Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,565
Kutokana na baadhi ya hospitali binafsi kusitisha huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia leo Machi mosi, 2024, uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umekuja na mpango wa dharura wa kuwahudumia.
Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wawe na mwendelezo wa huduma. Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mohamed Janabi amesema hayo leo kupitia mtandao wa Instagram wa hospitali hiyo.
Amesema MNH imeongeza muda wa kuona wagonjwa katika kliniki zote za Upanga kupitia vyumba 75 vya kuona wagonjwa na vyumba vya kuona wagonjwa 59 viliyopo Mloganzila.
Profesa Janabi amesema huduma inaanza saa tatu asubuhi hadi saa nne usiku au mpaka mgonjwa wa mwisho atakapomaliza kuonwa na daktari.