Bus la Ally's lagonga Kichwa cha Treni Manyoni Singida, Watu 13 wafariki Dunia, 25 wajeruhiwa

Minjingu Jingu

Senior Member
Nov 2, 2023
116
477
Ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ally's Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha Treni katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya Mji wa Manyoni Mkoani Singida, imesababisha vifo vya Watu 13 na kujeruhi wengine 25.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida, ACP Stella Mutabihirwa amesema “Ajali imetokea leo Novemba 29, 2023 Saa 10 Alfajiri, basi lilikuwa na Watu 57, idadi ya majeruhi na vifo ni mpaka muda huu (asubuhi), kichwa cha Treni kilichohusika kina namba za usajili V1951-9006 kilikuwa kikitokea Itigi kuelekea Manyoni.”

trc1.JPG
============

Kwa masikitiko makubwa,, majonzi na huzuni naandika uzi huu kuwatangazia ajali mbaya iliyotokea eneo la Manyoni ukitoka Dodoma kabla ya kufika round about kati ya Bus la Allys lenye number ya usajili T 178 DVB na Kichwa Cha Train.

Sikupenda kupiga picha kutokana na hali ya huzuni, majonzi, kilio na maumivu makali ambayo wanapitia abiria manusura. Huku wakiwa wamezungukwa na maiti zikiwemo za watoto na watu wazima.

Ni hali ya kutisha mpaka kichwa cha train kimehama kabisa katika njia yake na bus limepinduka na kupondeka vibaya sana Ubavuni.

Police wanaendelea kuchukua manusura na maiti kupeleka Hospital ya karibu hapa Singida.

Chanzo inasemekana ni kichwa cha train kupita kikiwa hakijawasha taa wala kupiga horn. Na inasemwa hii si mara ya kwanza. Na mpaka hapo kichwa kinaonekana taa ikiwa haijawaka. Kinanguruma tu.

IMG_20231129_051232.jpg

======

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani, baada ya basi la Kampuni ya Ally's Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, kugonga treni ya mizigo katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya mji wa Manyoni, mkoani Singida, leo Novemba 29, 2023 majira ya saa 11 alfajiri.

20231129_081820.jpg
20231129_081826.jpg
20231129_081831.jpg
20231129_081922.jpg
 
Sasa na wewe Ingia kwenye zoezi la kusaidia wahanga badala ya kuwa bize na mitandaoni.

Habari zitapatikana tu.
Ushauri mzuri sana.Kuna mtu/watu unakuta yupo/wapo bize kupiga picha ya mtu /watu anayehangaika/wanaohangaika ktk ajari badala ya kumsaidia/kuwasaidia,kwa kweli bado tuna safari ndefu.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom