Nakanusha: Hospitali za Umma hazipendi kutoa huduma mbovu isipokuwa majukumu yanawalemea

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,114
4,798
Kuna mdau amelalamika sana kwamba ameenda hospitali ya Umma akakuta huduma ni mbovu na wagonjwa ni wengi sana ila watumishi wanapiga tu story mpaka wagonjwa wengine wanazidiwa mapokezi.

Amedai mgonjwa anapokelewa saa mbili ila hadi saa nne hajapata huduma yoyote!

Naomba nikanushe na nijibu tuhuma za mdau.

Mimi nimefanya kazi hospitali zaidi ya moja, tatizo kubwa linalosababisha huduma zizorote hospitali za Umma ni ufinyu wa wafanyakazi wala sio kwamba ni wazembe.

Mfano nautolea kuna hospitali zinahitaji watu zaidi ya 30 lakini unakuta wahudumu ni kumi tu.

Mfano hospitali ya kanda ya mtwara kiuhalisia inatakiwa kuwa walau na wafanyakazi 200 lakini mpaka sasa wapo chini ya 50 idadi ambayo haiendani kabisa na jumla ya wagonjwa wanaokuja hapo.

Nimefanya kazi hospitali moja yenyewe ni kituo cha wanafunzi kufanya mafunzo kwa viitendo, ile hospitali ni kama imetelekezwa wahudumu ni wanafunzi tupu.

Hospitali za vijijini mpaka raia wanaitwa wasaidie kutoa huduma, imagine zahanati nzima muhudumu mmoja, hana off hana masaa ya kazi hata saa saba usiku anaamshwa akazalishe anazalisha mtu saa kumi usiku, halafu asubuhi anatakiwa kazini! haya mambo yapo na tunayapitua sio story,
wahudumu wa afya wanafanya kazi kubwa sana tusiwabeze.

Mfano mwingine mdau amelalamika kua unaenda hospitali saa mbili hadi saa saba hakuna huduma yyte.

Kuna hospitali kubwa tu lakini unakuta ina maabara mbili tu, au moja kiasi kwamba watu zaidi ya 200 wanasubiri majibu toka maabara moja kwa wakati mmoja.

Muiambie serikali ya CCM iboreshe huduma za afya musisingizie kua watumishi ni wazembe.

Wodi moja usiku mmoja unakuata ina muuguzi mmoja! Mnataka afanyeje?

Mhudumu mmoja wagonjwa 70 unategemea huduma gani bora hapo?

Tusidanganyane hapa wala tusilaumu wwatumishi wa afya

Kuna hospitali niliwai kushangaa usiku mzima nesi ni mmoja wodi nzima tena ni mwanafunzi

Narudia tena tatizo sio sisi watumishi tatizo ni serikali yenu.

Shida inakuja pale mgonjwa yuko wodi A anaona hapati huduma anashangaa kuona watumishi wengine wako nje wanazunguka ambao hata huwenda hawahusikibna hyo wodi.

Mtu akiwa na mgonjwa akiona mhudumu yoyote anataka amhudumie bila kujua hospitalini kuna vitengo mbalimbali.

Hata watumishi wa umma wanatamani wawahudumie vizuri kama private tatizo ni kulemewa na majukumu private watumishi wengi, wagonjwa wachache.

Umma watunishi wachache sana wagonjwa wengi!

Msilaumu watumishi mpk kuwatukana wanafanya kazi nzuri sana

serikali inabidi iongezeje bajeti wizara ya afya wajenge miundombinu inayoendana na idadi ya watu pia waongeze watu
mishi, muone kama huduma zitakua za hovyo

Mungu ibariki Tanzania na watumishi wa Afya
IMG_20220702_134236.jpg
 
mama anenda kirekebisha haya...tusiwe na shaka kabisa kabisa....
 
Unataka wananchi walalake kwa Nani?

Na kwa nini mmekubali muwe wachache ilihali wenye taaluma hiyo wapo tu na vyeti vyao mitaani.?

Kama mmekaa kwa kutulia ilihali mnajua mko watoa huduma wachache, basi mnao huo uwezo wa kuhudumia

Msilalamike, chapeni kazi!

Lakini pia, Mwendazake aliwezaje kuwafanya mpunguze haya malalamiko ya wananchi.?
 
serikali inalijua hilo lakini ipo kimya, zahanati huko vijijini zinaemdeshwa na mtumishi mmoja, mda mwingine hata yeye anachoka anafunga anajificha, ndo maisha yanavyoenda ivyo

lawama waipelekee CCM sio watu wasiohusika
Hii sekta inahitaji kipaumbele kama ilivyo elimu sema ndio hivyo, wanaotutawala wakiumwa wanatibiwa nje ya nchi hivyo hawaoni matatizo yanayowakabili raia.
 
Hata nyie mnaoajiriwa mnazingua, mkipata mishahara miwili mnaanza kujibu kunya...
Nakupa mfano mmoja hospitali ya wilaya unakuta wodi ya kujifungua mkunga mmoja wazazi 20, anamaliza huyu anaingia huyu unafikiri kwanini ukizingua asikujibu kunya
 
Mfumo mbovu wa Ujamaa alioujenga Nyerere ndiyo umetukwamisha kiuchumi. Uchumi ukikwama, hata huduma za afya zinakuwa mbaya. Ndiyo maana vigogo wakiugua wanaenda kutibiwa nje ya nchi.
 
Tatizo mnapenda sana rushwa halafu msivyo na aibu mnadai kabisa kama vile ni haki yenu..
Madaktari wengi hasa wanaohusika na uzazi wamegeuza hospital kuwa miradi yao binafsi.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Naungana na wewe mkuu , wahudumu wa Afya serikalini Kwanza niwape pongezi Sana , mnafanya kazi ngumu ya kuogofya mno , mazingira magumu ya kazi , mnakuwa overwhelming na idadi ya wagonjwa , wakat mwingine mgonjwa anakufia mkononi sio kwamba ni uzembe Ila vifaa hamna, unaweza Lia kabisa but nothing you can do....

Serikali yetu hi worst na terrible Sana upande wa Afya ....!!! Inashangaza hii ndo Wizara ambayo ingetakiwa kuongoza Kwa kuwa na ukubwa wa bajeti lakini hata kwenye top 5 nafkri hata haimo wakat ndo imebeba uhai wa raia ...

Watu wengi wanafariki Kwa kukosa matibabu stahiki , kiuhalisia daktari hawez fanya lolote kama mazingira sio wezeshi
 
Back
Top Bottom