Ridhiwani Kikwete: Serikali kuwabeba watumishi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu.

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
316
410
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema serikali imeendelea kutoa motisha ya kifedha na isiyo ya kifedha kwa watumishi wote ikiwemo watumishi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu kwa kuboresha viwango vya posho ya kazi baada ya masaa ya kazi, posho ya kujikimu wakati wa kusafiri, posho ya mawasiliano, kufikisha huduma ya umeme katika maeneo yao, kutoa magodoro, kutoa nyumba za walimu zenye staha na mengine mengi.

Kikwete ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wiki hii wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro, Anne Kilango Malecela aliyetaka kujua mkakati wa serikali kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu.

"Halmashauri zilizopo kwenye maeneo yenye mazingira magumu, kwa kutambua umuhimu wa kutoa motisha serikali inatekeleza mpango wake wa motisha kwa kufuata miongozo inayotoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kusimamia utoaji motisha mbalimbali kwa watumishi hao kutokana na hali na mazingira magumu ya sehemu wanakofanyia kazi." Alisema Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete.

Naibu Waziri Kikwete, akijibu swali la nyongeza la Mbunge Malecela aliyesema Jimbo lake lina mazingira magumu hasa uwepo wa milima na kuitaka serikali kwenda kuangalia mazingira ya watumishi na kuona namna ya kuwapa motisha zaidi ya kufanya kazi, amesema:-

"Nikuhakikishie Mbunge (Melecela) na Bunge hili tukufu kwamba serikali iko bega kwa bega nae kuhakikisha mazingira ya watumishi wake yanakwenda kurekebishwa. Mwaka 2020/2021 serikali iliteua tume ya wataalamu ambao walikwenda mikoa 27, halmashauri 117, manispaa 5, miji 4, majiji 4 pamoja na tarafa na miji mbalimbali ili kuangalia na kujiridhisha mazingira magumu ya watumishi na mazingira magumu yalionekana na ndiyo maana sasa serikali inajipanga kufika halmashauri yako (Same) na kote nchini ili kurekebisha mazingira ya watumishi wanaofanya kazi mazingira magumu.

Akiongeza majibu ya Naibu Waziri wake, Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene amesema suala la motisha ni haki kisheria kwa watumishi wote na kwamba mamlaka za serikali za mitaa kupitia halmashauri zake zote zina wajibu wa kutoa motisha kwa watumishi wake kwenye maeneo yao kwasababu wao wanawajua zaidi watumishi na mazingira yao.
 
Attachments

  • IMG-20231111-WA0001.jpg
    IMG-20231111-WA0001.jpg
    109 KB · Views: 5
  • IMG-20231111-WA0002.jpg
    IMG-20231111-WA0002.jpg
    188.9 KB · Views: 5

Mmmmmm upuuzi mtupuu na iongo uliopitilizaaa.....low IQ
 
Ha! Ha! Ha! ni sound hizo

Watumishi wa ngazi za chini wa Halmashauri wakitaka maslahi mazuri (house allowance, transport allowance, meals allowance, communication allowance, nakadhalika) kama ilivyo kwenye taasisi za umma na kwa viongozi ni waipige chini CCM, wakianza na uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 na kisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
 
Watumishi wote ni waiga fitna wasaliti waoga 200% hawana msimamo.....hata!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom