Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Ndiyo tatizo la hawa CPL, huwa wanapenda wahudumiwe kwa kutukuzwa flani, kwa kuwa alipita Depo. Ni uonevu huu, pole sana.

Mpe notice kwanza ili uwe umefuata taratibu za kumwondoa. Kisha ndiyo ziende harakati za kiutaratibu za kumtoa kwenye nyumba yako.

Kama akiendelea ksumbua kutoka na kulipa malimbikizo ya deni, na kwa kuwa hujui kambi yake, basi peleka shauri lake HQ (Upanga) ila jitahidi uwe na nyaraka zote.

Ova
Asante mkuu nimeshapoa.

Nashukuru kwa ushauri mzuri pia. Nitaufanyia kazi.
 
Mimi hao ndio huwa nawakomesha, akishaleta swaga za ujeshi akidhani ananitisha ndipo ninapofurahi, kama nilikuwa namhudumia kwa unyenyekevu nabadili, tunaenda sawa.

Ila sio katika namna ya kuvunjiana heshima, nambana kwa kutumia utaratibu uliowekwa. Sijui kwanini, mwisho huwa wanakuwa wapole.

Atanifanya nini? Kichwani kuna mtu ananipaga kiburi nitakuja kupigwa mimi jamani!

Uko vizuri mkuu.
 
Wakuu habarini za wakati huu. Naandika uzi huu nikiwa na simanzi sana!

Nina eneo langu Ukonga KMKM ambapo nimejenga nyumba moja kubwa ya kupangisha na vyumba vingine 4 vyenye sebule na choo ndani. Nimefanya uwekezaji huu kwa kujinyima sana tena nikitumia pesa yangu halali.

Mimi siishi Dsm kwa sasa. Changamoto ipo kwa mpangaji mmoja bwana mdogo ambaye ni Mwanajeshi mwenye cheo cha Coplo, ni rika langu, yuko kati ya 30-37; ananisumbua sana kulipa kodi. Nimemvumilia vya kutosha. Pamoja na kuweka kodi ndogo lakini bado jamaa ananisumbua mno.

So far namdai zaidi ya milioni moja. Kuna wakati nasafiri kwenda Dar kutazama maendeleo ya makazi yangu na nakutanaga nae lakini anaishia kunipiga sound. Jamaa ni mtaratibu sana, anazungumza kwa upole; kila nikijaribu kumtoa hata kwa kumsamehe hiyo kodi huwa napatwa na huruma.

Kwa sasa enough is enough. Mara ya mwisho nimekutana nae Desemba mwaka jana, akakiri kwa maandishi kwamba namdai na atalipa deni lote Jan. 29 mwaka huu. Kilichotokea ni kwamba tarehe 29 imepita na kakaa kimya! Nikimpigia simu zangu hapokei. Kwasababu niko mbali, nimemtuma mpangaji wangu mmoja ninayemwamwini ili anipe nizungumze nae ila inasemekana jamaa hayupo pale kwa takribani wiki 3, kuna tetesi ameenda kwenye kozi Kibaha.

Ningeweza kwenda kumshtaki kambini kwake lakini sijui yuko kambi gani, kuna wanaosema yuko Lugalo ila hawana uhakika.

Naombeni msaada wakuu, naamini kuna watu ni Wanajeshi humu, wengine mna ndugu zenu Jeshini na hamuwezi kukubali dhuluma ya namna hii, naombeni msaada wa namna ya kuitambua kambi yake, majina yake nayajua, niko tayari kumsamehe hiyo kodi ila anipishe ili nitafute mpangaji mwingine.

Naomba kuwasilisha.

N:B: Wapangaji wote wana Mikataba. Kimsingi huyu jamaa ameshavunja terms za Mkataba muda mrefu. Naweza kumdai kodi Kimahakama lakini sitaki kupoteza muda.
Popote pale kwenye ubaya jua kuna wema ulitangulia.
 
Unajua umeandika kama sisi humu ndio majirani zake huyo afande, sikiliza mdogo wangu, wakati wowote unapopatwa na tatizo lolote jaribu kuwa mtulivu na kama unahitaji ushauri toa maelezo ya kutosha yanayohusiana na msaada unaohitaji, pia usikurupuke kutoa hukumu au kuchukuwa maamuzi kwa kutumia hasira au utashi wako binafsi, unaweza kuwa umeonewa, umedhulumiwa, au vyovyote itakavyokuwa, lakini dunia hii haki pekee haikufanyi uwe na sauti mbele ya mamlaka au sheria, hususan upande huo wa magwanda, kwao wao hakuna sheria za duniani wala za mbinguni zinazofanya kazi, kwahiyo kuwa makini huyo anaweza hata kukunyanganya hiyo nyumba akasema ni yake na mamlaka ikakuweka wewe ndani na kusema ulitaka kumdhulumu, kwa kifupi umeyatimba, nakushauri mvumilie na mpe siku au mwezi kama hajalipa mwambie mimi nyumba nauza, utamuwachia msala huyo atakaekuja kununua, kwa kifupi umeyatimba.
Wewe ndio mpangaji unajaribu kujiongezea muda.
 
Huyo Hana Hela ana majukumu mengi na Mshahara hautoshi.. Vijana hawa wanatoka familia duni sana.. Inawezekana kabisa hata yeye anaumizwa na kodi yako Lkn anashindwa kupata pesa ya kukulipa.

