Waziri Mhagama Ampa Big Up Rais Mwinyi Ujenzi wa Skuli za Ghorofa Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,842
927

WAZIRI MHAGAMA AMPA BIG UP RAIS MWINYI UJENZI WA SKULI ZA GHOROFA ZANZIBAR

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Sera na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya nane ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuboresha mazingira ya elimu yanayoendana na adhma ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Waziri Mhagama ameeleza hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa skuli ya msingi ya Mwera ikiwa ni shamrashamra za kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mhagama amesema serikali inajidhatiti kuboresha mazingira ya elimu ikiwa ni pamoja na juhudi za kujenga madarasa na skuli za kisasa za ghorofa ambazo zinajengwa unguja na pemba 25 katika bajeti ya mwaka 2023/2024.

Akitoa taarifa ya kitaalamu Naibu Katibu Mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Mwanakhamis Ameir amesema ujenzi huo wa gorafa mbili ulianza mwezi Mei 2023 na kutarajiwa kukamilika mapema mwaka huu ambao umegharimu bilioni 4 na milioni mia tano na kuwepo kwa madarasa 29 pamoja na kumbi za mitihani, maabara na vyumba vya Tehama

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa eneo hilo Mbunge wa Jimbo la Uzini ambae pia ni Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Chilo ameipongeza serikali kwa hatua kubwa za maendeleo walizozifikisha katika jimbo hilo huku akisema ujenzi wa skuli hiyo unaenda kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika darasa.

jenista-pc-data.jpg
 
Wacha upande wa pili waendelee kujenga maghala. Maana ardhi bado ipo.
Huku bado tunaupiga mwingi!
 
Back
Top Bottom