Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

MREJESHO:

Kama wengi mlivyoshauri, jana nilifika Ngome-Upanga majira ya saa 9 alasiri. Nikapokelewa na na maafande pale getini nikaulizwa shida yangu, nikajieleza kwa ufupi, kabla ya kukaribishwa ndani nikapewa kiti kwanza nikae palepale getini na kupewa pole!

Afande mmoja muungwana sana ambaye alionekana ndio kiongozi wa walinzi wa siku ya jana pale getini, akaniomba nionyeshe nyaraka zozote (kama ninazo) kuthibitisha namdai. Nikatoa mkataba na commitment aliyoifanya Kwa maandishi nilipokutana nae mara ya mwisho Desemba mwaka Jana na kuahidi kunilipa ifikapo tar 29/01/2024.

Kwanza maafande wakanishangaa kwanini nimemruhusu akae muda wote huo bila kumbananisha alipe au nimfukuze.

Wakaniuliza kama nina picha yake nikawaonyesha picha yake aliyoweka Whatsapp. Baadhi ya maafande wakamtambua.

Wakaniomba sana kwamba nisipeleke hili swala ndani, watakachofanya ni kwamba watawasiliana nae ili j3 aje alipe au kama hana pesa achukue mkopo anilipe j3 hiyohiyo.

Kwahiyo wakaniomba nifike Ngome j3 kabla ya saa sita mchana. Nitamkuta mdeni wangu. Nikachukua namba ya yule afande in charge nikasepa zangu.

Wakuu, leo asubuhi wakati naamka nimekuta msg za mdeni wangu akinibembeleza kwamba j3 tukutane pale Ngome nje anilipe pesa yangu yote . Nadhani wale maafande wenzake wameshampigia.

Ndugu zangu, nawashukuru sana kwa ushauri. JF forever! Nimepanga akishanilipa tu j3 namlamba na notice ya mwezi mmoja ahame.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI.
Hongera mkuu wakati mwengine woga wako ndio unaokuzuia na kukurejesha nyuma, lakini pia usidharau ushsuri uliopewa wa kuwaogopa hao watu, ni kwa sababu tu kuna wengine hawajawahi kukutana na maswahibu ya hao jamaa mitaani ukiwakera, lakini ukweli ni kwamba wakati mwengine hao jamaa ukiwakera hata kama wao pia wana makosa wanaweza kuambizana wakaja na difenda mbili au tatu wakachezesha kipigo mtaa mzima, watakuanza wewe na wote watakaojifanya kukutetea, hata hivyo pamoja na kuahidi kukulipa nakushauri ukae kwa machale kwa sababu hayo malipo munafanyiana kienyeji huko juu utawala hawafahamu kinachoendelea kwa hiyo bado nakusisitiza kuwa makini sana ingawa ushauri kama huu nikiutoa naonekana mwendawazimu lakini kumbuka kwa muoga huenda kicheko kwa shujaa huenda kilio. Tusije tukaamka siku moja tukakuta magazeti yameandika mwili wa kijana......... Wakutwa umetupwa kwenye mtaro.
 
Nashukuru sana kwa ushauri huu mkuu. Nitaufanyia kazi.
 
Pole sana but anyway kama umeombwa usimripoti ngazi za juu basi kausha kikubwa amekupa chako flash ila keshajuwa we sio mnyonge unaweza tia kitumbua mchanga, cha muhimu we ukai hapo na sinkwamba ela yake pekee ndo unaitegemea

Kuna siku nilishawahi tia kofuli ktk bomba bila kusema kitu maana niliwapa bill yao alafu hawalipi na dawasco hawachelewi kukata nikatia kofuli na sijaonekana wiki nilivuoona notification ya malipo nikaja nikafungua adi kesho bili ikifika hailali

Uyo mjeda we mtreat tu kama watu wengine kama chumba atakuwa na umuhimu nacho basi atalipa kwa wakati kwa jinsi ulivyomwonyesha hii action,
 
Asante mkuu, nimekuelewa sana.

Nakushukuru mno.
 
AMESHANILIPA PESA YOTE IN CASH JANA, PLUS KODI YA MIEZI 3 IJAYO. SASA HIVI NI MWENDO WA PRE PAID ARRANGEMENT TU.

ASANTENI SANA WAKUU.
Heh.. kaendelea kuwa mpangaji wako tena? Huogopi akirudia kosa itakuwa usumbufu tena?
 
Mkuu, kashajua rangi zangu zote, before alinichukulia kolo.

Kalipa deni na kalipia mienzi mingine 6 ijayo, pesa tamu mkuu, nilishindwa kuikataa
 
Back
Top Bottom