Naibu Waziri Kihenzile Akutana na Watendaji TCAA, Awasisitiza Kufanyia Kazi Hoja za CAG

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,858
930

Naibu Waziri Kihenzile Akutana na Watendaji TCAA, Awasisitiza Kufanyia Kazi Hoja za CAG

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile (Mb) ameonana na watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Anga (TCAA) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Ndugu Hamza Johari.

Naibu Waziri Kihenzile amewapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya sambamba na kuwezesha Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) kuwa miongoni mwa Vyuo 9 bora Afrika na Vyuo 35 Duniani kwenye utoaji elimu ya Usafiri wa Anga.

Naibu Waziri Kihenzile amejitambulisha na Kama ilivyo ada kufikisha salam za Wizara iliyo chini ya Waziri Mhe. Prof. Makame Mbarawa na kuwasihi kuongeza kasi ya Kuongeza Mashirki ya Ndege ya ndani na Nje ya Nchi ili kuwezesha hitaji la usafiri wa Anga Nchini kupungua.

Aidha, Mhe. Kihenzile amewaelekeza kuendelea kusimamia Usafiri wa Anga kwa weledi zaidi ili kuendelea kudhibiti ajali za Ndege sambamba na kusimamia Maagizo ya Viongozi, kujipanga kushughulika na Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Vilevile, Kihenzile amewaasa TCAA kukaa na mashirika yanayotoa huduma ya usafiri wa Anga ili kufanyia kazi changamoto zinazotolewa na abiria ikiwemo kuahirishaahirisha safari kwa baadhi ya mashirka ya Ndege.
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.53(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.54.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.52.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.52(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.53(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.53.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.54(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 18.42.55.jpeg
 
Back
Top Bottom