Namhurumia Maggid Mjengwa

Namhurumia Maggid Mjengwa

"Anna Makinda akishinda hiyo kesho Iringa inaingia katika rekodi ya kutoa Spika kwa mara ya pili katika historia yaalikuwa Mhehe na Anna Makinda ni Mbena, wote ni hao hao".

Maggid article hii kidogo ina walakini siamini kama umeiandika kwa hisia za ukabila lakini hukufanya utafiti wa kina na kujiuliza je mhaya ama mkurya akisoma habari hii ataielewa vipi? Ninachokushauri jaribu kuweka hypothesis kabla hujaandika habari, lengo ni kuelemisha jamii.

Hii ni kauli iliyojaa haiba za "political correctness' za kisomi. Ndiyo maana unaona maneno kama "siamini" "kidogo" "walakini" "hisia" etc.

Kwa sie tusotaka kuremba mara nyingine tunaweza kurahisisha ujumbe zaidi.

Majjid, acha ukabila ! Huyo Nyerere unayesema kumuiga akiona utumbo huu atachefuka.
 
Mimi namfahamu kwa karibu sana Maggidi Mjengwa, kiukweli kabisa yeye si mtu anayeweza kununuliwa kiurahisi. Nimefanya kazi naye kwenye sehemu mbalimbali za tasnia ya habari na ujenzi wa jamii,lakini sikuona dalili kama ni mtu anayekubali kiurahisi kuwa na "Bei" kwa mafisadi au watu wengine.

Lakini Makala zake za hivi karibuni kwenye gazeti la Raia Mwema na picha anazozitundika kwenye blugo yake zinanipa maswali mengi sana. Ni makala na picha zinazoonyesha kama vile Mjengwa ameshawapigia magoti Mafisadi. Sijui ni nini kimemkuta Maggid Mjengwa. Kwa dhati kabisa namuonea huruma.

Anasubiri kupewa Ukuu wa Wilaya (mpya) ya KUNDUCHI! LOL Au ya Msoga?

Hahahahahah!
 
Mwalimu/ Mkufunzi Majjid rudi shule kasome tena historia ya nchi yako ili uweze kufundisha vizuri, kabla ya hapo sahihisha blog yako. Spika wa kwanza chini ya Nyerere Tanganyika alikuwa A.Y.A Karimjee, na wala si Adam Sapi Mkwawa.

Ndiyo maana jengo lililokuwa la bunge Dar linaitwa "Karimjee Hall"

Kwenye blog yako umeandika

mjengwa

Kiranga,

Nimeona hiyo, ahsante kwa kunisahihisha. Kuwa mwalimu si kuwa malaika. Niliposti items hizo nikiwa na haraka ya safari ya Njombe kutoka Iringa jioni ya leo. Pole kwa usumbufu.
 
Mimi namfahamu kwa karibu sana Maggidi Mjengwa, kiukweli kabisa yeye si mtu anayeweza kununuliwa kiurahisi. Nimefanya kazi naye kwenye sehemu mbalimbali za tasnia ya habari na ujenzi wa jamii,lakini sikuona dalili kama ni mtu anayekubali kiurahisi kuwa na "Bei" kwa mafisadi au watu wengine.

Lakini Makala zake za hivi karibuni kwenye gazeti la Raia Mwema na picha anazozitundika kwenye blugo yake zinanipa maswali mengi sana. Ni makala na picha zinazoonyesha kama vile Mjengwa ameshawapigia magoti Mafisadi. Sijui ni nini kimemkuta Maggid Mjengwa. Kwa dhati kabisa namuonea huruma.

Ukweli nashindwa nikuweke katika kundi gani, ila nitakuweka katika maombi ili mungu akufungue uweze kuona na kuelewa ukweli. Mjengwa ana haki zote za kuamini kile anacho amini ili mradi havunji sheria za nchi.
 
Kiranga,

Nimeona hiyo, ahsante kwa kunisahihisha. Kuwa mwalimu si kuwa malaika. Niliposti items hizo nikiwa na haraka ya safari ya Njombe kutoka Iringa jioni ya leo. Pole kwa usumbufu.

Siku nyingine ukiwa na haraka usipost, ngoja utulie. Halafu haraka ndiyo inasababisha umtaje Mkwawa badala ya Karimjee?

Vipi kusema "nilikuwa sijui hili, ahsante kwa kunijulisha" ? Kama huna uhakika na unachoandika fanya ucunguzi kwanza, kuna vijana hawajui historia ya nchi yetu, watakufanya wewe kama primary source hasa kwa sababu ushawaambia wewe mwalimu, utawapotosha.
 
Huyu jamaa mnayemuongelea hakuna ya kubishana hapa na kupoteza muda yy njaaaaaaaaaaaaaaaa ndo inayomfanya abadilike na wala sio kuwa anapenda kununuliwa na Mafisadi,Majidi Mjengwa kachoka unacheza na njaaa kudadeki:doh:
 
Mjengwa ana haki ya kutoa hisia zake kama mtanzania yeyote...huna sababu ya kumhurumia kwa kuwa tu huungi mkono hoja zake.
 
