Namiss sana huyu mtu msinishangae!!

Namiss sana huyu mtu msinishangae!!

hongera umeshapewa pewa yingi shoga angu,mi nina swali la kizushi, huko aliko unauhakika gani kama hakusaliti je na we hujapata ki bosile hapo ofisi?mwanaume kuvumilia hiyo mikiki ya nyoka huwa hawawezi kuvumilia for so long.

ukimchunguza kuku humli endelea hivyo hivyo miaka 50 ya ndoa itakuhusu.hureeee!
nijuavyo mimi mitongozo ipo tu, hii huwaga wala haipangwi but, ishu ni kuamua tu.
niko mkubwa sana Klein wangu form 4 sasa nikiwaza kuanza kuruka ruka huon tutabambana kwenye kordo za gesti?? hii tu ni sababu tosha ya kunifanya niishe maisha ya usafi ili wasije sema hata mama allikuwa anafanya hivi
 
hongera saaaaaaaaaaaaaana kwa kutamani tena na tena kuwa karibu na mumeo kwani kuna wengine wanatamani kila siku mke au mume asafiri kwa jinsi alivyomchoka,pole kwa upweke pia.

thanks mamiii
 
i wish wanawake wote wangesoma ulichoandika, nadhani wangejifunza kitu kwako, kama dada mwenye busara asiyebomoa ndoa kwa mikono yake mwnyewe!! Hongera en Be blessed,
thanks mkuu............but ni hisia zangu tu kitu ambacho chaweza kisiwe common kwa wote
 
sijui kama ni funzo kwa wengine ila najua tu nimeeleza ninavyojiskia moyoni..................ukweli leo siko poa nimemiss sana sana kiasi kwamba natamni nipewe poo niletewe tuongee kisha arudi kwenye kazi zake.
gfsonwin!!!
usingeandika tarehe ya hiyo ndoa ningedhani 'nimefumania' id ya wife jf...
coz we are suffering the same...
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin, hongereni sana Mungu aendelee kuwalinda na changamoto za dunia.
Sasa nimejua ni kwa nini huwa unamwaga mapwenti hapa kuhusiana na masuala ya ndoa na mahusiano, kumbe ndoa yenu imekula chumvi nyingi eh.....!
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin!!!
usingeandika tarehe ya hiyo ndoa ningedhani 'nimefumania' id ya wife jf...
coz we are suffering the same...

jamani pole sana sana.
sio mimi bana ila nafurah kwamba siko peke yangu so tunabadilishana experience. ila haya ni maisha magumu ever, bora kipindi mko wachumba but not mkiwa tayari ni mume na mke
 
Hongera sana bibie, si mchezo miaka 11. Sasa jamani kwenye hali kama hizi za kutengana ki utafutaji lazima kale ka kitu kanaitwa (savings) katunishwe ili mida kama hii mtu unachofanya ni kuvizia hizo visa na ticket unaruka fasta kumchungulia halafu basi.

Nimefurahi unampenda mume wako! Mungu akubariki sana. Happy Womens Day!!!
 
Pole sana teacher gfsonwin,

Ila kweli hakuna mtu anayeweza kujiganga hata kwa mambo madongo.....

Yaani hata kwa technologia yote...mmeshindwa kumalizana???

Kazi kwelikweli....:A S shade::shut-mouth:

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin, hongereni sana Mungu aendelee kuwalinda na changamoto za dunia.
Sasa nimejua ni kwa nini huwa unamwaga mapwenti hapa kuhusiana na masuala ya ndoa na mahusiano, kumbe ndoa yenu imekula chumvi nyingi eh.....!

namshukuru sana Mungu kwa hilo Mtambuzi ila tu leo akili imekaa vby sana nafikiri nahtaj chines tea ili kuwa sawa.
 
Last edited by a moderator:
jamani staki mtu anishauri ila tu nataka nishee na nyie experience hii ....

Hiyo kauli hapo juu imeniziba mdomo, lakini sikubali acha nikuache hata na neno moja .....

Hongera sana kwa kutimiza miaka hiyo ya ndoa, na nawatakia kheri na maisha marefu yenye kila baraka za mwenyezi Mungu!!!
 
nijuavyo mimi mitongozo ipo tu, hii huwaga wala haipangwi but, ishu ni kuamua tu.
niko mkubwa sana Klein wangu form 4 sasa nikiwaza kuanza kuruka ruka huon tutabambana kwenye kordo za gesti?? hii tu ni sababu tosha ya kunifanya niishe maisha ya usafi ili wasije sema hata mama allikuwa anafanya hivi

kidogo umejibu, ila ukubwa wa umri haihusiani kabisa na mihemko na ukifika umri wa ukubwani mihamu ndo inaongezeka sa we unawezaje kuhimili mikiki ya mihemko na mitongozo klein mtoe kabisa,na kuna zile siku zote yaaan hata kama yuko mbali utatamani umfate je umefanikiwaje kuzikabili au una njia mbadala?.
 
hepi anivesari mwalimu gfsonwin
ndoa yako furaha yako gfsonwin
Mola umtukuze, utukufu wake usiguse
za wengine ndoa zasambaratika, yako yaimarika
Mola umtukuze, utukufu wake usiguse
gfsonwin na G kila la heri niwatakie
upendo wenu somo kwa wengine
 
Pole sana teacher gfsonwin,

Ila kweli hakuna mtu anayeweza kujiganga hata kwa mambo madongo.....

