Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Uko sahihi kwa sehemu mkuu.

Ingawa lazima shauri lianzie Baraza la Ardhi la Kata kwa ajili ya Usuluhishi. Wakishindwa Kata ndio liende Wilaya.

Thanks anyway, ingawa sitaki huu usumbufu, nataka tu aachie chumba changu.
Kuna watu ni madhulumati yaliyokubuhu na wasumbufu tu kwahiyo akiamua anakwenda moja kwa moja baraza la wilaya anaweka wakili wa mchongo danadana zinaanza,nilishayapitia hayo ndugu kwahiyo najua ninachokisema.
 
Acha kutisha watu wewe kayatimba yap sheria zipo Na haki itapatikana muhimu yeye kujua cha kufanya akiwa na ushahidi,

Watu kama wewe ndio manaochangia usumbufu kama huu kisa vyeo vyenu
Nashukuru sana mkuu kwa back up hii.

Kuna watu sijui wamebeba nini kwenye vichwa vyao, wanadhani kudhulumu haki ya mtu ni rahisi namna hiyo.
 
Kama hutaki mambo mengi sijui mahakamani ,sijui polisi n.k ...

fanya hivi...

Nenda kwa mjumbe mwambie humtaki huyo mpangaji kwako na sababu ni hii.

hapo atapewa mwezi mmoja au siku kadhaa kama week 2 hivi za kuhama na atahama na

Ikibidi kabisa mtishie huyo mpangaji kwamba utaenda kazini kwake kushitaki kama atagoma kuhama. yaani asipohama huyo labda sijui..
Sitaki afikishe mwezi hapa kwangu. Next stop ni Upanga mkuu, nimeshauriwa na wadau nikaombe taarifa zake pale na kumshtaki pia; naweza kupata msaada.
 
Mkuu watu kama hao uwa wanajiandaa kusumbuana usikute ni mhaya au mnyaki wewe ukienda kwa mjumbe yeye anaenda baraza la ardhi na nyumba na mauongo kibao na hakuna sehemu yenye urasimu kama huko jambo dogo tu ambalo lingeweza kuisha kwa wiki au wiki mbili linachukua miaka mitano na hata ukija kushinda aambiwe akulipe fidia hana chochote cha kukulipa labda ungesema dawa ya wajinga kama hao ni kuwaroga tu kama kweli huo uchawi upo.
Kuwaroga tena mkuu
 
Huyo anachukulia poa lkn tumpe muda huyo jamaa hata kama ni kuruta sio maskini wakushindwa kulipa kodi, mshahara wa chini kwa mwanajeshi haupungui 1.2 take home, ndio ashindwe kulipa 50 au 70 kwenye hilo, na kama anaishi bila ya familia itakuwa pesa zote anamalizia kwenye pombe au wanawake, maana kwenye kambi nyingi za jeshi wameweka bar mshahara ukitoka tu inakuwa kama fungulia goli.
Kwenye pombe kweli ni mtu wa tungi sana na madem pia.

Recently ndio nimemuona ana kadem kamoja ambako nadhani anataka kukaoa, akiwepo hapa huwa kanaenda na kuishi nae.
 
Mimi nimetoa ushauri wangu kwa mujibu wa huyo mtoa mada akili yake ilivyo, sikutoa ushauri kama ningekuwa mimi, kwa sababu ningelikuwa mimi asingewahi hata kujaribu kunifanyia hivyo, tungeheshimiana
Jaribu kuficha ujinga wako mkuu (ujinga sio tusi)

Akili yangu unaijua wewe?

Yani una uwezo wa kuijua akili ya mtu kupitia uzi tu?
 
Kuna watu ni madhulumati yaliyokubuhu na wasumbufu tu kwahiyo akiamua anakwenda moja kwa moja baraza la wilaya anaweka wakili wa mchongo danadana zinaanza,nilishayapitia hayo ndugu kwahiyo najua ninachokisema.
Sheria ilishabadilika mkuu, lazima shauri lianzie Kata, wakishindwa wanaidhinisha ndio liende Wilaya.

Huyu ni bwana mdogo sana kama nikiamua ku-deal nae kidunia. Ana vingi vya kupoteza kuliko mimi. Ni vile tu sina muda wa kupoteza.
 
Back
Top Bottom