Siku nyingine ukiwa na haraka usipost, ngoja utulie. Halafu haraka ndiyo inasababisha umtaje Mkwawa badala ya Karimjee?

Vipi kusema "nilikuwa sijui hili, ahsante kwa kunijulisha" ? Kama huna uhakika na unachoandika fanya ucunguzi kwanza, kuna vijana hawajui historia ya nchi yetu, watakufanya wewe kama primary source hasa kwa sababu ushawaambia wewe mwalimu, utawapotosha.

Kiranga,
Ahsante sana kwa ushauri. Hilo la Karimjee nalifahamu, nilighafirika kutokana na haraka. Na sina maana huwa sifanyi makosa. Nayafanya mengi, na ni nani asiyefanya makosa?

Hapa kuna simulizi; ( Wanazuoni wa Kiislamu mnikosoe kama nimekosea mahali).

Kuna kisa pale Mtume Muhammad S.A.W aliposwalisha swala ya isha ( Salat al- 'Isha) pale Medina. Swala ya Isha ni swala ya usiku. Kwa kawaida ya swala ya isha ina rakaa nne. Usiku huo Mtume Muhammad S. A. W alipitiliza, akaswalisha rakaa tano. Mtume alipomaliza, muumini mmoja akajenga ujasiri, akamwuliza; " Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu, jambo la ajabu leo umeswalisha rakaa tano badala ya nne. Labda umepokea maagizo mapya kutoka kwa Mwenyezi Mungu".

Mtume akaonekana kushangaa, naye akawauliza waumini wengine. " Je, leo nimeswalisha salat al-Isha kwa rakaa tano?"

"Naam, Mtume wa Mwenyezi Mungu". Mtume alijibiwa na waumini.

Mtume Muhammad S. A. W akatamka; " Ndugu Waislamu wenzangu, mie ni mwanadamu kama nyie. Mniwie radhi, nimeghafirika".

Naam. Hata Mtume wa Mungu alikiri mapungufu. Sembuse sie wanadamu.
 
Wakati mwingine bwana lazima tukubali kwamba humu ndani Jamii Forum tunaleta topis za ujinga ujinga tuu! Yaani ni ufyolo mtupu kwenda mbele!! Maggid ni mwandishi wa jamii na amefungua blog yake na anatoa makala kwa maoni yake mwenyewe, and, guess what? He is entitled to his own opinion!

If you do not like what he wants why do you open his and Michuzi's blogspots? At least they are doing something they passionately like - what the hell have you done? Sam pipo bwana!!!

Maggid, uuseli vanyalukolo vatige navalonge swela! Keep up with what you and Michuzi are doing in your blogspot and all the best!!
Nilikuwa nakusoma kwa umakini nikidhani kuna la maana unaloandika kumbe ni ukabila ndio unakusumbua.
 
Kiranga,
Ahsante sana kwa ushauri. Hilo la Karimjee nalifahamu, nilighafirika kutokana na haraka. Na sina maana huwa sifanyi makosa. Nayafanya mengi, na ni nani asiyefanya makosa?

Hapa kuna simulizi; ( Wanazuoni wa Kiislamu mnikosoe kama nimekosea mahali).

Kuna kisa pale Mtume Muhammad S.A.W aliposwalisha swala ya isha ( Salat al- 'Isha) pale Medina. Swala ya Isha ni swala ya usiku. Kwa kawaida ya swala ya isha ina rakaa nne. Usiku huo Mtume Muhammad S. A. W alipitiliza, akaswalisha rakaa tano. Mtume alipomaliza, muumini mmoja akajenga ujasiri, akamwuliza; " Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu, jambo la ajabu leo umeswalisha rakaa tano badala ya nne. Labda umepokea maagizo mapya kutoka kwa Mwenyezi Mungu".

Mtume akaonekana kushangaa, naye akawauliza waumini wengine. " Je, leo nimeswalisha salat al-Isha kwa rakaa tano?"

"Naam, Mtume wa Mwenyezi Mungu". Mtume alijibiwa na waumini.

Mtume Muhammad S. A. W akatamka; " Ndugu Waislamu wenzangu, mie ni mwanadamu kama nyie. Mniwie radhi, nimeghafirika".

Naam. Hata Mtume wa Mungu alikiri mapungufu. Sembuse sie wanadamu.

Maggid kwanza nakupa hongera sana kwa kuja kwenye forum kujitetea inaonyesha umekomaa au unaendelea kukomaa, mtu kama Michuzi hawezi kutia pua yake humu, kweli binadamu tuna mapungufu lakini hii haituzii kutekeleza kazi zetu kwa ufanisi, nchi nyingi Afrika zimeathirika sana ukabila na udini kutokana na waandishi wa habari kutokuwa makini kwenye kazi zao, mfano wa karibu ni majirani zetu Uganda, Rwanda na Burundi. Nakushauri siku nyingine ukikosea toa samahani tu inatosha, hapa umejaribu kutetea hoja binadamu tunakosea hilo ni sawa kabisa kosa kubwa la ujumbe huu ni kutumia dini umemtumia mtume Muhammad S.AW . Dini na siasa haviendi pamoja vinginevyo dunia hii ingekuwa amani tupu. Wanasiasa wanazo imani za kidini lakini hawatumii dini kutekeleza majukumu yao ya kisiasa.
 
