MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
- Thread starter
- #21
Umeongea vizuri sana mkongwe. Ila umesahau jambo moja. Shida kwenye nchi yetu ilianza pale Nyerere alipokataa mawazo ya watu waliokuwa wanaona mbele kuliko yeye hasa Kambona.
Kwa jinsi Nyerere alivyomfanyia Kambona ndo laana ya hii nchi ilipoanzia. Kama hatujatubu ile dhambi, maendeleo ya kweli tuyasahau milele.
Kambona alipinga sana siasa za kukieneza zaidi Chama cha Mapindizi kuliko Serikali na huduma zake. Wakamuona mzandiki hafai, Kambona alipinga nchi kujiingiza kwenye siasa za ujamaa wakamuona chizi wakamfanya hadi akimbie nchi.
Ukitizama kwa makini mambo aliyopinga Kambona hadi kukorofishana na Nyerere ndo msingi na chanzo kikuu cha matatizo yanayotukabili hii leo.
Nakubaliana kabisa na wewe kabisa, mchango wa Oscar Kambona kwa hili taifa ni mkubwa mno, tena mkubwa sana. Nadhani hakustahili kufanyiwa vile na kina Mzee Nyerere. Nadhani njia sahihi ilikuwa kumuweka pembeni kuliko kumchafua vile mtu aluetoa mchango mkubwa kwa taifa:
- Kambona alivyoingia TANU ndani ya mwaka mmoja alikusanya wanachama 10000.
- Ndiye aliyeunda mifumo ya usalama hapa nchini akishauri kwamba vijana wa TYL ndiyo waingizwe kwenye idara mpya ya usalama wa taifa. Yeye ndiye aliyeenda kwa waisraeli ili watoe mafunzo kwa watanzania.
- Ndiye aliyezima uasi wa kijeshi wa KAR mwaka 1964 wakati Mzee Nyerere na Rashidi Kawawa wakiwa wamefichwa. Angekuwa ni mtu mbaya basi baadhi ya wanajeshi walipomwambia ajitangaze kuwa Raisi alikataa mzee wa watu.
- Kambona ndiye ARCHITECH wa FOREIGN POLICY ya Tanzania, alichokuwa anakizungumza Kambona miaka ya 60's mwanzoni ndicho ambacho Mzee Nyerere alikuwa akikizungumza miaka yote ya utawala wake.
Kambona was forced into the Dark-Side. Mambo mabaya aliyofanyiwa ndiyo yalipelekea Kambona aje kuwa na moyo mgumu vile. Mzee Nyerere alimwogopa Kambona hadi mwisho kwasababu yeye ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanamfahamu Nyerere kiundani (Hulka na Madhaifu yake), jambo ambalo Nyerere hakulipenda ukizingatia alishajitengenezea A CULT OF PERSONALITY.