Inawezekana Mshahara wenyewe umebaki kidogo Labda alikupa ili kukarabati kibanda cha wazazi nk.. Muonee huruma! Muache akae tu mkuu tu, Moyoni usimhesabu tena km mpangaji wako.. Mfanye km mdogo wako au mwanao Lkn Usimwambie kwamba akae bila kulipa! Anaweza kuchelewa kukulipa Lkn Anaweza kuja kuwa na faida zaidi kwako.. Kuwa binadamu ingawa Najua jinsi ilivyo ngumu Lkn jikaze ufanye Kazi ya Mungu!
 
Huo mzunguko ndio nisioutaka mkuu. Mali yangu mwenyewe halafu initese tena!

Anyway, nashukuru kwa ushauri.
Mwanajeshi akiamua kukuzurumu nyumba, hutoweza kumfanya chochote; na mpaka ameshindwa kukulipa maana yake ameshakusoma na akaona udhaifu wako, sio kwamba hana hela ya kulipa.
Mamlaka zimewekwa ili kuwafanya watu waishi kwa mujibu wa sheria na taratibu, wakati mwingine urasimu ni muhimu ili kupata haki yako.

Mfano; akisema hatoki hapo kwako, utamfanya nini?​
 
Hivi huko kambini kwao na HQ huwa kuna ushirikiano mzuri kwa wapeleka malalamiko kiasi ninachokisoma hapa?
Nimesikia kuna ushirikiano wa hali ya juu sana. Wanadai ni afadhali ufanye ufedhuli jeshini kuliko uraiani kwasababu unakuwa unalidhalilisha jeshi.

Na mara nyingi ukiweza ku-justify madai yako huwa wanamkopesha askari husika kwa lazima wakulipe halafu watamkata kwa utaratibu wanaoujua wao.
 
Huyo Hana Hela ana majukumu mengi na Mshahara hautoshi.. Vijana hawa wanatoka familia duni sana.. Inawezekana kabisa hata yeye anaumizwa na kodi yako Lkn anashindwa kupata pesa ya kukulipa.

Inawezekana Mshahara wenyewe umebaki kidogo Labda alikupa ili kukarabati kibanda cha wazazi nk.. Muonee huruma! Muache akae tu mkuu tu, Moyoni usimhesabu tena km mpangaji wako.. Mfanye km mdogo wako au mwanao Lkn Usimwambie kwamba akae bila kulipa! Anaweza kuchelewa kukulipa Lkn Anaweza kuja kuwa na faida zaidi kwako.. Kuwa binadamu ingawa Najua jinsi ilivyo ngumu Lkn jikaze ufanye Kazi ya Mungu!

Dah yani ulivyoandika kiungwana inaelekea wewe ndio huyu mpangaji mkuu
 
Mwanajeshi akiamua kukuzurumu nyumba, hutoweza kumfanya chochote; na mpaka ameshindwa kukulipa maana yake ameshakusoma na akaona udhaifu wako, sio kwamba hana hela ya kulipa.
Mamlaka zimewekwa ili kuwafanya watu waishi kwa mujibu wa sheria na taratibu, wakati mwingine urasimu ni muhimu ili kupata haki yako.

Mfano; akisema hatoki hapo kwako, utamfanya nini?​
Nitamfanya nini?? Aisee

Kwani kinachothibitisha umiliki wa nyumba ni hati ya nyumba au existance ya mtu kwenye nyumba hiyo?

Hili swali ni la ajabu sana mkuu

Mamlaka kama Mahakama zipo mkuu, naweza kumtoa kwa nguvu kwa amri ya Mahakama, lakini huyu ni bwana mdogo sana siwezi kufika huko. Najua namna ya ku-deal nae.
 
Unajua umeandika kama sisi humu ndio majirani zake huyo afande, sikiliza mdogo wangu, wakati wowote unapopatwa na tatizo lolote jaribu kuwa mtulivu na kama unahitaji ushauri toa maelezo ya kutosha yanayohusiana na msaada unaohitaji, pia usikurupuke kutoa hukumu au kuchukuwa maamuzi kwa kutumia hasira au utashi wako binafsi, unaweza kuwa umeonewa, umedhulumiwa, au vyovyote itakavyokuwa, lakini dunia hii haki pekee haikufanyi uwe na sauti mbele ya mamlaka au sheria, hususan upande huo wa magwanda, kwao wao hakuna sheria za duniani wala za mbinguni zinazofanya kazi, kwahiyo kuwa makini huyo anaweza hata kukunyanganya hiyo nyumba akasema ni yake na mamlaka ikakuweka wewe ndani na kusema ulitaka kumdhulumu, kwa kifupi umeyatimba, nakushauri mvumilie na mpe siku au mwezi kama hajalipa mwambie mimi nyumba nauza, utamuwachia msala huyo atakaekuja kununua, kwa kifupi umeyatimba.
Ww jamaa ni kilaza sana nawasikitikia watoto wako mkeo, hivi ww unaweza kweli kusimamia familia kweli?

Wanaume hatupo ipo kijana acha mambo ya kike, usiogope kudai haki hako hata siku moja. Alafu hao wanajeshi akienda kambini atapata msaada vizur tu na atalipwa.. hao watu wa vyeo vya chini wana viburi kwasaba ya zile gwanda
 
Nilidhani nimemshangaa jamaa mwenyewe, kumbe tupo wengi
 
Back
Top Bottom