Najuta kuacha kazi

Najuta kuacha kazi

hata sukari kilo 1 anashindwa
Ndio hapo.. imagine ingekua vise versa mwanamke ndo ana hela.. afu aseme maisha magum hawez kumtembelea mama mkwe wake hana cha kupeleka, ila kwao anaenda na zawadi juu.. people are so selfish.
 
Tatizo kubwa hapa ni wivu. Kwamba mume wako anawatunza wazazi wake lakini wewe huwezi kumtunza mzazi wako. Naamin hata yeye angekuwa hatumi hela kwao wala usingeumia kiasi hiki. Pia angekuwa haendi kwao, wala usingekuwa na shida. Women!Jealousy!
Duuuh!.. sidhani kama uko fair. Maneno ya mtu alieshiba bila kujali asienacho.
Watu mnafurahiaga sana kumdunisha mtu alie tiari hajiwezi. Mnaona mko sawa yote mnayofanya na kuvijustify in a best twisted way..
 
Basi hapa ndo nilikuwa nafeli,maana huwa sina tabia ya kuomba twice
Yaan best usipokuwa na moyo wa uthubutu ukamnyenyekea ukasubiri akutimizie kila kitu na ivi ni km shemela ana ubinafsi flani utachoka sana jiongeze uku ukimpa heshima ile ile atakuelewa
 
🤣🤣🤣

🤣🤣🤣 we kwanini uwe na jeuri, KE mwengine haishi visa tu maana si ana hela yake...Anakuwa anavimba tu, kitu hata unachomkataza asifanye anafanya makusudi maana hata ukimaindi haimstui ye anapeta tu. Si anajiweza bana...

Wanaume wengi tunatumia hio mbinu kama weapon ya kuwafanya wake zetu wenye kipato na wanaojisahau kuwa submissive. Ubaya ni kuwa mke akianza kuwa tegemezi 100% mizinga inawahi kutuchosha ndio unaanza kumkwepa tu.
Hapo ndo huwa changamoto kubwa, afu uwa mna mawazo yenu ya inferiority flan mwanamke akiwa na pesa asikutegemee kwa vitu vidogovidogo......mnakosea, acheni mwanamke atafute mtasaidiana coz hata familia yake huwa inamtegemea sasa kwann aombe pesa ya matumizi kwako, aombe sjui mama hana sukari, sjui dogo ada, aaaghhhrr mnakera mnafikiri kuolewa ndo kutenganishwa na familia yake sasa???
 
Yaan best usipokuwa na moyo wa uthubutu ukamnyenyekea ukasubiri akutimizie kila kitu na ivi ni km shemela ana ubinafsi flani utachoka sana jiongeze uku ukimpa heshima ile ile atakuelewa
Aanze kuuza hata papuchi,mtaji upo anao
 
Mme wako hakuamini uenda una matumizi mabaya ya hela hasa kipindi kile ulipokuwa nazo. Uenda pesa yako yote ilikuwa inaishia nyumbani kwenu tena kwa jeuri pasipo kuchangia kitu hapo kwenye familia yako ya sasa. Ndiyo maana anapata shida hata kukupatia mtaji akijua utautumbua na kisha mtaanza kugombana. Inabidi umuaminishe mmeo kwamba umebadilika na una nidhamu ni pesa.
 
Pole sana kuacha kazi ni mbaya sana labda uolewe huna kazi, lakini Mme akwambie acha halafu hana budget yeyote kwako mmmm mbaya! niwachache sana ambao anaweza saidia kwao na mkewe kwa usawa au hata ile kiasi , wapo husema sijaoa ukoo nimekuoa wewe, hawajui kama yeye alivyozaliwa na mkewe vivyo hivyo, kaa chini ongea naye.
 
My dear nilishakaa naye tukaongea na tukamaliza kwa kumshukuru Mungu (Maombi)ila huwezi amini ni six months toka tuongee na yupo kimya jamani..i will try tena leo kama akija na mood nzuri..Asante
Mtu wawapi huyo, maana kuna wengine wanaishi kwa kukushikiwa na familia zao badala ya wao kukaa chini na mkewe kupanga mikakati yao
 
1.kwamda huwo mlioishi na mwenza wako kwenye ndoa + uchumba lazima utakua unamjua vizuri mwenza wako ilitakiwa uwe umejiongeza kwa namna yoyote ile upate njia mbadala ya kuingiza kipato mf kwa ela ya matumizi unayoachiwa kuibudget ukaingia vikoba mwisho wa siku ada za ndugu zako zisingekushinda

2. Mumeo akiwa chumbani kwenye mood nzuri ndosehemu ya kuomba vitu kama mitaji na mambo yanayoshabihiana na hayo,ruksa ya kwenda kwenu inaombwa hapo unataka kunambia hujafundwa wewe??miaka hiyo 6 yote kwenu hujaenda au?

Kuwa mpole na mnyenyekevu kwa mmeo atakupa ruksa ya kufanya haya unayoyaona magumu ila ukipewa nafasi usiinue mabega na kuonyesha dharau utaishia kuwekwa benchi

Cc Kingsmann
Tuwaongezee sauti amor

Unforgetable
 
Ongea na mumeo kama mlipanga uache kazi naimani mnaweza kupanga ni jinsi gani mnaweza kuondokana na changamoto uliyonayo .
Ushauli ukitaka kuacha kazi sababu mume kakwambia hakikisha anakipato Mara 2 au tatu yako
Tatizo si kipato bali ni ule moyo wakumpa mkewe ili naye asaidie ndugu zake au wazazi wake, uchoyo wakwani ni wazazi wangu!
 
Kuna siku nilimwambia jioni yake akanipa elfu 50 nimtumie mama
Kwanini asiiweke kwenye budget zake anapowatumia kwao bila kukumbushwa nawewe anakupa unamtumia mama? Ubinafsi mkubwa wakati kakuachisha kazi yako ongea naye tena usichoke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom