Najuta kuacha kazi

Najuta kuacha kazi

La Princesa pole sana
Kwanza jiondoe kwenye hilo group kwa sasa jipe muda wa kuchanganua mambo
Mzungumze na mume wako magumu unayopitia na kumuelewesha unahitaji kumtunza mzazi wako na pia akusaidie mawazo kwa pamoja kama familia namna ya kujikwamua kiuchumi na mengineyo.
 
Unathubutuje kusema kua mume wako hajakukosea? Kitendo cha kuto kujali wazazi wako na huku akijua huna kipato ni kosa kubwa kuliko kumkuta na mchepuko!
Hiyo tabia ya mumeo ya kibinafsi sana binafsi mimi nisingeweza, nashibaje wakati sina uhakika kama mama yangu amepata chakula !?
 
Duuh kwaio kwanini wazazi wako wasiwasomeshe hao wadogo zako? Hadi uwasomeshe wewe? Ni jukumu la mzazi kusomesha mtoto wake, ila kwa ushuhuda tu mimi nilishawahi kuacha kazi sehemu ili nijiajiri sikua na back up plan nilitaka nimgeze mzee wangu aisee nilipitia waya mkali sana siwezi kusahau 2016 ilikua ngumu sana sema sababu CV ilikua inaeleweka nikaanza omba kazi tena Mungu si athumani wala abdallah nikapata lazi kufanya kazi miezi minne ikafungwa ofisini nikasota miezi kama 11 nikaja pata sehemu..ambayo kimsingi si haba maisha yanaendam.cha msingi omba kazi upya utapata tu
Familia hazifanani, wengine sisi watoto wa kwanza ndio wakombozi wa familia nzima
Binafsi nimeshiriki kikamilifu kuwafikisha wadogo zangu walipofika na najisikia fahari
 
Chezea wanaume akijua tu ana deni kwako
Kila siku atarudi hana mood ama kachoka,

I've been there namuelewa bi dada anachopitia
Nami ndo maana nkamwambia awe na msimamo, wengine adi mnuniane wiki nzima akiona umekaza anashuka mambo yanaenda na ahadi zinaanza kutekelezeka, kitu mwanaume apendi ni kuona una jeuri ya kufanya mambo yako bila kumtegemea kwa kila jambo
 
Unathubutuje kusema kua mume wako hajakukosea? Kitendo cha kuto kujali wazazi wako na huku akijua huna kipato ni kosa kubwa kuliko kumkuta na mchepuko!
Hiyo tabia ya mumeo ya kibinafsi sana binafsi mimi nisingeweza, nashibaje wakati sina uhakika kama mama yangu amepata chakula !?
Yaan apo ndo anazingua, bidada kawa km housemaid sasa ata salam kwao ataki, je mama akiwa na shida kweli atasaidika kwa mkwe???
 
Shemeji mke wa bwana mdogo alileta hizo na jamaa akamwambia nenda. 5 months down the line mwanamke anataka kurudi na jamaa akagoma kabisa. Ilibidi mwanamke akalilie ukweni na mama mtu kumrudisha kwa nguvu mguu kwa mguu. Kuondoka home kwa hasira in most case inaharibu badala ya kujenga
Kuna wengine wanaondoka na mambo yao yanawaendea fresh tu tena unakuta anampiga fimbo jamaa kiuchumi
 
Familia hazufanani, wengine sisi watoto wa kwanza ndio wakombozi wa familia nzima
Binafsi nimeshiriki kikamilifu kuwafikisha wadogo zangu walioofika na najisikia fahari
Sawa mkuu ni kweli kama ulivyosema kua familia hazifanani..hongera kwa kuwasomesha wadogo zako..
 
Mkataba wangu wa kazi uliisha nikatafuta kazi sehemu nyingine nikapata,mme wangu akanishawishi kuwa mshahara ni mdogo kuliko Mwanzo halafu ni mbali na yeye so bora nijiajiri huku nikiangalia fam kwa ukaribu

Toka nimeacha kazi,nakosa hata pesa ya mahitaji yangu muhimu,mtaji nilioahidiwa siuoni,nna madeni chungu nzima coz nawasomesha wadogo zangu wawili walikoko college(jamaa hajawi hata kunisupport na anajua situation ya nyumbani kwetu) inaniuma sana pale mama yangu anaponiomba hata elfu 20 nakosa ya kumpa wakati nikiwa kazini nilikuwa nampa pesa nyingi na kuhudumia fam bila shida..

Roho inaniuma coz ninashuhudia jinsi mme wangu na wanafamilia wenzie wanavyopanga budget ya matumizi ya wazazi wao (kwa whattsapp family group na amount ili wawapelekee wazazi wao wakati mimi mama yangu hana kitu kabisa..kwa kweli nimekata tamaa na sijui hata nifanye nini😭😭kuna wakati natamani hata kurudi kwetu ili nikajipange upya na kuanza upya maisha yangu ila nafsi inakataa

Note:mme wangu hajawahi kunikosea ni mambo kama hayo tu ndo yanayoniumiza,halafu anapenda niende kwao tu,hataki niende kwetu na wakati njia ya kwenda kwao ni lazima upite mkoani kwetu na mara nyingi tunakuwa na private car but kupita anakuwa mgumu sana..hivi wanawake wenzangu mliopo kwenye ndoa situations kama hizi mnazihandle vipi?NISAIDIENI NAKUFA kwa MAWAZO

PS: NSSF nao wananizungusha kweli kunipa kapesa kangu kadogo,nina imani nikikapata katanisaidia kuinuka tena

MI ni mwanaume ila wanaume wengi ni kama Ma Mbwa, imeniuma sana, tafuta kazi tu taratibu; haya mandoa ni vidungo!

Mungu akisaidie na akupe wepesi ili hili jaribu likuache mapema, wanaume si watu wa kuamini kwenye pesa!
 
Yaan apo ndo anazingua, bidada kawa km housemaid sasa ata salam kwao ataki, je mama akiwa na shida kweli atasaidika kwa mkwe???
Alafu anajisifu kabisa kua hawana matatizo wakati huyo mumewe ni tatizo kubwa sana, mimi bora mwanaume awe na michepuko huko lakini linapokuja suala la wazazi wake na wangu hakika nitasimama kidedea
 
Kuna wengine wanaondoka na mambo yao yanawaendea fresh tu tena unakuta anampiga fimbo jamaa kiuchumi
Kabisa. Cha muhimu ni kutumia akili tu badala ya moyo kabla na/au baada ya kuamua kubwaga manyanga
 
Kazi zetu miye na mwenza wangu naonaga Ndiyo zinaleta utulivu ktk mahusiano yetu.
Sababu shida za familia yangu huwa hazimgusi yeye moja kwa moja.
Pole sana kumunyesha kuwa hupendi anza kuomba kazi tena, km anajitambua anaweza rudi kwenye mstari.
Wanaume hawapendi wanawake wawe tegemezi 💯 lkn pia hawapendi woote muwe mnatoka asbh.
 
1. Hakuna marefu yasiokuwa na mwisho

2. Kila jambo linachangamoto zake....vumilia

3. Huwezi kumwambia akuelewe wewe binafsi hilo halipo
..... Newton's first law of motion & momentum

The body will continue in its state of rest or uniform motion unless acted by external force

Huyo anahitaji external force...this force must come from one among his family...mtu ambaye yeye anamgwaya na kumsikiliza, anaweza kuwa baba, mama , kaka/dada au mjomba/Shangazi nk
Na huyu mtu lazima pia awe na uelewano mzuri kwako na anakuheshimu nakukusikiliza shida zako... HUYO NDIYO MPE MATESO YAKO AYAFIKISHE KWA MUMEO....external force, meaning the rate of change of momentum is directly proportional to the equal applied force. What you're applying is not proportional to change the state of rest or uniform motion of you're husband..... He is used to hear from you and you're just as making noise to him. Someone respected from external may do at least.

2. Ukifanya mchezo/mzaha ndoa yako inavunjika na inaokena upo at the edge if trend showing throughout you're presentation is real at that state....psychologically you're at the plastic deformation prior to breaking point with respect to hooks law of elasticity on materials failure mode.

Thanks
I LIKE IT MKUU
 
Bila shaka kama ni mumeo wa ndoa jaribu sana kuangalia wapi ulimi ulikuponza .. zen ujiweke sawa na dhani mambo yatakua poa tuu.. wanaume hatujui kupigiana makelele na mwanamke action inatosha
Mkuu hakuna cha ulimi hapo ulipomponza huyo mwanaume tu ni selfish mama pole sana ebu jitahidi kuanza kutafuta kazi tena Mungu anaweza kukusaidia ukapata
 
wanawake kulalamika ni jadi yenu,dada kuwa na subira mwelewe mumeo mpe muda kidogo naamini jamaa atakuwa amebanana na jambo fulani.
 
Huenda, au pia itakuwa mme wake ni mkali.
Mimi nilipokaribia kujigungua niliacha kazi lkn na mkataba wangu ulikuwa mbioni kuisha. Hivyo tukakubaliana na Mr nitulie kwa muda ili nipate nafasi na muda wa kulea mtoto hasa kwa vile kituo changu kilikuwa mbali na kwangu.
Ila tangu nimejifungua, almost a year now sijawahi kupata changamoto za fedha na mme wangu wala sio kusema ana mshahara mkubwa sana. Na mara anasaidia kwetu au wadogo zangu waliopo chuo bila ht ya mm kujua, nakuja kujua badae sana tena kupitia kwa mama au wadogo zangu wenyewe. Na kwa hilo kila siku namshukru sana Mungu.
Doh!. Pole sana. Utakua kiaina unamuogopa mmeo. Means sio rafikiako kiviiile..
Me siko kune ndoa. Ushauri wangu unaweza kua ni wa ki-wapenzi zaidi.. ila pole sana
 
Uko sawa kbs
Alafu anajisifu kabisa kua hawana matatizo wakati huyo mumewe ni tatizo kubwa sana, mimi bora mwanaume awe na michepuko huko lakini linapokuja suala la wazazi wake na wangu hakika nitasimama kidedea
 
Jaribu kufkiria kipind unafanya kazi na unapata hela ulikuwa na mchango gani kweny familia , ulikuwa na tabia gan za tofaut

Usije mlaumu mshkaj kumbe ww ndo umeyataka

All in all badilika inaonekana ukishika hela kidogo unakuwa tofaut ndo maan inampa shida yy kukuamini tena

Anza kumjengea uaminifu utampa moyo wa kukupa mtaj tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom