Naitazama Hoteli ya Kiromo View Resort kwa Uchungu

Naitazama Hoteli ya Kiromo View Resort kwa Uchungu

Sawa na uwekezaji wa serikali kwenye kiwanda Cha kuzuia mazalia ya mbu pale Kibaha. Kinaitwa Tanzania biotech products Limited
Kwamba kwenye kujenga hicho kiwanda cha Tanzania Biotech Products Ltd serikali nayo ilijipanga kama alivyofanya Bakheresa kwenye ujenzi wa hiyo Verde hotel? Mbona huu ni mzaha sasa.
 
Mleta mada nimekuelewa vizuri na naunga mkono hoja, lazima sisi kama nchi tuwe na MIKAKATI + KITENGO kwa ajili ya kuwaongoza na kuwasupport wawekezaji wazawa kama huyu Kiromo

Binafsi niliumia na naendelea kuumia kuona mahotel ya Marehemu Bilionaire Mrema kama Ngurdoto et al kuwa vile yalivyo

Nchi yenye vitanda vichache kwa ajili ya wageni/ watalii, nchi yenye changamoto ya ajira haikuwa busara kuziachia zile hotels,
INGAWA nasikia Ngurdoto yenyewe imepata mwekezezaji, wish na zingine zipate huo uwekezaji
 
Kila Biashara huwa ina changamoto. Ila Biashara ya hotel huwa ni ngumu mno.


Hata matajiri wakubwa tz wanaiogopa. Mo mwenyewe na utajiri wake hana hoteli [emoji1787][emoji1787]

Hata gsm hana hoteli [emoji1787]

Bakhresa kajenga hoteli ya kitalii Zanzibar inaitwa verde. Ila ile hoteli inabebwa na location na sekta ya utalii. Hapo watu azam walipiga hesabu kali mno.


Wengine wanajenga hoteli/lodge/guest. Ili wakopesheke kiurahisi na mabenki ya kitanzania hasa NMB,Crdb,NBC na Benki ya posta(TCB). Ndio maana matajiri wengi wa level ya mkoa au wilaya huwa wana lodge, hotel. Huwa ni "MAELEKEZO" toka benki wanazotumia kukopea hela hasa kuwa na kigezo cha mali isiyohamishika. Fanya utafiti kisha connect dots

Nimekupata vizuri sana mkuu
 
View attachment 2841395

Leo nipo safarini kuelekea Dar es salaam kupitia route ya Msata-Bagamoyo. Nimepita hotel ya kitalii ya KIROMO VIEW RESORT ambayo ilizinduliwa na Kikwete mwaka 2009.

Hivi sasa yamebaki maghofu chakavu tu. Sifahamu ni sababu zipi zilimfanya muwekezaji ashindwe kuendeleza uwekezaji ule, ila naamini kabisa sera za uwekezaji ni changamoto Tanzania.

Uwekezaji Tanzania unategemea ni nani yupo madarakani. Hatuongozwi na sera wala sheria bali mihemko ya atakaeingia madarakani.

NB: KIROMO inawakilisha biashara nyingi zilizokufa kutokana na kukosekana kwa sera thabiti za uwekezaji.

Mungu iponye Tanzania.
Mkuu.. Mkoa wa pwani mgumu sanaa... Hata watalii hamna, hata biashara sio kivilee.. Nawasilisha
 
Hongera kwa uchambuzi mzuri.

Biashara ya hotel huwa ni ngumu sana. Inahitaji akili, pesa, ubunifu na management nzuri.
Usione vyaelea, vimeundwa
Na hoteli nyingi hapa Tz huwa zinafeli kiaina hiyo. Huwa zinaanza vizuri kidogo lakini baadae huduma zinakuwa mbovu wateja wanaanza kuhama.

Hiyo hoteli ya Kiromo tulishakwenda mara mbili tatu za mwanzo, na kila tulipokuwa tunakwenda huduma zilizidi kuharibika, mwisho tulihama kabisa.

Nakubaliana na baadhi wa waandishi wa humu kwa kweli hoteli/lodges nyingi za eneo la Bagamoyo zimefeli kutokana na huduma mbovu hasa kwa wale wanaotumia vijana wenyeji wa pale, yaani hawako serious kabisa kabisa.
 
Back
Top Bottom