Mazungumzo na Maggid Mjengwa: Kwaya ya Tanu ya Rajabu Matimbwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
MAZUNGUMZO YANGU NA MAGGID MJENGWA WASIFU WA JULIUS NYERERE: KWAYA YA TANU YA RAJAB MATIMBWA NA WENZAKE

Ukishughulishwa na maisha ya Mwalimu Nyerere peke yake ukawasahu wale aliokuwanao kuna hatari ya Nyerere kuonekana, ''Super Man,'' jitu la miraba minne anaeweza hata kuibeba treni akapaa nayo mbinguni.

Ikiwa hivi historia ya Nyerere inakosa ukweli na haivutii kusoma.

Nimeeleza makala iliyopita watu waliojumuika kuifanya mikutano ya TANU ipendeze na kuvutia watu na katika hayo kupata wanachama wapya kila uchao.

Rajab Matimbwa mwaka wa 1954 alikuwa kijana mdogo wa miaka 20 hivi katokea Chole, Uzaramo kaja Dar es Salaam kutafuta maisha.

Rajab akapata kazi ya kuuza mgahawa wa John Rupia uliokuwa pembeni ya Pugu Road na baada ya hapo akapata kazi nyingine ya kuuza maji New Street mkabala wa ofisi ya TANU.

TANU ilipoasisiwa Rajab na wenzake wanne, Abdallah, Juma, Binoga na Katumbwele wakaanzisha kwaya ya kwanza ya TANU wakikutana kwenye ofisi ya TANU uani kutunga nyimbo na kufanya mazoezi ya kuimba.

Said akatunga nyimbo ya kwanza iliyokuwa ikisema, '' Watanganyika njooni tuchanganyike tukisifie chama chetu cha TANU Mola akipenda tupate uhuru.''

Rajab akatunga, ''Sikia wana kuteseka nchi ni shida tupu yatukalia sisi Watanganyika tunateseka kutawaliwa ni fedheha.''

Hizi nyimbo zilipokuwa zikiimbwa pale Mnazi Mmoja kabla Nyerere hajapanda jukwaani zilikuwa zikiwajaza hamasa wananchi.

Miaka mingi ikapita Rajab Matimbwa mtu mzima, mzee karudi kijijini.

Siku moja akaja mjini Dar es Salaam na ikamjia hamu ya kupita ofisi ya CCM ajikumbushe historia yake lau kwa kuliangalia jengo lile lililokuwa ofisi ya TANU.

Alishangaa kukuta jengo jipya la fahari na nje ya jengo kakuta walinzi ambao kila fikae pale lazima awaone ikiwa anataka kuingia ndani ya jengo.

Fikra zilimrudisha miaka mingi nyuma alipokuwa mwanakwaya wa TANU na ofisi ya TANU ilikuwa wazi kwa kila mwananchi.

Muda wote nje ya ofisi ile palikuwa na watu wengi wao wazee na kanzu zao nadhifu wako pale wengine wanakuja kwa shida zao na wengine wanakuja pale kwa mazungumzo ya kawaida ya barza.

Huu ulikuwa wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Rajab kasimama pembeni anaangalia ile hali akitegemea labda ataweza kumuona mtu anemfahamu.

Hakuwepo.

Hakumuona mtu yeyote anaemjua. Aliondoka pale kichwa amekiinamisha kwa huzuni.

TANU yao ilikuwa imekwenda na watu wake.

PICHA:

Picha ya kwanza ni Ofisi ya TANU baada ile ya mwanzo kuvunjwa yenye kibao kinachosema hapa ndipo ilipoundwa TANU 1954 na ofisi zilizokuja kujengwa baadae.

Picha ya mwisho ni Mzee Rajab Athmani Matimbwa watu wa mwanzo kuingia TANU kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa mstari wa mbele.

TANU (CCM) OFFICE LUMUMBA MIAKA YA 2000.JPG
CCM JENGO JIPYA.jpg
RAJAB MATIMBWA.JPG
 
Nimeona kwenye page ya Mjengwa mazungumzo yenu. Hivi media zetu walishawai kukutafuta ili wapate kitu kwenye hilo ghala lililosheni Maarifa mengi? Naitaji siku moja nikutafute nami nipate mawili matatu kwaajili ya vijana wangu siku za usoni
 
Nimeona kwenye page ya Mjengwa mazungumzo yenu. Hivi media zetu walishawai kukutafuta ili wapate kitu kwenye hilo ghala lililosheni Maarifa mengi? Naitaji siku moja nikutafute nami nipate mawili matatu kwaajili ya vijana wangu siku za usoni

ukipata jibu uni-tag
 
kwa wenzetu majengo kama hayo huwa yanahifadhiwa kwa kumbukumbu za vizazi vijavyo na pia kutumika kama makumbusho na mambo ya utalii ccm walitakiwa wajenge jengo sehemu nyingine maana kama maeneo na viwanja wanavyo vya kutosha pale palitakiwa kuwepo na maktaba ambayo imesheheni historia ya TANU matokeo yake vijana waliopo kwa kutojua historia wanawanyanyasa watu waliotengeneza ajira zao kabla hata ya kufikiliwa kuzaliwa
 
Nimeona kwenye page ya Mjengwa mazungumzo yenu. Hivi media zetu walishawai kukutafuta ili wapate kitu kwenye hilo ghala lililosheni Maarifa mengi? Naitaji siku moja nikutafute nami nipate mawili matatu kwaajili ya vijana wangu siku za usoni
Alex...
Tutakutana siku moja.
 
Huyu Mzee ajfunze kitu kimoja kikubwa
''Tenda wem wende zako usingojee shukurani''
 
Back
Top Bottom