Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,629
- 13,551
Kila Biashara huwa ina changamoto. Ila Biashara ya hotel huwa ni ngumu mno.Kiromo imekufa kwa sababu ya mismanagement ya mwenye mali. Sitaki kuingia mambo ya makabila, lakini yule Mhaya alikuwa na matatizo ya kihaya kwenye biashara. Angekuwa mchagga pale ungeshangaa.
Hata matajiri wakubwa tz wanaiogopa. Mo mwenyewe na utajiri wake hana hoteli 🤣🤣
Hata gsm hana hoteli 🤣
Bakhresa kajenga hoteli ya kitalii Zanzibar inaitwa verde. Ila ile hoteli inabebwa na location na sekta ya utalii. Hapo watu azam walipiga hesabu kali mno.
Wengine wanajenga hoteli/lodge/guest. Ili wakopesheke kiurahisi na mabenki ya kitanzania hasa NMB,Crdb,NBC na Benki ya posta(TCB). Ndio maana matajiri wengi wa level ya mkoa au wilaya huwa wana lodge, hotel. Huwa ni "MAELEKEZO" toka benki wanazotumia kukopea hela hasa kuwa na kigezo cha mali isiyohamishika. Fanya utafiti kisha connect dots