Yaani hata kwa technologia yote...mmeshindwa kumalizana???

Kazi kwelikweli....:A S shade::shut-mouth:

Babu DC!!
hahahahhhaha! babu nimeskype lakin bado.
kiu yangu nimuone nimguse, aniguse,
tukae mezani tule sote, tulale pamoja,
niwajibike kike juu yake like kumuandalia nguo kumtandikia kitanda
yaani utu tuvitu utu ndo nliotumiss kuvifanya juu yake.
huwaga vinaleta raha fulan, hebu pata picha bibi asbh anahangaika kukubrashia kiatu uvae na nguo kanyoosha unafkiri haskii raha??

nakwambia hivi vina raha kuliko hata ya mpera wenyewe.
 
Hiyo kauli hapo juu imeniziba mdomo, lakini sikubali acha nikuache hata na neno moja .....

Hongera sana kwa kutimiza miaka hiyo ya ndoa, na nawatakia kheri na maisha marefu yenye kila baraka za mwenyezi Mungu!!!
amen kaka mkubwa hiyo niliiweka manake nilijua niiacha blank watu watanishauri kisha nianze kulia si unajua kummiss umpendaye kunavyotesa??
 
Very Geurgious, miaka 10 unammisi Mr namna hii...This is the love of all, Mungu akupe faraja ya kumsubiri. Bravo my sister
 
kidogo umejibu, ila ukubwa wa umri haihusiani kabisa na mihemko na ukifika umri wa ukubwani mihamu ndo inaongezeka sa we unawezaje kuhimili mikiki ya mihemko na mitongozo klein mtoe kabisa,na kuna zile siku zote yaaan hata kama yuko mbali utatamani umfate je umefanikiwaje kuzikabili au una njia mbadala?.

labda hukunielewa kila jambo ni maamuzi tu, na Klein nimemweka kama moja ya factor. nijuavyo mimi tamaa zangu za mwili haziwez kuushinda utash wangu. the thing is siwez kuwaza kitu amvbacho sina uwezo nacho kwasasa.
 
Jamani mwaka 2002/4/21 ilikuwa ni siku ya ajabu sana maishani mwangu as ilizima taa ya ukapera na kuwasha taa ya u-mke wa mtu.

sijui nini kipo akilini mwangu leo, manake hata kazini sijaenda, but i feel like nimtakie hubby wangu happy anniversary ya 11 yrs ya ndoa wakati siku haijafika. I know kwa hii miaka 10 iliyopita haikuwa migumu sana kwetu, but pia haikuwa rahisi. najua aliponikosea na nilisamehe na hata pale nilipokosea nilikiri na akasamehe na kusahau.

usiku wa leo nimelala na mawazo sana as if labda ndio nasubiria siku ya ndoa, nimemuwaza sana hadi kujikuta nashindwa hata kuconcetrate kwenye mambo ya msingi, i wish angekuwepo karibu labda angejua nnavyojiskia, nimemuemail, nimeskype nae but bado kiu yangu haijaisha, natamani nipae niende alipo labda nikisema nae usoni atajua jinsi gani ambavyo najiskia juu yake. ameniambia mengi matamu lkn bado kiu haijakatika nimetizama nguo na viatu vyake nikajikuta nalia wapendwa kwa kummiss mume wangu!!!!!!!!!!

seriously G nakumiss honey..................yaani hata aya matakataka ya skype hayana maana kwangu maana ni uwepo wako tu nauhitaj kwangu.
aaaggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrr nashindwa kufanya kazi mwenzenu nisaidieni. mbaya zaid sasa na yeye anaumia the same as mimi kiasi kwamba anafika mahali anasema aache kilichompeleka arudi nyumban but nikifikiria life wise hiyo sio akili.

jamani staki mtu anishauri ila tu nataka nishee na nyie experience hii ninayoipata ili mjue kabla ya kuamua kutengana kwaajili ya kwenda kutafuta maisha mnatakiwa mfikirie mtafanyaje kwa maisha yaliyobaki.
cacico na snowhite msiseme kitu kwenye huu uzi.

Miss you sana sana baba Klein wangu mwaaaaaaaaaah!

Mnajuana wenyewe bana, maana siku hizi shetani anajiinua sana hata kama mtu ana kakidumu kakumliwaza hawezi kushindwa kuandika haya...samahani lakini. Hii imenikumbusha nikiwa chuo somewhere kuna dada nilikuwa nimejitambulisha mpaka kwao for marriage. Alikuwa ananiandikia E-mails hizo mpaka sasa nime-zi save na kibaya zaidi mpaka rafiki zangu walikuwa wanamuonea huruma jinsi anavyopata taabu kutokuwa karibu nami, lakini baadaye nikaja ku-porve beyond reasonable doubt kwamba ananiibia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom