Hmaster
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 346
- 86
Mimi ni bonge la handsome na ki ukweli nakubalika kirahisi sana kwa wanawake ingawa si mtu wa kujali sana masuala ya mapenzi kwa vile ninajua madhala ya kuendekeza sana. Hata hivyo nina tatizo moja kubwa nalo ni kuachia mapema hata kwa mtu niliyempenda sana mwanzoni. Hapa namaanisha kwamba ingawa si mtu wa kubadilisha wanawake mara kwa mara lakini kwa yule atakayebahatika kukutana na mimi basi huwa tuna muda mfupi tu kabla sijamwacha. Huwa inakuwa ngumu sana kumwacha mwanamke ambaye hajakukosea jambo lakini huwa najitahidi hadi naweza na yeye kubaki kunitazama tu. Kwa kuwa sipendi hali hii hebu wadau mnipe ushauri ni vipi nidumu na demu mmoja. Nawasilisha.