza kwenye biashara na biashara ikainuka Tena ndio mpaka wakafikia na pesa hizo million 12 kwenye account yao, walikuwa wanafanya biashara ya matunda, kupeleka kwenye masuper market, jamaa alisajili kampuni so walikuwa wanajulikana super market nyingi kupeleka matunda tofauti tofauti, kutoka mikoa tofauti, matunda mengine walikuwa wanatoa masokoni humu humu dar es salaam

Nilimpa jibu gani baada ya kuniomba nikaongee naye huyo share mwenzake, niliingiwa na wasi wasi nilimwambia, kwanza yule jamaa sio ndugu yangu wa damu ila ni family friend, wazee wetu walikutana kwenye office flan walikuwa wakifanya kazi wote huko ndipo ukaribu ulianza

Na nikamuelekeza ndugu zake jamaa , pamoja na mjomba wake ambaye anasikilizana naye sana na nilimwambia aende akaongee naye atamsaidia kumuita jamaa aongee naye, baada ya mambo yao ya kibiashara kwenda vibaya

Then nilimuuliza hawakuandikishiana popote kuwa wanaingia makubaliano ya kuingia share ya biashara, yaani nilimaanisha hakukuwa na maandishi au barua ya mjumbe/ mwenyekiti alisema hapana hawakufanya hivyo

Binafsi nilihofia kuwa kimbele mbele, nikaona unaweza ukajifanya mjuaji ukarogwa wewe Kwa mambo yao wenyewe

2014 kati kati ya mwaka nilipataga trip za mikoani nikasafiri
So baada ya mizunguuko yangu huko mikoano nilirudi dar mwaka 2016 nilimkuta jamaa aliyenishtakia kuwa anarogwa ni chizi , yaani ni chizi kabsa , amechanganyikiwa akili, mchafu mchafu, nywele nyingi kichwani anazurula tu mitaani na ana soda mbili huku peps huku coca anakunywa aisee hatari, alitaka kunipa soda moja nilikataa, cha ajabu anakumbuka watu, aliponiona alinikimbilia na kunipa huge, yaani alinikumbatia kwa furaha na kuanza kupiga story, moyo wangu ulijawa na simanzi na nikajihisi mwenye hatia sana moyoni mwangu, yaani nilijiambia moyoni , pengine ningepigana kuongea na kusuruhisha lile jambo jamaa asingekuwa hivi, aliniomba nimnunulie chakula nilimnunulia

Nilivyofika home, nililia na kusononeka usiku mzima, na kujiuliza kuwa hii ni kweli imenikutia mimi au naota , sikuamini kabsa nilichokiona aisee iliniuma sana na inaendelea kunitesa sababu mpaka hii 2026 jamaa bado tu hana hali nzuri, ni chizi kabsa yaani

Inasemekana jamaa aliyemroga hiyo 2014 , alifatwa na kuelezwa kuhusu yeye na share mwenzake, kwanza alikataa kama kaingia share naye na wala hajawahi kupokea pesa kwa huyo mwenzake , alikataa katu katu, na kuhusu kumroga alisema kuwa hawezi kufanya hivyo kwani hakuna sababu ya kumfanyia hivyo, aisee usikubali kuingia makubaliano na mtu bila maandishi na mashahidi ni muhimu sana aisee, wajumbe,wenyekiti, ni muhimu isidharau

Hii ni 2026 , huyo jamaa inasemekana amemroga mwenzake ana zinga la jumba hapo madale na amelimaliza teari ila nasikia bado ajaamia, aisee kwa M/Mungu huko tutaenda kustaajabu vitu vingi sana aisee

Inanitesa sana kama mimi ndio nimemfanyia hayo mambo na isitoshe alishafatwa na kuongea na alikataa kuwa hajamfanyia hivyo mwenzake na Bado ina nitesa yaani asingefatwa kweli nashangaa inanitesa Nini? Najiona kama shahidi kwenye hili jambo, M/Mungu azidi kunipa moyo wa huruma hivi hivi

Hii story nilishawahi kuiwasilisha humu JF mda sana nikiwa na I'd zangu tofauti tofauti za zamani kama utaikumbuka hii story ujue ni mimi nimeileta tena nikiwa nimezaliwa upya, usiache kufanya ibada mwana JF, hakika Kuna nguvu kubwa zaidi ya nguvu zote sijui utaiitaje utajua mwenyewe kama ni NATURE, M/MUNGU, ALLAH, JESUS, YEHOVA, au vyovyote utakavyoita ila ipo nguvu inayotuongoza wote na itulinde aamini


M/Mungu atunusuru, amiina
 
Mimi nafikiri watu wanaodai wanarogwa wana matatizo ya akili. Wengi wanakuwa hawako sawa kichwani
Kulingana na namna ulivyotandikwa mkuu... Uchaw mwingine ww mwenyew huwez jua kam umerogwa, ila wengine ndio wanajua...

Mwingine unatandikw uchaw na gwiji ambaye anataka had ww mwenyew ujue ili ujichanganye kulipiz kisas kumbe ana genge la kiroho
 
Back
Top Bottom