Bin Chuma75
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 1,003
- 1,102
Wakuu, mi ninamtoto nilikuwa namlea baada ya wazazi wake kushindwa kumlea tangu mdogo, na bahati mbaya hata hao wazazi kwa sasa hawajulikani hata walipo sababu waliachana na kila mmoja wao akapotelea anakujua mwenyewe, sasa huyu mtoto nimemsomesha shule za private kuanzia awali mpaka kidato cha nne, uwezo wangu wa msaada wa kielimu ukaishia hapo, kidato cha 5 na 6 nikampeleka shule ya serikali, sasa, sasa naomba kujua ni njia gani naweza kufanya huyu kijana aweze kupata mkopo wa elimu ya juu? Maana nasikia moja wapo ya kigezo cha kukosa mkopo ni kusomeshwa shule za private.
NB: mimi ni mlezi tu nilietoa mchango wangu kwake, na wazazi wake halisi hawajulikani walipo kwa sasa.
NB: mimi ni mlezi tu nilietoa mchango wangu kwake, na wazazi wake halisi hawajulikani walipo kwa sasa.