Nakukumbusha tu: Nyumba ndogo haziolewi

Nakukumbusha tu: Nyumba ndogo haziolewi

Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*

*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*

*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.*

```Ujumbe huu mzuri umfikie kila mmoja wetu katika familia yake.

Jr[emoji769]

Jr[emoji769]

Ili msamaha uweze kukubalika na kuleta matokeo chanya ni lazima uwe na mambo yafuatayo:
1. Mkosaji aoneshe kujutia makosa yake alofanya
2. Mkosaji asitafute kujitetea wakati wa kutubu
3. Mkosaji aoneshe kutorudia makosa (hususa yaleyale) mageuko!

Sasa pale ambapo mke anamsamehe mume leo baada ya muda mfupi mume anarudia kuchepuka hapo msamaha utafanya kazi kweli?
Halafu wanaume wengine kuchepuka ni mfumo Wao wa maisha yani anazani hawezi ishi bila mchepuko!
Kumsamehe mtu ambae kila mara unamkuta na kosa hilo hilo tuseme ukweli ni ngumu!
Ingekuwa ukishamsamehe mara moja anaacha makosa ingependeza!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafanya kazi kweli au nayo inahitaji imani Kama maombi?
😂😂😂hv na ww unaamini kwenye hayo madude ya chumvi😂😂si shirki hyo.jaman😂😂😂 lbd km ushawah enda kwa mganba utaona kawaida..khaaa
 
Kuchepuka/ Nyumba ndogo zina athari ktk maeneo yafuatayo:
1. Kiimani - ni dhambi
2. Kimaadili - haipendezi
3. Kiafya - ni hatari kiafya (magonjwa) hata kifo na watoto kubaki yatima na mahangaiko!
4. Kiuchumi - rasilimali za familia ikiwemo fedha na muda kutumika kusiko shahili!
5. Impairment of marriage love kwa mwenza wa ndoa
6. N.k


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukulia mke na mume wote wanafanya kazi,
Hela ya mke ifanye mambo ya maendeleo lakini ya mume ndo iende kutunza michepuko!
Je hiyo ni haki?
Ndo maana wanawake wengine huchukua tahadhari kabla ya hatari kwa kujifanyia mambo yake kimya kimya
ikibidi unamwambia kabisa najenga na nanunua mashamba kwa jina langu sababu integrity yako kwenye ndoa iko mashakani!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ili mtu asamehewe kuna vigezo!
1.Mkosaji aoneshe kujutia kosa
2. Mkosaji asitafute kujitetea
3. Mkosaji aazimie kutorudia kosa

Sasa mtu mfano anasamehewa leo kesho anachepuka tena je utaendelea kumsamehe?!
Yani kuna watu kuchepuka ni sehemu ya mfumo wa maisha!

Cc: Mshana Jr et al


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tungekua na utamaduni wa kufanya utafiti mara kwa mara mimi nazani kiwango cha talaka huenda kitakuwa kimeongezeka kwenye takwimu!
Haiwezekani eti ifike mahali mwanamke kuolewa awe ameji risk maisha yake
Nazani haipaswi ifike huko!
Wadada wengi wameamua kuachika wanalea watoto wao wenyewe wameacha waume zao wafanye umalaya!
Halafu wanaume wa hivyo hutia huruma sana!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ili mtu asamehewe kuna vigezo!
1.Mkosaji aoneshe kujutia kosa
2. Mkosaji asitafute kujitetea
3. Mkosaji aazimie kutorudia kosa

Sasa mtu mfano anasamehewa leo kesho anachepuka tena je utaendelea kumsamehe?!
Yani kuna watu kuchepuka ni sehemu ya mfumo wa maisha!

Cc: Mshana Jr et al


Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanaume yoyote kamili, mwenye afya njema/ both akili na mwili , uchumi wa kati/kawaida.....

Kuchepuka ni lazima (hakuepukiki)

Labda umroge [emoji116] [emoji116] [emoji116]
IMG-20190123-WA0069.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti unasema nini wewe Mshana!? Nyumba ndogo ni msingi imara wa ndoa nyingi!? Acha kupotosha wanaume wenzio hivi hiyo michepuko ni misingi au mipasuko!? Hiyo ndio chanzo cha migogoro isiyokwisha kwenye familia nyingi maana moyo ni mmoja hauna nguvu ya kupenda kuwili sawa sawia, wanaume wengi mkishakua na nyumba ndogo dharau kwa wake zenu huzidi Mara dufu. Ogopeni magonjwa hivi huwa mnajiulizaga kipindi unalala kwa mkeo yule hawala yako huwa analala na nani? Sasa hivi kuna gonjwa lisilokingwa na kinga ya condom mnatuletea homa za Ini ndani ya nyumba,tulieni wapuuz nyie

Sent using Jamii Forums mobile app

Nyumba ndogo ni msingi wa Ndoa bora, nakubaliana na Mshana 100% si mda na mie nitaitafuta, sijawahi kuwa nayo, huyu MWANAMKE mshenzy, hafanyi majukumu yake, KABISA NA WAZEE WANASEMA SIWEZI OA MPAKA KIFO, HAPA NI NYUMBA NDOGO TU ITANISAIDIA!
 
Imeandikwa ikimbieni zinaa!
Lakini wanaume wengi siku hizi wanaikimbilia zinaa!
Ni kweli wanawake wengine wanawatega wanaume wa watu kwa kuvaa mavazi ya uchi, kujicjekeshakesha na kuwaomba hela wanaume za watu n.k
Lakini wanaume mwerevu anaejielewa huwadharau wanawake wa hivyo na kuona kuwa ni Vya wote[emoji108][emoji108]
Kwa nini ukubali kuingia kwenye mtego?
Kwa nini ukubali kunaswa?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂hv na ww unaamini kwenye hayo madude ya chumvi😂😂si shirki hyo.jaman😂😂😂 lbd km ushawah enda kwa mganba utaona kawaida..khaaa
Sijawahi enda, kwani chumvi ni ushirikina? Hata baadhi ya makanisa wanaagiza tupeleke chumvi ikaombewe 😄
 
Halafu wanasema mume wa mtu ndo Mzuri sana kuliko single man!
Wanasema mume wa mtu Hanaga hiyana katika kuhonga!
Mume wa mtu hagandi mwanamke maana ana commitments nyingi zikiwemo za kazi na za kifamilia!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ewe mwanaume uliyeoa umtende mkeo kwa mambo ya hiyana!
Mwaka mpya huu nakisihi mkaribie Mungu wako kwa kwenda Nyumba za Sala na kuuashika mafundisho yake!
Neno la Mungu lina nguvu kubwa !
Kuishi na mke wa ujana wako bila kuchepuka inawesekana!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom