Najuta kuacha kazi

Najuta kuacha kazi

Mkataba wangu wa kazi uliisha nikatafuta kazi sehemu nyingine nikapata,mme wangu akanishawishi kuwa mshahara ni mdogo kuliko Mwanzo halafu ni mbali na yeye so bora nijiajiri huku nikiangalia fam kwa ukaribu

Toka nimeacha kazi,nakosa hata pesa ya mahitaji yangu muhimu,mtaji nilioahidiwa siuoni,nna madeni chungu nzima coz nawasomesha wadogo zangu wawili walikoko college(jamaa hajawi hata kunisupport na anajua situation ya nyumbani kwetu) inaniuma sana pale mama yangu anaponiomba hata elfu 20 nakosa ya kumpa wakati nikiwa kazini nilikuwa nampa pesa nyingi na kuhudumia fam bila shida..

Roho inaniuma coz ninashuhudia jinsi mme wangu na wanafamilia wenzie wanavyopanga budget ya matumizi ya wazazi wao (kwa whattsapp family group na amount ili wawapelekee wazazi wao wakati mimi mama yangu hana kitu kabisa..kwa kweli nimekata tamaa na sijui hata nifanye ninikuna wakati natamani hata kurudi kwetu ili nikajipange upya na kuanza upya maisha yangu ila nafsi inakataa

Note:mme wangu hajawahi kunikosea ni mambo kama hayo tu ndo yanayoniumiza,halafu anapenda niende kwao tu,hataki niende kwetu na wakati njia ya kwenda kwao ni lazima upite mkoani kwetu na mara nyingi tunakuwa na private car but kupita anakuwa mgumu sana..hivi wanawake wenzangu mliopo kwenye ndoa situations kama hizi mnazihandle vipi?NISAIDIENI NAKUFA kwa MAWAZO

PS: NSSF nao wananizungusha kweli kunipa kapesa kangu kadogo,nina imani nikikapata katanisaidia kuinuka tena
Siri za kifamilia unazileta nje??
 
Asante,mkuu nakwambia hivi pesa ya kujikimu mahitaji yangu mwenyewe nakosa kwa mfano wakati nipo kazini nilikuwa naenda saloon nasuka,nafanya pedicure now siwezi coz nakosa hiyo pesa

Sokoni huwa naenda naye tunanunua vitu yeye analipa hapo ndo ilipo changamoto,pesa yake kuishika ni mpaka awe amesafiri na hapo vitu vinakuwepo ndani so ndo anaweza akaacha pesa kiasi ya emergency
Mpenzi huyo mmeo kazidi sasa hata kama ni ubinafsi si hivyo, niachishwe kazi hata matumizi yangu nikose aise hapana, wakati mwingine tunajifundisha kjongea pasipo kupenda wala kutaka huko nikuburuzana sasa, tafuta kazi mwenzangu maana utapauka mpaka, na usitafute kwa ubabe mwambie mtu kukaa bila kazi siwezi ili usionekane mbabe
 
Wanaume wengi hawapendi tufanye kazi ila pia hawataki tuwategemee kwa kila kitu. Akili kumkichwa, anaekushawishi kuacha kazi ilihali hakusaidii kwa lolote inapaswa ujitafakari sana maana kuna leo na kesho.
Mkuu kumbe ushaolewa? Basi nimechelewa
 
Yupo close na dada yake kuliko wewe?

Ninavyoona..mambo mengi huwa anaanza kumwambia dadake halafu mi ndo nafuatia au unakuta kingine hajaniambia bado kwenye story na dadake anajikuta kaniambia akidhani najua kumbe nakuwa sijui..ila siwezi kumjudge katika hili
 
Duuuh!.. sidhani kama uko fair. Maneno ya mtu alieshiba bila kujali asienacho.
Watu mnafurahiaga sana kumdunisha mtu alie tiari hajiwezi. Mnaona mko sawa yote mnayofanya na kuvijustify in a best twisted way..
Kujenga hoja ni mtihani kwa wengi. Inawezekana ana suala la msingi, ila namna anavyolielezea linamfanya aonekane 'mtu wa ajabu'. Lazima tumuambie ukweli kwasababu vinginevyo hili jambo litamvunjia ndoa yake. Lakin pia, lazima aelewe kwamba kama anataka mtaji, sio lazima apewe na mumewe. Aombe kwa ndugu zake, wajomba, binamu, apate mtaji afanye biashara. Pia, lazima aonyeshe nia. Aanze hata kuuza maandazi(mtaji wake ni mali kauli kwa mangi-mafuta,unga,hamira).Chapati ni rahisi zaidi. Let her take initiatives.

Nyie mnaelialia nae hapa mtaonekana mnamjali sana. Mtamdis hata mume wake wakat hamjasikiliza mume wake kujua kwann hajampa mtaji kama alivyoahidi. Ukweli ni kwamba hapa wengi ni waombolezaji, wanalia na wewe leo, kesho wakisikia msiba kwingine, wanaondoka na kwenda kulia kwingine.
 
Mkataba wangu wa kazi uliisha nikatafuta kazi sehemu nyingine nikapata,mme wangu akanishawishi kuwa mshahara ni mdogo kuliko Mwanzo halafu ni mbali na yeye so bora nijiajiri huku nikiangalia fam kwa ukaribu

Toka nimeacha kazi,nakosa hata pesa ya mahitaji yangu muhimu,mtaji nilioahidiwa siuoni,nna madeni chungu nzima coz nawasomesha wadogo zangu wawili walikoko college(jamaa hajawi hata kunisupport na anajua situation ya nyumbani kwetu) inaniuma sana pale mama yangu anaponiomba hata elfu 20 nakosa ya kumpa wakati nikiwa kazini nilikuwa nampa pesa nyingi na kuhudumia fam bila shida..

Roho inaniuma coz ninashuhudia jinsi mme wangu na wanafamilia wenzie wanavyopanga budget ya matumizi ya wazazi wao (kwa whattsapp family group na amount ili wawapelekee wazazi wao wakati mimi mama yangu hana kitu kabisa..kwa kweli nimekata tamaa na sijui hata nifanye nini😭😭kuna wakati natamani hata kurudi kwetu ili nikajipange upya na kuanza upya maisha yangu ila nafsi inakataa

Note:mme wangu hajawahi kunikosea ni mambo kama hayo tu ndo yanayoniumiza,halafu anapenda niende kwao tu,hataki niende kwetu na wakati njia ya kwenda kwao ni lazima upite mkoani kwetu na mara nyingi tunakuwa na private car but kupita anakuwa mgumu sana..hivi wanawake wenzangu mliopo kwenye ndoa situations kama hizi mnazihandle vipi?NISAIDIENI NAKUFA kwa MAWAZO

PS: NSSF nao wananizungusha kweli kunipa kapesa kangu kadogo,nina imani nikikapata katanisaidia kuinuka tena
pole mama,,ila ulikosea sana kuacha kazi mapema bila kupewa msingi wa mtaji kwanza,,ilitakiwa akupe kwanza at least 10-15m ndio uache kazi,,sometimes sisi wanaume tuna porojo nyingi kwa wake zetu ila kuzitekeleza ndo inakua ngumu,,huyo jamaa alikua anatamani tangu cku nyingi ubaki nyumbani ulee familia,kifupi ni kwamba hataki ufanye kazi
 
mjumbe nasoma maoni, nawaza mke wangu aje kuomba ushauri online hv namuacha siku hiyohiyo
 
kwa unyenyekevu na busara kubwa kaa na mume wako muongee na kuzungmza juu ya hayo...kama ni mtu mwelewa ataelewa tu na i think suluhisho litapatikana.....
 
Ninavyoona..mambo mengi huwa anaanza kumwambia dadake halafu mi ndo nafuatia au unakuta kingine hajaniambia bado kwenye story na dadake anajikuta kaniambia akidhani najua kumbe nakuwa sijui..ila siwezi kumjudge katika hili
Hapo umeliwa yaani sio vizuri kabisa na ndiyo unakosa mahutaji muhimu , huko wanashauriana kwanza, kwani huyo dada yeye hana mme mpaka anapata muda wakuongea na kaka yake hivyo asiongee na mmewe? Kaa chini na mmeo uongee naye taratibu huenda mazingira aliokulia
 
pole mama,,ila ulikosea sana kuacha kazi mapema bila kupewa msingi wa mtaji kwanza,,ilitakiwa akupe kwanza at least 10-15m ndio uache kazi,,sometimes sisi wanaume tuna porojo nyingi kwa wake zetu ila kuzitekeleza ndo inakua ngumu,,huyo jamaa alikua anatamani tangu cku nyingi ubaki nyumbani ulee familia,kifupi ni kwamba hataki ufanye kazi
Yaani kukaa nyumbani sio tatizo, lakini tatizo linalokuja mahitaji muhimu baba hawajibiki
ipasavyo kumuweka mke kama mtu waziada mbaya sana hiyo
 
Mkataba wangu wa kazi uliisha nikatafuta kazi sehemu nyingine nikapata,mme wangu akanishawishi kuwa mshahara ni mdogo kuliko Mwanzo halafu ni mbali na yeye so bora nijiajiri huku nikiangalia fam kwa ukaribu

Toka nimeacha kazi,nakosa hata pesa ya mahitaji yangu muhimu,mtaji nilioahidiwa siuoni,nna madeni chungu nzima coz nawasomesha wadogo zangu wawili walikoko college(jamaa hajawi hata kunisupport na anajua situation ya nyumbani kwetu) inaniuma sana pale mama yangu anaponiomba hata elfu 20 nakosa ya kumpa wakati nikiwa kazini nilikuwa nampa pesa nyingi na kuhudumia fam bila shida..

Roho inaniuma coz ninashuhudia jinsi mme wangu na wanafamilia wenzie wanavyopanga budget ya matumizi ya wazazi wao (kwa whattsapp family group na amount ili wawapelekee wazazi wao wakati mimi mama yangu hana kitu kabisa..kwa kweli nimekata tamaa na sijui hata nifanye ninikuna wakati natamani hata kurudi kwetu ili nikajipange upya na kuanza upya maisha yangu ila nafsi inakataa

Note:mme wangu hajawahi kunikosea ni mambo kama hayo tu ndo yanayoniumiza,halafu anapenda niende kwao tu,hataki niende kwetu na wakati njia ya kwenda kwao ni lazima upite mkoani kwetu na mara nyingi tunakuwa na private car but kupita anakuwa mgumu sana..hivi wanawake wenzangu mliopo kwenye ndoa situations kama hizi mnazihandle vipi?NISAIDIENI NAKUFA kwa MAWAZO

PS: NSSF nao wananizungusha kweli kunipa kapesa kangu kadogo,nina imani nikikapata katanisaidia kuinuka tena
Jaribu kutafuta mtu wa NSSF uongee nae akusaidie ku push your issue.

Hope you see the sun shining again, pole maa.
 
pole mama,,ila ulikosea sana kuacha kazi mapema bila kupewa msingi wa mtaji kwanza,,ilitakiwa akupe kwanza at least 10-15m ndio uache kazi,,sometimes sisi wanaume tuna porojo nyingi kwa wake zetu ila kuzitekeleza ndo inakua ngumu,,huyo jamaa alikua anatamani tangu cku nyingi ubaki nyumbani ulee familia,kifupi ni kwamba hataki ufanye kazi
Hapo kwenye kuwa na porojo nyingi ni sahihi kabisa. Kuna porojo unaweza kutamkiwa..... unabaki mdomo wazi. Unajifanya kama hujasikia hivi.... ili siku ipite.
 
umeoma mamaeee,mtuvumilie tu kwa kweli tulee familia
 
Kwa haraka kinachosumbua ni hela ya mama na wadogo zako, vitu ambavyo mumeo ni ngumu kutimiza kwa 100% ,hakuna hali ngumu hapo ila ni huruma yako tu ndio inatengeneza hiyo hali.
 
na na QUOTE="La Princesa, post: 33009424, member: 190145"]
Mkataba wangu wa kazi uliisha nikatafuta kazi sehemu nyingine nikapata,mme wangu akanishawishi kuwa mshahara ni mdogo kuliko Mwanzo halafu ni mbali na yeye so bora nijiajiri huku nikiangalia fam kwa ukaribu

Toka nimeacha kazi,nakosa hata pesa ya mahitaji yangu muhimu,mtaji nilioahidiwa siuoni,nna madeni chungu nzima coz nawasomesha wadogo zangu wawili walikoko college(jamaa hajawi hata kunisupport na anajua situation ya nyumbani kwetu) inaniuma sana pale mama yangu anaponiomba hata elfu 20 nakosa ya kumpa wakati nikiwa kazini nilikuwa nampa pesa nyingi na kuhudumia fam bila shida..

