Kwanini wanawake wanaamini wanaume tunakufa mapema

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Ndugu zangu ikiwa ni siku nyingine iliyo zungukwa na hali ya hewa nzuri pamoja na haya maua tuliyoumbiwa huku duniani nawatakia siku njema na majukumu mema

Ndugu kama kichwa cha somo kinavyo ainisha katika jamii zetu hawa wanawake wetu tunao wapenda na kuhangaika nao sana wanaamini kabisa pasi na mashaka yeyote kwamba mwanaume ndiye anayetangulia kufa siku zote hivyo atabaki mwenyewe na siyo vinginevyo,

pia tunavyoenda kwenye majukumu yetu wakati mwingine wanaamini tutafia huko na inawezekana kutorudi nyumbani , jambo linalowafanya wakati mwingine tunapo aga wake zetu kwenda kwenye majukumu ya kutafuta ugali wanatuangalia mara mbili mbili kwa mashaka sana

Ndugu zangu jambo hili huwafanya wanawake kuweka tamaa sana ya mali kuliko utu kwa lengo la kujitajirisha binafsi yake na kujihudumia ikitokea mwanaume umekufa na kumwacha peke.

Je, ni kwanini basi wanawake wetu hawa wazuri , mawaridi ya mioyo yetu na inayotupa utelezi murua pamoja na burudani hasa hasa wakati huu wa mvua na baridi za hapa na pale wanaamini sisi wanaume wao ndiyo tunakufa mapema kuliko wao.?

Nakaribisha maoni yenu
 
Through experience.Mf, mimi nimesoma chuo fulani miaka 20 iliyopita.Nilipomaliza chuo nilifanya kazi maeneo yale yale karibu na hicho chuo.Tangu mwaka huo walimu wa kiume waliotufundisha wameishakufa zaidi ya walimu 10 na wakike 2 tu.
 
Je, nini chanzo cha vifo vyao?
 
Sababu ni nyingi mno. Ila chache ni kuwa tunamichezo hatarishi, umalaya, maisha magumu, mishe nyingi hatutulii nyumbani, hatusali, kukimbiza magari nk
 
Ndugu zangu ikiwa ni siku nyingine iliyo zungukwa na hali ya hewa nzuri pamoja na haya maua tuliyoumbiwa huku duniani nawatakia siku njema na majukumu mema

Ndugu kama kichwa cha somo kinavyo ainisha katika jamii zetu hawa wanawake wetu tunao wapenda na kuhangaika nao sana wanaamini kabisa pasi na mashaka yeyote kwamba mwanaume ndiye anayetangulia kufa siku zote hivyo atabaki mwenyewe na siyo vinginevyo,

pia tunavyoenda kwenye majukumu yetu wakati mwingine wanaamini tutafia huko na inawezekana kutorudi nyumbani , jambo linalowafanya wakati mwingine tunapo aga wake zetu kwenda kwenye majukumu ya kutafuta ugali wanatuangalia mara mbili mbili kwa mashaka sana

Ndugu zangu jambo hili huwafanya wanawake kuweka tamaa sana ya mali kuliko utu kwa lengo la kujitajirisha binafsi yake na kujihudumia ikitokea mwanaume umekufa na kumwacha peke.

Je, ni kwanini basi wanawake wetu hawa wazuri , mawaridi ya mioyo yetu na inayotupa utelezi murua pamoja na burudani hasa hasa wakati huu wa mvua na baridi za hapa na pale wanaamini sisi wanaume wao ndiyo tunakufa mapema kuliko wao.?

Nakaribisha maoni yenu
kwasababu mwanaume likimkaa kooni, moyoni au akilini haliachi wala kulitoa akapata nafuu, hung"ang"ana nalo kibabe na polepole humtafuna na kumlemea na hatimae humchosha na mwishowe hufa na kijiba cha roho, lakini mwanamke aanweza liachia, akasemehe na kusahau, akasonga mbele na maisha yakasonga....
 
Back
Top Bottom