Kiranga,
Ahsante sana kwa ushauri. Hilo la Karimjee nalifahamu, nilighafirika kutokana na haraka. Na sina maana huwa sifanyi makosa. Nayafanya mengi, na ni nani asiyefanya makosa?

Hapa kuna simulizi; ( Wanazuoni wa Kiislamu mnikosoe kama nimekosea mahali).

Kuna kisa pale Mtume Muhammad S.A.W aliposwalisha swala ya isha ( Salat al- 'Isha) pale Medina. Swala ya Isha ni swala ya usiku. Kwa kawaida ya swala ya isha ina rakaa nne. Usiku huo Mtume Muhammad S. A. W alipitiliza, akaswalisha rakaa tano. Mtume alipomaliza, muumini mmoja akajenga ujasiri, akamwuliza; " Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu, jambo la ajabu leo umeswalisha rakaa tano badala ya nne. Labda umepokea maagizo mapya kutoka kwa Mwenyezi Mungu".

Mtume akaonekana kushangaa, naye akawauliza waumini wengine. " Je, leo nimeswalisha salat al-Isha kwa rakaa tano?"

"Naam, Mtume wa Mwenyezi Mungu". Mtume alijibiwa na waumini.

Mtume Muhammad S. A. W akatamka; " Ndugu Waislamu wenzangu, mie ni mwanadamu kama nyie. Mniwie radhi, nimeghafirika".

Naam. Hata Mtume wa Mungu alikiri mapungufu. Sembuse sie wanadamu.

Afanaaaaleik sasa Majjid ndiye mtume aliyeghafilika au vipi ? 🙂

Astaghafirullah, astaghafirullah !
 
Hapa ninawashangaa sana wanaosema kumjadili Maggid ni simple mind.Wanashindwa kuelewa kuwa status ya Maggid ni tofauti na wengi wetu humu maana yeye ni mwandishi na maandiko yake yana influence watu wengi wenye uelewa tofauti.Inaweza kuwa influence nzuri au mbaya vile vile kutegemea na inavyopokelewa na wanajamii.Kwa hiyo basi sioni kosa lolote hapa kumjadili Maggid kwa sababu kwa kutumia kalamu yake anaweza kuwafikia wananchi wengi kushinda mimi na wewe.Na kama inaonekana kuna chembechembe za makosa katika ujumbe wake basi ni vyema ujumbe ukamfikia ili aone watu wanamtazama vipi katika maandishi yake.Ikumbukwe kuwa hata waliomsulubisha Yesu Kristo hawakumchukia yeye kama Yesu bali walihofia ujumbe wake aliokuwa akiuhubiri,vivyo hivyo kwa ndugu yetu huyu inapoonekana ujumbe wake unaenda tofauti basi sioni ubaya wowote wa kujadili kile alichoandika.
 
Afanaaaaleik sasa Majjid ndiye mtume aliyeghafilika au vipi ? 🙂

Astaghafirullah, astaghafirullah !

Kiranga msamehe ndugu Maggid ameaghafilika lakini ujumbe wako ameupata, siku nyingine atakuwa makini zaidi, kama utaweza muombe tumpate Michuzi angalau kwa siku moja tu ! Kwani tunahaja kumuelemisha mchimvi huyu (michuzi)
 
Unanikumbusha mbali sana; nakuwa nawaona akina mama wanasukana nywele, mara jamaa anapita, wanaanza kumjadili, katika jadili hiyo, kuna negative na postive, lakini wanajadili mtu wanayemuona na kumfahamu!

forum kama hii yenye members zaidi ya elfu kumi, unapoadnika lines kama hizi bila any clue kwa msomaji, unajidharaulisha kuliko akina mama wanaosukana nywele!

next time ili wewe uonekane una akili na kutaka kumvuta mjengwa upande wako, andika au post alichoandika, read btn the lines na kosoa kwa hoja kila alichoandika, YOU will then simply qualify as greath thinker
ulicholeta hapa ni sawa na kusema unanilaumu kwa nini nimevaa shati la bluu wakati wewe umevaa nyeupe!!! you ant everyone to be like yoou!! probably many in this forum are like you!!! kutumia mabavu kushawishi watu, badala ya lugha ya mvuto na hoja isiyopingika!!!
Waberoya mzee vipi au mama vipi? Kiranga amefafanua vizuri sana dhana ya kuzungumza watu jinsi ilivyo. Hapa hakuna anayemzungumza Maggid kwa kimo, rangi, umri, kabila, mahusiano yake na mkewe. Tunajadili maandishi yake kwenye magazeti na picha anazotundika kwenye blog yake.

Lazima ukumbuke kwamba Maggid walaji wa uandishi wake ni sisi, sasa kuna kosa gani kumwambia Mpishi wetu kwamba siku hizi wali wake umejaa chuya?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom