Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Tuko vizuri mkuu!
tapatalk_jpeg_1544296142852.jpeg
 
Nini wanachokula sasa hivi ambacho walikuwa hawakili zamani?
Kwa hiyo hata haya ya Makampuni kupunguza Wafanyakazi, Makampuni na Biashara mbalimbali kufungwa, Benki Kufilisika, Fremu kukosa Wapangaji, etc ni maswala ya mitandaoni tu eee??
 
Hayo ni masuala ya kawaida kabisa katika uchumi wa kibepari.

Wewe hujawahi huko nyuma kusikia watu wameachishwa kazi?

Hujawahi kusikia benki kufilisika?

Hakuna lililo la ajabu hapo.
 
Yalikuwepo ndio,
But not this extent.
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍
 
Wananchi wangepewa uhuru wa kusema kinachoendelea ungejua tulipo na hali tuliyonayo, actually huku uraiani ukisema maisha magumu hata mgambo tu anakutia ndani, au usishangae ukatoweka mtaani/duniani., KILICHOPO NI KUWA Wanaosema maisha ni mepesi ni wale waliowazunguka waheshimiwa, na wanaosema maisha ni magumu ni wale wanaowazunguka wananchi, PROOF; BEI ZA MAZAO ZIPO CHINI ilhali mbolea ipo juu... BEI ZA BIDHAA ZIMEPANDA Km vifaa vyote vya ujenzi, vifaa vya nyumbani, n.k.... AJIRA IMEKUWA SHIDA Kuanzia za serikali kuu na mtaani, (utawala huu unaongoza kwa kuharibu ajira na sio kutengeneza).... VIWANDA VYA MDOMO. Kiuhalisia hakuna viwanda, mkoa mzima una kiwanda kimoja lakini ripoti ya mkuu wa mkoa anasema viwanda 2000, ipo hv, viwanda vingekuwepo hata kelele ya ajira isingekuwepo.. WATAWALA HAWAYASEMI HAYA WAO WANATAJA ndege, flyover, kufunga wapinzani na nidhamu kazini kwamba ndo maendeleo... (natabiri tu? KM KULIA HALI NGUMU NI KUKOSA HELA ZA MADEAL MWAKA 2020 1/4 YA WATANZANIA WATASOMEKA WAPIGA MADEAL
 
Nyani Ngabu uko sahihi kabisa,hizi ni njama za mabeberu na makuadi wao kujaribu ku-discredit na kumkatisha tamaa JPM.Sisi jukumu letu liwe kumtia moyo,by telling him that he is in the right track and that he should move forward.Makuadi wa mabeberu watapiga kelele,lakini wanapopiga kelele,na infact kelele zao zinapozidi we should know that our strategies are biting hard, na huo uwe ndio wakati wetu wa kukaza kamba.
 
Hali ngumu mzee lakini sijui kwa wewe uko basi tupe ata kadili kidogo
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Mkuu,rafikï yako musiba hajambo? Yale mafungu bado mnapewa?
 
Mleta mada uu mzima kweli? ndio utafiti ulioufanya? nakushauri nenda kijiji ulichozaliwa acha kuaminisha watu ugoro.
 
Maisha ni mazuri sana tanzania..watu wanakula na kusaza..ajira ziko bwerere....biashara zinashamiri....viwanda vinafunguliwa...bei za vyakula ziko chini sanaaa kuliko wakati wowote....hospitali zimetapakaa kila mahali...yaani ni full raha full kipupwe
 
Back
Top Bottom