Nakubaliana na Rais Mwinyi kwamba Manaibu Waziri wanaongeza gharama za Serikali naamini Rais Magufuli atafanya hivyo pia!

Kiukweli sehemu moja muhimu ya kupunguza matumizi ya Serikali ni kuwaondoa manaibu waziri kwani zaidi ya kujibu maswali bungeni huwa sioni kazi nyingine ya maana wanayofanya.

Katika hili nakubaliana kabisa na Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi la kutoteua manaibu Waziri katika baraza lake.

Ni imani yangu utaratibu huu una baraka za chama na hata Rais Magufuli atafanya vivyo hivyo.

Maendeleo hayana vyama!
Sasa wewe kijisehemu kama Zanzibar ambapo ukipiga filimbi wote wanasikia manaibu waziri wanini?

Hata hao mawaziri ni mzigo tu kwa kamkoa ka Zanzibar
 
Hivi ukubwa Zanzibar yote yaani Unguja na Pemba ni sawa na ukubwa wa mji gani ulioko Tanzania bara?
 
Hata bara naibu waziri wa nini?
Bara kuna raia zaidi ya 60M, hii nchi ni kubwa na changamoto ni nyingi sana.

Kazi ya Naibu waziri ni kushiriki katika utungaji wa sera na kusimamia utekelezaji wake siku kwa siku. Sasa fikiria nchi hii ilivy9 kubwa na changamoto zake waziri wa maji akae bungeni kujibu hoja na hapohapo awepo field kutatua changamoto.

Kwa bara hao watu hawakwepeki kwa Zanzibar hata kuwa na mawaziri 6 ni mzigo na gharama zisizo na lazima
 
Kiukweli sehemu moja muhimu ya kupunguza matumizi ya Serikali ni kuwaondoa manaibu waziri kwani zaidi ya kujibu maswali bungeni huwa sioni kazi nyingine ya maana wanayofanya.

Katika hili nakubaliana kabisa na Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi la kutoteua manaibu Waziri katika baraza lake.

Ni imani yangu utaratibu huu una baraka za chama na hata Rais Magufuli atafanya vivyo hivyo.

Maendeleo hayana vyama!
Napingana na wewe. Manaibu waziri ni muhimu hasa pale majukumu ya wizara ni makubwa sana. Mfano Wizara ya Fedha kuna upande wa kusimamia makusanyo na kuna kusimamia matumizi (budget), kichwa cha waziri mmoja hakiwezi kubeba yote hayo na kuwa msemaji wake.
 
Zanzibar ni ndogo sana mkuu hamna haja ya manaibu ila kwa mainland inakuwa ngumu kidgo Tanganyika ina eneo kubwa manaibu muhimu.
Unaovyoongea kwa huruma utafikiri ushafanya kazi ya uwaziri
 
hata hao mawaziri wawili aliowateuwa kabla ya kumteuwa waziri mkuu wanatosha kabisa.
By the way nchi haina hela na wahisani hawatatoa hela.

"hii sio awamu ya kula raha, mimi mwenyewe mke wangu hanipi raha"
 
Bara kuna raia zaidi ya 60M, hii nchi ni kubwa na changamoto ni nyingi sana.

Kazi ya Naibu waziri ni kushiriki katika utungaji wa sera na kusimamia utekelezaji wake siku kwa siku. Sasa fikiria nchi hii ilivy9 kubwa na changamoto zake waziri wa maji akae bungeni kujibu hoja na hapohapo awepo field kutatua changamoto.

Kwa bara hao watu hawakwepeki kwa Zanzibar hata kuwa na mawaziri 6 ni mzigo na gharama zisizo na lazima
Kazi zote anazofanya naibu waziri zinafanywa pia na DED chini ya waziri wa Tamisemi.

Naibu waziri hana kazi yoyote zaidi ya kujibu maswali ya " nyongeza" bungeni!
 
Bendera kufuata upepo saa hizi unapongeza akija akitengua kauli yake pia utapongeza..
 
Kazi zote anazofanya naibu waziri zinafanywa pia na DED chini ya waziri wa Tamisemi.

Naibu waziri hana kazi yoyote zaidi ya kujibu maswali ya " nyongeza" bungeni!
Hivi unakijua unachokijadili lakini? Unayajua majukumu ya DED? Unaijua job description ya DED na Waziri?

Unajua tofauti ya mtumishi na kiongozi wa kisiasa?

Kazi ya Waziri au Naibu waziri kwa nature ya Job descriptions zao kamwe haziwezi fanywa na DED au katibu mkuu. Unless hujui hawa watu majukumu yao kikatiba na kisheria ni yapi.
 
Napingana na wewe. Manaibu waziri ni muhimu hasa pale majukumu ya wizara ni makubwa sana. Mfano Wizara ya Fedha kuna upande wa kusimamia makusanyo na kuna kusimamia matumizi (budget), kichwa cha waziri mmoja hakiwezi kubeba yote hayo na kuwa msemaji wake.
Kusimamia matumizi na mapato ni jukumu la katibu mkuu wa wizara.
 
Hivi unakijua unachokijadili lakini? Unayajua majukumu ya DED? Unaijua job description ya DED na Waziri?

Unajua tofauti ya mtumishi na kiongozi wa kisiasa?

Kazi ya Waziri au Naibu waziri kwa nature ya Job descriptions zao kamwe haziwezi fanywa na DED au katibu mkuu. Unless hujui hawa watu majukumu yao kikatiba na kisheria ni yapi.
Kwanza tofautisha Waziri na Naibu waziri.

Naibu waziri siyo waziri lazima uelewe hilo

Naibu waziri ni karani tu bwashee!
 
Kiukweli sehemu moja muhimu ya kupunguza matumizi ya Serikali ni kuwaondoa manaibu waziri kwani zaidi ya kujibu maswali bungeni huwa sioni kazi nyingine ya maana wanayofanya.

Katika hili nakubaliana kabisa na Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi la kutoteua manaibu Waziri katika baraza lake.

Ni imani yangu utaratibu huu una baraka za chama na hata Rais Magufuli atafanya vivyo hivyo.

Maendeleo hayana vyama!
Hili ni jambo la msingi sana, mawaziri na makatibu wakuu wanatosha.
 
hata hao mawaziri wawili aliowateuwa kabla ya kumteuwa waziri mkuu wanatosha kabisa.
By the way nchi haina hela na wahisani hawatatoa hela.

"hii sio awamu ya kula raha, mimi mwenyewe mke wangu hanipi raha"
Wahisani watatoa fedha kama kawaida bwashee.

Siasa ni sayansi!
 
Kwanza tofautisha Waziri na Naibu waziri.

Naibu waziri siyo waziri lazima uelewe hilo

Naibu waziri ni karani tu bwashee!
Waziri na Naibu waziri wote na watunga sera na wasimamizi wa sera katika wizara walizokabidhiwa.

Waziri na Naibu waziri wao ni wasimamizi, watungaji wa sera ambazo watekelezaji wake ni hao Makatibu wakuu Ma DED n.k

Naibu waziri sio karani. Anaweza kutekeleza majukumu yote ya Waziri kama atakavyoelekezwa na Rais au Waziri mkuu.

Tofauti ya Waziri na Naibu waziri ni kwamba Naibu waziri sio mjumbe wa baraza la mawaziri.

Kwa maneno mengine ni msaidizi wa Kisera kwa waziri na ni serikali.

Serikali ni Rais, Makamu wa Rais, waziri mkuu mawaziri na manaibu wao.

NB: hii ni quote ya mwisho kwako maana umeonesha utoto wa hali ya juu. Nimesikitika mno kupoteza muda wangu.
 
Zanzibar ni mikoa miwili tu, bahati yao inaitwa nchi, sioni umuhimu wa manaibu Waziri hata Mawaziri wanatakiwa wawe saba tu.
Dharau za watu kama wewe ndizo zinazofanya wazanzibari wawachukie watanganyika. Zanzibar ni nchi na itabaki kuwa nchi na ndio maana Tanzania inaitwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania - United republic of Tanzania, nataraji unajua maana ya neno UNITED na pia kuwa ulifunzwa na walimu wako kuwa neno tanzania ni linatokana na TANganyika na ZANzibar na ia ndio common letters kwenye majina ya nchi zote mbili. Ukubwa na udogo wa nchi yetu zanzibar huumaanishi kitu, Tanzania ni muungano wa nchi mbili ukitaka usitake.
 
Waziri na Naibu waziri wote na watunga sera na wasimamizi wa sera katika wizara walizokabidhiwa.

Waziri na Naibu waziri wao ni wasimamizi, watungaji wa sera ambazo watekelezaji wake ni hao Makatibu wakuu Ma DED n.k

Naibu waziri sio karani. Anaweza kutekeleza majukumu yote ya Waziri kama atakavyoelekezwa na Rais au Waziri mkuu.

Tofauti ya Waziri na Naibu waziri ni kwamba Naibu waziri sio mjumbe wa baraza la mawaziri.

Kwa maneno mengine ni msaidizi wa Kisera kwa waziri na ni serikali.

Serikali ni Rais, Makamu wa Rais, waziri mkuu mawaziri na manaibu wao.

NB: hii ni quote ya mwisho kwako maana umeonesha utoto wa hali ya juu. Nimesikitika mno kupoteza muda wangu.
Unajua kwanini bungeni naibu waziri hujibu maswali kwa niaba ya waziri?

Na akizidiwa husaidiwa na Waziri kamili yoyote lakini si yeye kufunga mjadala?

Usiishi kwa kukariri bwashee!
 
Back
Top Bottom