Roho inaniuma coz ninashuhudia jinsi mme wangu na wanafamilia wenzie wanavyopanga budget ya matumizi ya wazazi wao (kwa whattsapp family group na amount ili wawapelekee wazazi wao wakati mimi mama yangu hana kitu kabisa..kwa kweli nimekata tamaa na sijui hata nifanye nini😭😭kuna wakati natamani hata kurudi kwetu ili nikajipange upya na kuanza upya maisha yangu ila nafsi inakataa

Note:mme wangu hajawahi kunikosea ni mambo kama hayo tu ndo yanayoniumiza,halafu anapenda niende kwao tu,hataki niende kwetu na wakati njia ya kwenda kwao ni lazima upite mkoani kwetu na mara nyingi tunakuwa na private car but kupita anakuwa mgumu sana..hivi wanawake wenzangu mliopo kwenye ndoa situations kama hizi mnazihandle vipi?NISAIDIENI NAKUFA kwa MAWAZO

PS: NSSF nao wananizungusha kweli kunipa kapesa kangu kadogo,nina imani nikikapata katanisaidia kuinuka tena
[/QUOTE]
Dada yangu kwanza kabisa pole na Hall hiyo uliyokuwa nayo. Kama ambavyo kuna mchangiaji kachangia ni kwamba unahitaji ushauri kutoka kwa watu wenye hekima na uzoefu kwenye mambo ya ndoa na pili unahitaji hekima ya hali ya juu kupima ushauri unaopewa humu.

Ipo hivi, unapoamua kuolewa maana yake unaachana na familia ya nyumbani kwenu na 95% ya akili yako inatakiwa kufikiria maisha ya ndoa yako ndiyo maana wakristo wanaambiawa MTU ATAMUACHA BABA YAKE NA MAMA YAKE NA KUAMBATANA NA MKEWE NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA.Maana yake ni kwamba kusomesha wadogo zako kimsingi sio jukumu lako,ni msaada ambao unautoa pale tu ambapo hauathiri ndoa yako. Maana hayo ni maisha ya wadogo zako ambapo mwenye jukumu ni wazazi wako.Hao wadogo zako wakimaliza vyuo huwezi kuwalazimisha kusomesha wanao utabaki mzigo wako na mumeo.

Mumeo aliamua uache kazi baada ya kuona kazi yako haina faida kwenye ndoa yenu,maana amekupa muda ufanye kazi pengine akirudi nyumbani umechelewa kazini kuna huduma anazikosa but kinachopatikana kinapelekwa kusikojulikana.

Kuhusu mama yako hiyo ni haki kusaidiwa na mumeo. Kama walivyoshauri wenzangu kaa na mumeo mwekeze kuwa mama yako kwa sasa kiuchumi hajiwezi na kwamba anahitaji msaada wenu( sio wako) kama watoto wake. Tumia rugha ya heshima na liache jambo hilo kwake sio kwako tens. Yaani acha awe anatuma yeye hizo pesa kwa mama yako. Mfanye awe Karibu na mama yako.

Kuhusu kufanya kazi tena ni vizuri but usifosi ongea nae taratibu. Uwe kama unaeomba na sio unaedai, mwambie kuwa unatamani kumsaidia maana unaona majukumu ya familia ni mengi, ( Ila usigusie matatizo ya wadogo zako). Dada yangu sisi wanaume tulip oa hatupendi wake zetu Ku concentrate sana kwao, tunapenda kuona akili zao zinawaza familia. Hizo mama mama, mara wadogo zangu dada yangu zitakupotezea ndoa na hata ukiolewa mahali pengine utayakuta hayohayo.

Tuulize sisi tumesomesha wadogo zetu hata vocha hawezi kukununulia na ana masters. Hangaika na wanao na mumeo na wazazi wanu basi.

Asante
 
HUU USIPOUANGALIA VIZURI, NA UKIUSIKILIZA SAAANA USHAURI WA WANAWAKE WENZAKO AU VIJANA AMBAO HAWAJAOA AU NDOA ZAO BADO CHANGA NDIYO MWANZO WA KUVUNJIKA NDOA YAKO.

KUWA MAKINI SANA. NIMESOMA HISIA ZAKO, NA NIMESOMA USHAURI AMBAO WATU WENGI WAMEKUSHAURI, DADA YANGU WENGI WANEKUPOTOSHA WACHACHE WAMEKUAMBIA UKWELI. SEMA SHIDA UNAAMINI KWENYE HISIA ZAKO MNO. YAANI UNAOMBA USHAURI HUKU UNA MAAMUZI TAYARI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom