Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Ukweli hali ni mbaya! Usitake tuongee saba,bado tunahitajika kwenye familia zetu!
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Mke wa mtu ktk ubora wako,mwanaume aliyekamilika hawezi kuandika uharo wako,can't you see the difference?
 
Mantiki ya hichi unachokisema mkuu...nimeshindwa kuona data za kiutafiti kupitia andiko lako.
 
Umeniangusha sana.....hivi unajua Hata Bei ya Kilo ya sukari? Unajua ni ajira ngapi (rasmi) zimetolewa tangu 2016? Je, unajua ni kiwango gani cha makato kinawakumba watumishi hadi kupelekea mshahara kiduchu? Usione watu wanakula na kunywa zingine ni Mbwembwe za mikopo na Vicoba...bila shaka huishi Tz na kama upo hapahapa basi unaishi huko Kwa wenye nazo..karibu kwetu mkuu sio mbali saana na -Lumumba street.
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Kwa kweli, nyani umekuwa nyani halisi. Nenda Burundi ambako machafuko ni sehemu ya maisha yao. Yale uliyoyabainisha kufanywa hapa Tz, yapo tu japo kuna machafuko. Syria hali kukubalika. Kitu ninachokiona kutoka kwako ni kuwa "Wewe hufanyi kazi za watanzania walio wengi. Unapata fedha za bure kutoka sehemu fulani", sasa unafanya katathmini uchwara, ku-justify uzuzu, majivuno na kiburi unachopewa na vifedha hivyo vya bure. Watu kama wewe tunao wengi, Kwa kuwa ninasema ujinga kuusadikisha ulimwengu kuwa nchi yenu iko sawa. Njoo huku ninakoishi nikuoneshe familia ambazo zinakosa hata mlo wa siku moja. Watoto wanalala njaa siku mbili wakisubiria mama wafanye kibarua cha kulima apewe shilingi 1500/=. Njoo uone tunavyouza muhogo Kwa shilingi. 100/= Kwa kilo ili uweze kuilipa watoto wetu walionyimwa mikopo ya elimu ya juu. Njoo tukuoneshe tunavyoishi Kwa matumaini ya kufikiria kesho itakuwa ahueni, baada ya kulima na mazao yetu yanaozea ndani. Njoo we nyani tukuoneshe hali mbaya. Remember the French Revolution!

Sent from my HUAWEI GRA-L09 using JamiiForums mobile app
 
Umeniangusha sana.....hivi unajua Hata Bei ya Kilo ya sukari? Unajua ni ajira ngapi (rasmi) zimetolewa tangu 2016? Je, unajua ni kiwango gani cha makato kinawakumba watumishi hadi kupelekea mshahara kiduchu? Usione watu wanakula na kunywa zingine ni Mbwembwe za mikopo na Vicoba...bila shaka huishi Tz na kama upo hapahapa basi unaishi huko Kwa wenye nazo..karibu kwetu mkuu sio mbali saana na -Lumumba street.

Hivi nyie watu mnaposikia neno ajira mnakuwa mnawaza mwajiri ni serikali tu?
 
Kwa kweli, nyani umekuwa nyani halisi. Nenda Burundi ambako machafuko ni sehemu ya maisha yao. Yale uliyoyabainisha kufanywa hapa Tz, yapo tu japo kuna machafuko. Syria hali kukubalika. Kitu ninachokiona kutoka kwako ni kuwa "Wewe hufanyi kazi za watanzania walio wengi. Unapata fedha za bure kutoka sehemu fulani", sasa unafanya katathmini uchwara, ku-justify uzuzu, majivuno na kiburi unachopewa na vifedha hivyo vya bure. Watu kama wewe tunao wengi, Kwa kuwa ninasema ujinga kuusadikisha ulimwengu kuwa nchi yenu iko sawa. Njoo huku ninakoishi nikuoneshe familia ambazo zinakosa hata mlo wa siku moja. Watoto wanalala njaa siku mbili wakisubiria mama wafanye kibarua cha kulima apewe shilingi 1500/=. Njoo uone tunavyouza muhogo Kwa shilingi. 100/= Kwa kilo ili uweze kuilipa watoto wetu walionyimwa mikopo ya elimu ya juu. Njoo tukuoneshe tunavyoishi Kwa matumaini ya kufikiria kesho itakuwa ahueni, baada ya kulima na mazao yetu yanaozea ndani. Njoo we nyani tukuoneshe hali mbaya. Remember the French Revolution!

Sent from my HUAWEI GRA-L09 using JamiiForums mobile app

Go to hell.
 
Hayo ni masuala ya kawaida kabisa katika uchumi wa kibepari.

Wewe hujawahi huko nyuma kusikia watu wameachishwa kazi?

Hujawahi kusikia benki kufilisika?

Hakuna lililo la ajabu hapo.
Tatizo si kuachishwa kazi.. bali idadi ya kuachishwa kazi. Kwasasa ni.kubwa kuliko hapo nyuma.
 
Hivi nyie watu mnaposikia neno ajira mnakuwa mnawaza mwajiri ni serikali tu?
kama mwajiri si serikali je, wewe umeshatoa ajira ngapi mpaka sasa? Kama jukumu si la serikali ktk kupunguza tatizo la ajira, Labda unadhani ajira zitatoka wapi kwa "Poor private sector" yetu kiasi hichi? Hebu amka acha kulala fofofo!!
 
kaka zaman bata zilikua kama zote bwana... watu wanapak magari yao wanapanda daladala unsema hali sio mbaya..watu kila jumamos walikua wanaenda minada ya nyama lakin sasa hv waulize hao masai anaishia kuuza mbuzi 20 out of 100@day?aka sitak kukubaliana na hoja yako[emoji26]
walokua wanapenda kupiga pamba ss hv hawavai kivile.. khaa
Mbona kawaida to!!!
 
Go to hell.
Why should I go to he'll? I am responding to your stupid comments which you thought they were wise ones. Kuwa limbukeni katika maisha ni kitu kibaya sana. Nyani wewe ni limbukeni. Watu kama wewe ukiwaangalia background wametokea familia zenye umaskini wa kunuka, lakini mkipewa vifedha kidogo, niko tayari hata kuuza mama zenu, kisha mnajifanya kujua kila kitu. Kwa taarifa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. At the end you are the one who will go to he'll.

Sent from my HUAWEI GRA-L09 using JamiiForums mobile app
 
Yup!

It’s always been like that.

Hata Magu atapoondoka itakuwa hivyo hivyo tu.
Yaani nashindwa kushangaa, ina maana hawa wote wanaokushambulia kabla ya JPM walikuwa na maisha mazuri saaana ila baada ya Magu kuingia wamechoka? Mtaani sio jehanam kama watu humu wanavyojaribu kuonesha na December hii watu wanaenda vacations zao za milimani na nje ya nchi kama kawaida.
 
Nami nipo mtaani humu humu. Nazunguka huku na kule. Naona kwa macho yangu mwenyewe. Siongelei mambo ambayo siyaoni au ambayo siwezi kuyaona.

Lakini ukiwasikiliza hawa wanaharakati wa mitandaoni unaweza kudhani huko nyuma tulikuwa nchi yenye uchumi wa nchi za dunia ya kwanza na sasa uchumi huo umebadilika kabisa kisa Rais Magufuli.

Halafu sasa, hawa wanaolalamika mitandaoni wanazitoa wapi hela za kununua bando na kuja kulalamika eti hali ni mbaya.

Kama hali ni mbaya si waache kununua bando na wanunue chakula wale.

Bando na chakula kipi cha muhimu?
 
Back
Top Bottom