Mosi, Mimi kama mwanaume napingana kwa 100% na nyumba ndogo kwani huo ni uzinifu na uzinifu wowote hauna matokeo mema hata kwa huyo mzinifu mwenyewe achilia mbali ndoa ya huyo mzinifu.
Pili, huenda Mshana jr hakuwa na nia mbaya kabisa na alikuwa na point kubwa sema uwasilishaji wake ndo haukuwa sawa.
Tatu, hakuna atakayepinga hata mmoja kwamba mwanamke na mwanaume ni viumbe wawili wanaofanana vyema kwa vitu vingi lakini pia wana tofauti chungu nzima, mpaka Yesu anarudi mwanamke na mwanaume hawawezi kuwa na usawa wa kila kitu, lazima watatofautiana kwenye baadhi ya mambo. Mfano kimaumbile mwanamke anapitia vipindi kadhaa ambavyo mumewe hapitii kama hedhi, uzazi, hivi ni vipindi ambavyo mwanamke inabidi akae bench asishiriki haki ya ndoa, walau hedhi si siku nyingi lakini uzazi unachukua siku nyingi.
Kwa wanaume pia wanatofautiana wenyewe kwa wenyewe kuna wanaoweza kukaa kipindi kirefu bila kushiriki tendo la ndoa na kuna wasioweza. Sasa hilo group la pili ndo hupata shida sana kwenye dharura ya kimaumbile ya mwanamke.
Lakini pia kwa takwimu sahihi ni dhahiri kabisa idadi ya wanawake ni kubwa zaidi ya wanaume (hapo kwenye idadi ya wanaume watoe wasio na nguvu za kiume, wazee na wanaoshiriki ushoga), hivyo inapelekea imbalance kwenye suala la mahusiano, wengi hawaoni hilo kwa kuwa huwa hawafanyi research lakini pia wengi ni wabinafsi.
Hitimisho: busara au suluhisho ya changamoto hizo si nyumba ndogo bali ni mwanaume kuongeza mke wa halali lakini katika misingi sahihi itakayohakikisha hadidimizi haki zozote za mke mkubwa, yaani awe muadilifu na kama hauwezi uadilifu basi ajitahidi kuvumilia japo kimaumbile huwa ni kutwanga maji
Sent using
Jamii Forums mobile app