Naibu Waziri Mambo ya Ndani afika eneo la ajali ya Treni na Basi iliyoua watu 13, Novemba 29, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,103
12,566
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ametembelea eneo ambalo kumetokea ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ally’s Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha Treni katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya Mji wa Manyoni Mkoani Singida.

Awali, akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida, ACP Stella Mutabihirwa amesema imesababisha vifo vya Watu 13 na kujeruhi wengine 34.

ACP Stella Mutabihirwa amesema “Ajali imetokea leo Novemba 29, 2023 Saa 10 Alfajiri, basi lilikuwa na Watu 57, idadi hiyo ya majeruhi na vifo ni mpaka muda wa asubuhi.

Ameongeza “Kichwa cha Treni kilichohusika kina Namba za Usajili V1951-9006, kilikuwa kikitokea Itigi kuelekea Manyoni.”

a3c0fda6-1a90-4faf-a40c-5dd679891046.jpg

ba40d62f-d01a-4797-81b2-d54a374e7e51.jpg

e0376db2-131c-4b69-9462-3b62108f1619.jpg

b99e5e13-c428-4e2e-9c85-0add2d0669a8.jpg

SII.JPG

SI.JPG
 
Dah,,, hivi dereva mpaka unagonga kichwa cha treni na njia hiyo kila siku unapita huu ni uzembe wa kiwango gani
 
Ila hii nchi viongozi hawana mawazo kabisa,juzi imetokea ajali ya bus la baraka imeua watu wengi,hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa!leo imetokea hii ya allystars imeua watu 13,utashangaa inapita kimya!Mungu tu atusaidie kwa kweli
 
Halafu kwenye train za umeme watanzania wanataka kuanza na train zenye speed ya 160km/ph

Hiyo tu ya 30km/ph kila mwaka ajali na miundombinu yenyewe ku-maintain mtihani. Ni mwaka huu tu ndio sijasikia njia aijaondoka mvua.

Train tunazolilia speed yake unaiona ile, mara hii hapa; kasheshe wafugaji, watoto wanaokatiza njia ya reli na ujuaji wetu.

Busara ni kuanza na train zenye speed ndogo kwanza jamaa wapate uzoefu kabla ya kukimbilia train za 160km/ph kisa miundombinu SGR inaruhusu.
 
Ya umeme itapita juu ya barabara
 
Back
Top Bottom