Kibajaji01
Member
- Sep 22, 2023
- 15
- 39
Wakuu naombeni msaada wenu wa kimawazo kwenye hili.
Mimi ni mwalimu wa physics na chemistry ila sijabahatika kupata ajira serikalini, sasa kuna shule mbili nafundisha let say shule X na shule Y. Shule X nalipwa laki tatu, wakati shule Y nalipwa 250,000/=
Shida inapokuja shule Y wanao nilipa 250 wao hawana shida walinambia sababu ya hela wanayonipa ni ndogo basi niwe naenda muda wa vipindi tu kufundisha na kuondoka, ila hawa shule X wanaonipa 300 wao hawataki nifundishe shule nyingine tofauti na wao, yaani niwepo kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi, Jumatatu hadi Ijumaa tunatoka saa 11 isipokua Jumamosi tu ndio tunatoka saa nane mchana.
Sasa wiki hii shule X wameniita na kuniambia nichague shule moja nitakayo fanya kazi. Naombeni ushauri wakuu, nibaki na hii ya 250 niwe naenda muda wa vipindi tu ambapo ni siku tatu kwa wiki au niendelee na shule X ya 300?