Airport ya Iringa Kufungua Utalii Kusini, Ujenzi Wafikia 82% - Naibu Waziri Kihenzile

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,899
944

AIRPOT YA IRINGA KUFUNGUA UTALII KUSINI, UJENZI WAFIKIA 82% - NAIBU WAZIRI KIHENZILE

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Mwakiposa Kihenzile amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kufufua Uwanja wa Ndege wa Iringa na kuujenga kwa kiwango cha Kisasa ili kuinua Utalii wa Kusini.

Mhe. Kihenzile amesema Uwanja huo unaunganisha dunia na Hifadhii kubwa Kimataifa ya Ruaha National Park. Akizungumza baada ya kutembelea uwanja huo Naibu Waziri Kihenzile alipongeza TANROAD na TAA kwa usimamizi wa ujenzi ambao mpaka sasa umefikia 82%.

Aidha, alieleza kuwa Sambamba na ujenzi huo, Rais Samia anajenga barabara ya Ruaha National Park kiwango cha lami ili kuhakikisha utalii huo unakuwa wa kisasa.

Ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Nduli kilichopo mkoani Iringa umefikia asilimia 82 huku kikitarajiwa kumalizika mwishoni wa mwezi Desemba 2023

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema hayo baada ya kutembelea kiwanja hicho ambacho kilichogharimu zaidi ya bilioni 63.7 ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wake.

Kihenzile amesema ujenzi wa kiwanja hichi cha ndege kitasaidia kuinua uchumi wa wakazi wa Mkoa wa Iringa kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii ambapo Naibu Waziri Kihenzile amesema wanaendelea kuboresha ukarabati wa viwanja vyote nchini ili kuendelea kukuza uchumi.
 

Attachments

  • F96J_nSWsAAoY1c.jpg
    F96J_nSWsAAoY1c.jpg
    98.9 KB · Views: 11
  • F96J_nZXcAAGSAP.jpg
    F96J_nZXcAAGSAP.jpg
    86.4 KB · Views: 12
  • DSC_2253.JPG
    DSC_2253.JPG
    1.1 MB · Views: 11
  • DSC_2258.JPG
    DSC_2258.JPG
    1.7 MB · Views: 11
  • DSC_2270.JPG
    DSC_2270.JPG
    979.4 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-11-01 at 10.42.57(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-01 at 10.42.57(1).jpeg
    30.5 KB · Views: 8
Back
Top Bottom