Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

kaka zaman bata zilikua kama zote bwana... watu wanapak magari yao wanapanda daladala unsema hali sio mbaya..watu kila jumamos walikua wanaenda minada ya nyama lakin sasa hv waulize hao masai anaishia kuuza mbuzi 20 out of 100@day?aka sitak kukubaliana na hoja yako😥
walokua wanapenda kupiga pamba ss hv hawavai kivile.. khaa

Nakuhakikishia UNAZO SABABU BILIONI MOJA za kutoa kwa KUFELI kwako. Ila mark my words wenzio wasiotafuta sababu wanazidi kutoboa na kila siku wanapata hela na kufanya maendeleo, Mfano Mbwana Samatta,Dogo janja, Diamond na wengi sana ambao hawamtafuti wa kumpa lawama pale wanapokwama.
 
Chukua Balimi hapo ulipo. Bili walete kwangu.
 
kwa huku mtaani walio karibu na watawala walamba keki ya taifa hawawezi jua ukweli. hali mbaya kuliko. wapambe wanabaki kuzibaziba
 
Nakuhakikishia UNAZO SABABU BILIONI MOJA za kutoa kwa KUFELI kwako. Ila mark my words wenzio wasiotafuta sababu wanazidi kutoboa na kila siku wanapata hela na kufanya maendeleo, Mfano Mbwana Samatta,Dogo janja, Diamond na wengi sana ambao hawamtafuti wa kumpa lawama pale wanapokwama.

nikufuate nn mkuu unipe dili😢
 
Mkuu NN labda tuanzie tu kama una kitega uchumi chochote unaonaje ufanisi wake awamu hii kama baa,guest house (kuna moja ulisema unayo sijui Muhunze/Malampaka) , mradi wa kufuga kuku/mayai, duka la nguo na bidhaa mchanganyiko,

Kama hauna wewe mradi wowote ebu uliza kwa ndugu na jamaa pia wenye miradi ya kariba hiyo

Hoja itapata mashiko baada ya kurudi na mrejesho kwa utafiti huo mdogo mkuu
 
Maisha ni yale yale...

Tofauti ni kwamba wale waliyozoea kujipatia pesa bila kuvuja jasho au kwa biashara zisizo halali ndiyo waliyoporomoka na kukwama...

Na kwenye mitandao people will say anything even if they know nothing...

Cc: mahondaw
 
Mkuu NN labda tuanzie tu kama una kitega uchumi chochote unaonaje ufanisi wake awamu hii kama baa,guest house (kuna moja ulisema unayo sijui Muhunze/Malampaka) , mradi wa kufuga kuku/mayai, duka la nguo na bidhaa mchanganyiko,

Kama hauna wewe mradi wowote ebu uliza kwa ndugu na jamaa pia wenye miradi ya kariba hiyo

Hoja itapata mashiko baada ya kurudi na mrejesho kwa utafiti huo mdogo mkuu

Kitega uchumi nilichonacho kinafanya vizuri tu.

Mwisho wa mwezi huu/ mwanzo wa mwezi ujao kinalipa tena.

Zero kwenye akaunti zazidi kuongezeka tu.
 
Ukweli unao moyoni kuhusu Hall halisi ya nchi yetu ilivyo sasa kwani haiitaji kuwa na Level ya elimu ya vidudu au PhD ili kubaini kuwa hali ni mbaya maybe kama we ni msukule wa mkuu wa kaya
 
mkuu hali ni mbaya kuna mizigo huwa nauza kwa laki 2-3 leo hii napunguza hadi kilo 1 ila holaaaaa sipati mtu.

wakulima wa korosho watapokea ma bilioni ila hutayaona kwenye mzunguko ni mwendo wa ukame wa mkwanja
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Kuna utafiti wowote uliofanya, au umekuja tu kumwaga upupu? wee endelea tu kubeba mabox utumwani maisha ya huku tuachie wenyewe tunaoyaishi
 
Watu wa mitandaoni wanazungumza majeraha.
 
Huko Usukumani kuna pombe gani kali sana? Maana si kwa kulewa huku.
 
Kuna utafiti wowote uliofanya, au umekuja tu kumwaga upupu? wee endelea tu kubeba mabox utumwani maisha ya huku tuachie wenyewe tunaoyaishi

Nilitafuta kusoma jibu kama hili toka mwanzo, sikuliona. Kwa hiyo mleta hoja ndio kawa 'Twaweza' mpya na utafiti anaodai ameufanya kwa kutembelea vijiwe. Na hii 'Twaweza' mpya ndio inayokubalika zaidi kwetu, kwa maslahi ya taifa letu!
 
Jumatatu ingine hiyo ndo imewadia.

Watu mtanunua bando na kuanza kulialia eti hali ni mbaya! Eti hakuna uhuru wa kutoa maoni huku mkiyatoa hayo hayo maoni mnayosema uhuru wa kuyatoa haupo.
 
Ukitaka kumjua Mwendawazimu, mpe Kilemba Ajifunge
 
Back
Top Bottom