😎Hata mimi nikuwa na mashaka makubwa sana kuhusu uwepo wa huyu kiumbe anayeitwa shetani, kwa sababu kwa maelezo ya vitabu vyote vya dini ni kuwa huyu kiumbe alikua ni Malaika mkuu aliyekuwa ameumbwa na mungu kwa ajili ya malengo yake mwenyewe mpaka siku alipomuasi muumba wake ambaye ni Mungu kwa mujibu wa hizo hadithi za kwenye vitabu;
Naomba wajuzi wa haya mambo waje hapa kilingeni kujibu hoja, bila kuleta Jazba.
Maswali.😱
1 -Ni kwanini Mungu anaendelea kumvumilia huyo kiumbe anayeitwa shetani katika harakati za kuwaangamiza viumbe wengine walioumbwa na Mungu wanaoitwa binadamu?
2 -Mungu Muumba wa binadamu na Shetani atapata faida gani kuwachoma binadamu ambao kwa maelezo ya vitabu hivyo upeo wake wa kuelewa mambo ni mdogo kuliko wa shetani aliyekua Malaika wake Mkuu?
3 -Inamaana Mungu wakati anamuumba shetani hakujua kama angeweza kumuasi?
4 -Nilini shetani alibadilika na kuwa na mapembe na mkia kama taswira ya shetani inavyoonyeshwa na wanazuoni wa dini?
5-huko kwenye hivyo vitabu kuna hadithi ya Adamu na Hawa ama Eva, na kwa mujibu wa hadithi za humo ni kuwa baada ya kula tunda walipewa adhabu na moja ya viumbe vilivyopewa adhabu ni nyoka, Ni kwanini mungu ampe nyoka adhabu wakati aliingiliwa na shetani badala ya kumpa adhabu shetani?
6 -Je Mungu anakiogopa kiumbe chake alichokiumba (Shetani) hadi anashindwa kukichukulia hatua stahiki na badala yake amempa uhuru wa kuingilia viumbe dhaifu kama nyoka na binadamu.😎