Naitazama Hoteli ya Kiromo View Resort kwa Uchungu

Naitazama Hoteli ya Kiromo View Resort kwa Uchungu

Haramu kibaya,

Niliwahi kulala hapo Hoteli aikuwa na standard, huduma ziilikua mbovu mbaya zaidi Location aliojenga aikuwa sahihi

Ilipaswa kuwa Gest house na sio hotel
Wewe ukuwai(aikuwa) kulala apo(aikuwa), si hajabu(ajabu) na mwalimu wako naye kama wewe.
 
Bongo watu huwa wanajianzishia tu biashara bila utafiti
 
View attachment 2841395

Leo nipo safarini kuelekea Dar es salaam kupitia route ya Msata-Bagamoyo. Nimepita hotel ya kitalii ya KIROMO VIEW RESORT ambayo ilizinduliwa na Kikwete mwaka 2009.

Hivi sasa yamebaki maghofu chakavu tu. Sifahamu ni sababu zipi zilimfanya muwekezaji ashindwe kuendeleza uwekezaji ule, ila naamini kabisa sera za uwekezaji ni changamoto Tanzania.

Uwekezaji Tanzania unategemea ni nani yupo madarakani. Hatuongozwi na sera wala sheria bali mihemko ya atakaeingia madarakani.

NB: KIROMO inawakilisha biashara nyingi zilizokufa kutokana na kukosekana kwa sera thabiti za uwekezaji.

Mungu iponye Tanzania.
Sera ya Uwekazaji Tanzania ni ovyo kabisa ndio maana wawekazaji wengi hawaamini kuja kuekeza TZ inategemea nani yuko madarakani akiondoka unawezwa kufanya chochote au hata kufilisiwa kila kitu labda utie mkataba wa kimataifa hapo kdg unaweza kufanikisha.
 
Bongo watu uwekeza kwa upepo na sio utafiti wa kina

Pale kabla ujafika Chalinze Nako Kuna kalodge ka makuti kilijengwa Enzi za Da gama kishajifia

Biashara zinazoongoza kufa Tanzania ni Hoteli, Bar, Kumbi

Location mbovu, Management mazoea, Poor standard
Sahihi sana, hasa hapo kwenye management mazoea na huduma mbovu za wahadumu.
 
Kila Biashara huwa ina changamoto. Ila Biashara ya hotel huwa ni ngumu mno.


Hata matajiri wakubwa tz wanaiogopa. Mo mwenyewe na utajiri wake hana hoteli 🤣🤣

Hata gsm hana hoteli 🤣

Bakhresa kajenga hoteli ya kitalii Zanzibar inaitwa verde. Ila ile hoteli inabebwa na location na sekta ya utalii. Hapo watu azam walipiga hesabu kali mno.


Wengine wanajenga hoteli/lodge/guest. Ili wakopesheke kiurahisi na mabenki ya kitanzania hasa NMB,Crdb,NBC na Benki ya posta(TCB). Ndio maana matajiri wengi wa level ya mkoa au wilaya huwa wana lodge, hotel. Huwa ni "MAELEKEZO" toka benki wanazotumia kukopea hela hasa kuwa na kigezo cha mali isiyohamishika. Fanya utafiti kisha connect dots
Sahihi, biashara ya Hotel bongo inataka usimamizi wa karibu sana wa mmiliki, ukimuachia manager na wafanyakazi wake tu utakuta wamepageuza danguro uchwara, kijiwe cha mabishano ya mpira na umbea wa mitaani huku wahadumu slow wakitoa huduma mbovu kuliko kwa nyodo na kukesha instagram muda wa kazi.
 
Ukimwita mara 3 tatu anasema bwana wee usinisumbue
Shida tupu, na ukiwalekeza jinsi ya kutoa huduma stahiki ukirudi kesho yake unaona wanabishana na kusukumana nani aje kukuhudumia.
 
Nimeamini watanzania wengi ni wajuaji.

Hii story humu kila mtu anasema lake.
Kiufupi mmoja wa wamiliki wa hii hoteli alifariki na alikua ni mhaya mmoja hivi. Wengine wapo wanaendelea na mishe zingine
Kufa kwa mhaya mmoja ndiyo hoteli ife nayo? Haiwezekani hayo ni matatizo ya masifa ya wahaya tu
 
Muwe mnakuja na habari kamili hata ikibidi mnamtafuta mwenyewe au hata kufanya uchunguzi hapo hapo
Lakini sasa ukitaka kusikia speculation endelea kusoma
Umeweka picha ngoja zitungiwe mashairi
 
View attachment 2841395

Leo nipo safarini kuelekea Dar es salaam kupitia route ya Msata-Bagamoyo. Nimepita hotel ya kitalii ya KIROMO VIEW RESORT ambayo ilizinduliwa na Kikwete mwaka 2009.

Hivi sasa yamebaki maghofu chakavu tu. Sifahamu ni sababu zipi zilimfanya muwekezaji ashindwe kuendeleza uwekezaji ule, ila naamini kabisa sera za uwekezaji ni changamoto Tanzania.

Uwekezaji Tanzania unategemea ni nani yupo madarakani. Hatuongozwi na sera wala sheria bali mihemko ya atakaeingia madarakani.

NB: KIROMO inawakilisha biashara nyingi zilizokufa kutokana na kukosekana kwa sera thabiti za uwekezaji.

Mungu iponye Tanzania.
Kazi ya Mwendazake hiyo
 
Back
Top Bottom